Wauguzi 6 watiwa hatiani kwa kusababisha Mama kukosa Mtoto kwa Uzembe

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) limewataka  Wauguzi wanaojijua kuwa wanatumia vyeti feki  popote walipo nchini kujisalimisha mara moja kabla halijaamua kuwafuata huko waliko.

Hayo yamesemwa na Msajili wa TNMC Bi. Agnes Mtawa ambapo amebainisha kwamba katika kikao cha 193 kilichofanywa na Baraza hilo limewabaini watu 15 wanaojitambulisha kuwa ni wauguzi lakini kanzi data ya Baraza hilo imeonesha kuwa vyeti hivyo siyo halali na leseni wanazotumia ni za kugushi.

Amesema kuwa  Baraza limejadili suala la baadhi ya watu wanaogushi vyeti na leseni za taaluma ya uuguzi na ukunga ambapo limebaini kuwa katika robo mwaka Aprili - Juni, 2018 watu watano walitambuliwa kugushi vyeti na leseni hivyo wamepelekwa kwenye vyombo vya dola ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Pamoja na Baraza limewapa onyo kali Wauguzi Wakunga sita katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa kushindwa kutimiza majukumu yao ya kitaaluma wakati wakitoa huduma kwa mgonjwa hali ambayo ilipelekea mama mjamzito kupoteza mtoto kwa sababu ya uzembe.


from MPEKUZI

Comments