Undani wa Tukio la Mhadhiri UDOM Kuuawa Kwa Kuchomwa Kisu na Mumewe

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Rose Mndenye ( 31) inadaiwa ameuawa na mume wake kwa kile kinachodaiwa ni sababu za  wivu wa mapenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk Caroline Damiani alisema walimpokea marehemu hiyo jana usiku saa 5.30 usiku.

Dk Damian alisema Mdenye alifikishwa hospitali hapo akiwa tayari ameshafariki dunia huku akiwa na majeraha makubwa katika mwili wake.

Alisema mwili wa marehemu alifikishwa hospitalini hapo akitokea katika eneo la Swaswa umbali wa kilometa 15 kutoka katika ya Jiji la Dodoma.

“Tulimpokea jana usiku saa 5.30 usiku, alikuwa tayari ameshafariki,alikuwa na majeraha sehemu za mwili  wake,”alisema.

Naye Ofisa Uhusiano wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Beatrice Mtenga alisema walipata taarifa za mhadhiri huyo kuchomwa kisu na mume wake jana usiku.

“Tulipata taarifa jana na sababu ya kifo ni kuchomwa na kisu na muwe wake sababu za wivu wa mapenzi,”alisema.

Mtenga alipohojiwa kama anamjua mumewe alisema kwamba hawamjui lakini wanaendelea kutafuta habari zake na watatoa taarifa baadaye.

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi wa Jiji la Dodoma, Gilles Muroto,alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, huku akidai kwamba Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi  kuhusu chanzo cha kifo ni nini.

Taarifa kutoka nyumbani kwao Swaswa zinasema kwamba Mdenya aliuawa na mumewe ambaye ni Mchungaji  wa Kanisa la TAG katika eneo la Swaswa, John Mwaisango na alimwua mkewe saa 2.27 akiwa jikoni.

Akizungumza mkwe wa marehemu, Lamra Ngenzi, alisema chanzo cha kifo chake hajajua kilichosababisha mkwe wake kuuawa na mumewe.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo (UDOM) anayeshughulikia Fedha, Utawala na Mipango, Adam Mwakalobo alisema amepokea taarifa za kufariki Mdenye jana usiku saa 4.45.

Mwakalobo alieanda hospitali na walipokea mwili wa marehemu ambaye alikuwa akifundisha chuo hicho tangu 2011 kama mhadhiri msaidizi wa idara ya Utawala wa Biashara.

Mdenye alikuwa mhadhiri wa kompyuta baada ya kusoma shahada ya kompyuta Udsm kati ya 2007-10 na akasoma shahada ya uzamili Udom kati ya 2013-15 hadi mauti yanamfika alikuwa mhadhiri msaidizi.

“Alikuwa akifundisha wanachuo kati ya 3,000-5000 wanaochukua kozi hiyo ambayo wamepokea kifo hicho kwa mshituko mkubwa,” alisema.

Mdenye amefariki dunia na kuacha mtoto mmoja mdogo wa umri wa mwaka mmoja na nusu.

Mwili wa marehemu utaagwa leo na kusafirishwa kwenda wilayani Ludewa mkoani Njombe  kwa mazishi.


from MPEKUZI

Comments