Mahakama Kenya Yazuia Vifungu 26 Sheria ya Makosa ya Mtandaoni

Mahakama Kuu ya nchini Kenya imezuia matumizi ya vifungu kadhaa vya Sheria ya mtandao iliyopitishwa na kusainiwa na Rais Kenyatta wiki mbili zilizopita nchini humo.

Mahakama imevizuia vifungu 26 vya Sheria hiyo mpaka hapo shauri litakaposikilizwa, hatua hii inafikiwa baada vya chama cha Wanahabari na waendeshaji wa Blogu kufungua pingamizi.

Akitoa uamuzi huo Jaji wa Mahakama Kuu, Chacha Mwita amesema kuwa sheria hiyo ni kandamizi kwa haki za binadamu ikiwemo uhuru wa kujieleza.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 18 mwaka huu ambapo itasikilizwa tena.


from MPEKUZI

Comments