Wapinzani waipigia kura ya hapana bajeti Kuu ya Serikali

Wabunge wanane wa CUF wanaomuunga mkono Ibrahim Lipumba wameipiga kura ya ‘ndio’ Bajeti ya Serikali ya mwaka 2018/19 ya Sh32.45 trilioni.

Kati ya wabunge hao wawili ni wa majimbo ambao ni Maftaha Nachuma (Mtwara Mjini) na Magdalena Sakaya (Kaliua).

Wangine sita ni wa Viti Maalum ambao ni; Zainab Mndolwa, Alfredina Kahigi, Rukia Kassim, Nuru Bafadhili, Kiza Mayeye, Rehema Migilla.

Kura zao za ‘ndio’ zimeshangiliwa na wabunge wengine wa CCM ambao wengine waligonga meza huku wakisimama kuwashangilia.

Sakaya yeye amepiga kura  huku akisema; “‘ndio kwa maendeleo ya wana Kaliua.”

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Jacqueline Ngonyani ‘Msongozi’ alipoitwa yeye alianza kwa kupiga vigele gele kisha akasema;  ‘ndiooooo’ na kuendelea kupiga vigelegele jambo lililoibua shangwe ndani ya ukumbi huo hasa kutoka upande wa CCM.

Kura za wabunge wa CCM walioshangiliwa mara baada ya kusema ‘ndio’ ni za Hussein Bashe (Nzega Mjini), Nape Nnauye (Mtama), na Abdallah Bulembo (Kuteuliwa).

Jina la Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu lilipoitwa wabunge walikaa kimya kwa muda huku  minong’ono ikisikika kwa mbali.

Mawaziri ambao hawakuwapo ni; Dk Augustine Mahiga (Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa) na Profesa Palamagamba Kabudi wa Katiba na Sheria.

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe amekuwa miongoni mwa wabunge wa upinzani ambao hawakuwepo bungeni.


from MPEKUZI

Comments