Zungu amtaka Mwakyembe kutaja sababu za kufungiwa wimbo wa ‘mwanaume mashine’

Mbunge wa jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemtaka Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe aje na majibu bungeni kumweleza sababu za wimbo wa 'Mwanaume mashine' kufungiwa.

Zungu amesema hayo leo April 27, 2018 wakati akihairisha kikao cha bungeni na kumtaka waziri jioni ya leo kuja na sababu za kufungiwa wimbo huo kwa kuwa yeye anaona ni wimbo ambao hauna mapungufu kwa sababu humo ndani ya wimbo wamezungumziwa wa kina Kichuya na kina Tabwe ambao ni wachezaji wa Simba na Yanga.

"Mhe. Waziri jioni kwenye majibu hebu nielimishe kidogo kuhusu huu wimbo 'Mwanaume mashine' umeufungia kisa nini, maana wimbo huu unamtaja Kichuya, Msuva na Jumapili tunataka tuisikie hebu tuambieni sababu ya kuifungia ni nini" alisisitiza Zungu


from MPEKUZI

Comments