Rais Magufuli afurahishwa na Tuzo ya Grace

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amefurahishwa na ushindi alioupta mjasiriamali Dr. Elizabeth Kilili ambaye amepata tuzo nchini Marekani kupitia bidhaa zake za 'Grace product'.

Rais Magufuli ameeleza furaha yake hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ambapo zaidi amesifu namna ambavyo Dr. Elizabeth alitumia fursa hiyo kukitangaza Kiswahili baada ya kukitumia wakati akishukuru umati wa watu waliokuwepo ukumbini.

Sherehe za utoaji tuzo hizo maarufu kama 'International Quality summit' kwa mwaka 2018 zilifanyika May 27-28 2018, jijini New York nchini Marekani. Tuzo hizo ambazo hutolewa kwa makundi maalum ikiwemo viongozi pamoja na wazalishaji wa bidhaa asili zimefanyika kwa mara ya 32.

''Nimefurahishwa na ushindi wa Grace Products, lakini pia  nimefurahishwa kwa kutumia Kiswahili kukizungumza nchini Marekani, hongereni sana Grace Products''. ameandika Rais.

Kwa upande wake Dr. Elizabeth ameeleza kufurahishwa na pongezi hizo za Mh. Rais, huku akisema zimempa changamoto ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kwenda sambamba na falsafa ya Rais ambayo ni Tanzania ya viwanda.


from MPEKUZI

Comments