Historia Imeandikwa......Rais Kim Jong-Un Avuka Mpaka na Kuingia Korea Kusini

Rais Kim Jong-Un wa Korea Kaskazini amekuwa kiongozi wa kwanza wa taifa hilo kuvuka mpaka wa kijeshi uliowekwa kuzitenganisha nchi hizo mbili baada ya vita ya mataifa hayo mawili mwaka 1953. Akiwa ni mwenye tabasamu rais Korea kusini Moon Jae-in amempokea mgeni wake katika eneo la mpakani.

Ni miaka 65 hadi sasa kwa kiongozi wa Korea Kaskazini kuwahi kuvuka mpaka wa kijeshi uliowekwa kuzitenganisha Korea Kaskazini na Korea Kusini tangu kumalizika kwa vita vya mataifa hayo mawili mwaka 1953.

Eneo la mpaka huo aliouvuka Kim Jong Un wakati akielekea Korea kusini ni lenye kilomita 250 na upana wa kilomita nne,ambapo mara baada ya kuuvuka tu watu walipiga makofi kwa kuandikwa kwa historia.

Mkutano huo wa tatu baada ya mkutano wa mwaka 2000 na 2007 ni matokeo ya jitihada zilizofanyika miezi kadhaa kuimarisha mahusiano kati ya Korea hizi mbili na kufungua milango ya mkutano kati ya Kim na Rais wa Marekani Donald Trump.

Kim alitangaza juma lililopita kuwa angesitisha zoezi la majaribio ya silaha za nuklia kwa sasa.Hatua hiyo ilikaribishwa na Marekani na Korea Kusini kama hatua nzuri,ingawa watafiti wa China wameonyesha kuwa eneo linakofanyika jaribio la nuklia la Korea Kaskazini huenda lisitumike tena baada ya mwamba kuporomoka baada ya jaribio la mwisho la mwezi Septemba.

Korea Kusini na Marekani zimesema zinasitisha mazoezi ya kijeshi kwa siku moja kupisha mkutano huo.

Kim ameongozana na maafisa tisa, akiwemo dada yake, Kim Yo-jong,aliyeongoza ujumbe wa Korea Kaskazini kwenye michuano ya Olimpiki nchini Korea Kusini mapema mwaka huu.Mkutano huu pia utawahusisha maafisa wa juu wa kijeshi na wanadiplomasia.


from MPEKUZI

Comments