Bunge lahairishwa rasmi hadi Septemba

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa hoja ya kuahirishwa kwa mkutano wa 11 wa Bunge la Bajeti ulioanza Aprili 3 na kumalizika leo Ijumaa Juni 29, 2018.

Akiwasilisha hoja hiyo leo bungeni, Majaliwa amesema maswali 530 ya msingi na 1705 ya nyongeza yameulizwa na wabunge.

Pamoja na mambo mengine, Majaliwa amezungumzia masuala mbalimbali, zikiwemo halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 ya mikopo kwa ajili ya vijana, wanawake na wenye ulemavu na zisaidie uundaji wa Saccos shirikishi za makundi.

Kuhusu uchangiaji damu, amewaomba wananchi kujenga utamaduni wa kuchangia damu ili kuwezesha upatikanaji wa damu kwa wingi kwa wenye uhitaji.

Akizungumzia Virusi vya Ukimwi na kampeni ya upimaji Ukimwi ya Furaha Yangu, amesema hadi kufikia Machi, 2018 watu wanaoishi na VVU walikuwa milioni 1.02, kati yao watu milioni 1.0 walikuwa wanatumia dawa za kufubaza virusi hivyo.

Kwa upande wake, Spika wa Bunge Job Ndugai amesema, “tumemaliza Bunge hili maarufu la korosho na kuliwaka kweli kweli, Serikali imetuambia tuiamini na nafikiri mambo yatakwenda muswano.”


from MPEKUZI

Comments