Rais Magufuli: Hakuna Chakula cha Bure Kitakachogawiwa Mwaka Huu

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, amewapa ujumbe mzito watanzania kupitia wakazi wa kondoa mkoani Dodoma akiwataka wazitumie vizuri mvua zinazonyesha na kuhakikisha wanajihusisha na kilimo kisawa sawa ili kuepukana na njaa.

Magufuli aliwataka wananchi kuzitumia vizuri mvua zinazoendelea kunyesha badala ya kuziona kero kwao huku akisema,hakuna mtu yeyote atakayepewa msaada wa chakula msimu huu.

Alisema yapo baadhi ya maeneo wananchi hawalimi lakini baadaye wataanza kulia njaa na kuomba chakula.

“Hivi mvua inanyesha namna   hii baadaye uje useme una  njaa ,na hii nawaeleza watanzania wote kuanzia Kongwa mpaka Chato,hakuna atakayepewa msaada wa chakula.”alisema Magufuli.

Akieleza zaidi alisema,wananchi wanaoishi kando kando mwa barabara  wanapaswa kuitumiwa katika kukuza Uchumi ili wanufaike na kuwataka wananchi kulima kwa bidii huku akisema,bila kufanya hivyo barabara hiyo haitawasaidia

Amewasifia wanawake wanaoishi kandokando mwa barabara katika mikoa ambayo tayari wanaitumia nafasi hiyo kama fursa na kuwataka wote wanaojidekeza kusubiri serikali kuwahudumia hasa vipindi vya njaa kwamba hawatafanikiwa.


from MPEKUZI

Comments