UPDTES: Lowassa Karudi Tena Mahakamani.....Watuhumiwa Hawajaletwa, Mahakama Kufanya Maamuzi Mchana Huu

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa amerejea tena mahakamani  mchana huu akiwa na Ndg. Mgeja.

Awali, Lowassa na Sumaye  waliondoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya muasisi wa Chadema, Victor Kimesera.

 Hadi mmchana huu watuhumiwa wote wakiongozwa na Mh. Freeman Mbowe ambao wapo gerezani Segerea waliokuwa waletwe Kisutu, hawajaletwa

 Baada ya sintofahamu ya kutofikishwa mahakamani kwa viongozi hao, mahakama ilisema itatoa uamuzi mchana huu.
 
Hatua hiyo imekuja baada ya mawakili wa pande zote mbili, kuingia kwa Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri anayesikiliza shauri hilo na kukubaliana nini cha kufanya.

Katika makubaliano yao mawakili hao na mahakama, walikubaliana kuwasiliana na Magereza ili wafanye kazi yao kama hao watuhumiwa  wanaletwa leo au hawaletwi, au mahakama iendeleea kusoma uamuzi wa dhamana hiyo.


from MPEKUZI

Comments