Adhabu ukikamatwa umetupa uchafu Dodoma

kiwa ni siku kadhaa zimepita tangu Rais John Magufuli kutangaza kuipa hadhi Dodoma kuwa jiji, Mkurugenzi wa jiji hilo Godwin Kunambi ameanzisha mpango wa kuwapatia bima za afya bure wafagiaji wa maeneo yanayozunguka jiji hilo ili kuweza kuwasaidia .

Kunambi kwa kushirikiana na Mkuu wa mkoa huo Dr Bilinith Mahenge wametangaza adhabu kwa watu wote watakaokutwa wanatupa uchafu katika maeneo yanayozunguka jiji hilo.

”Mtu akitupa uchafu Dodoma anaandikiwa kulipa na anaandikwa kwenye mtandao jina lake linabaki humo, makosa yakifika matano hadi manne tunatoa majina yao kwenye magazeti”. Amesema Kunambi


from MPEKUZI

Comments