Ummy atoa onyo juu ya chanjo ya Saratani ya Mlango wa uzazi

Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, ametoa onyo kwa wataalamu wa Afya nchi nzima kutothubutu kutoa chanjo ya Saratani ya Mlango wa uzazi  kwa watoto wenye umri wa miaka 14 bila ridhaa za wa wazazi.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa chanjo ya Saratani ya mlango wa uzazi kwa watoto wenye umri wa miaka 14, akiwa mkoani Tanga ambapo pia ameshauri  wanawake kupima kama wana tatizo hilo.

"Naomba kutoa rai nikiwa hapa Tanga , mtoto achanjwe pale ambapo mzazi wake akiwa ameridhia. Msimchanje mtoto bila ridhaa. Hili ni agizo kwa nchi nzima," Ummy.

Pamoja na hayo Waziri Ummy amesema kwamba mpaka sasa wagonjwa wengi hufika hospitalini wakiwa na asilimia 80 za ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi.

Mbali na hayo Waziri huyo ameweka wazi kwamba vituo vyote vya afya vinavyomilikiwa na serikali vimejengewa uwezo na kupewa vifaa vya ajili ya matibabu ya saratani ili kupunguza tatizo la wagonjwa.


from MPEKUZI

Comments