Waziri Aipa Siku 30 TANESCO

Serikali ya awamu tano kupitia Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametoa mwezi mmoja kwa mameneja wote wa mikoa wa Shirika la Umeme nchini Tanesco kuwaunganishia umeme wananchi ambao tayari washalipia huduma hiyo na meneja atakayeshindwa kutekeleza agizo hilo ajiuzulu kazi mara moja.

Dkt. Kalemani ametoa agizo hilo wakati alipokuwa kwenye ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa umeme vijijini (REA), awamu ya tatu katika maeneo mbalimbali wilayani kyela na kusema wananchi wamekuwa wanaolipia huduma ya kuunganishiwa umeme wamekuwa wakipatia kero nyingi bila ya kupewa huduma hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Hunter Mwakifuna ameishukuru Wizara ya Nishati kuwa kuwaelekeza wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini kuwashirikisha viongozi wa maeneo husika, hatua ambayo imepunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.


from MPEKUZI

Comments