TANGA RAHA- Sehemu ya Arobaini na Nne ( 44 )

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

“Asante sana mke wangu”
Nilizungumza huku nikimvuta karibu Rahma, na akakilaza kifua kichwa chake juu ya kifua changu
“Ila mume wangu, ninasiri moja kubwa sana katika maisha yetu, ambayo inanisumbua sana kwenye kipindi chote cha maisha yangu”
“SIRI.....!!, Siri gani?”

ENDELEA
“Nitakuambia tu mume wangu, subiri kwanza watu waondoke”
“Hapana, naomba uniambie mke wangu”
“Nitakuambia tu mume wangu, nakuomba uwe mvumilivu.Ngoja kwanza nikazungumza na hao watu nje, alafu nitarudi kukuambia”
Nikamtazama Rahma kwa macho makali ya kumchunguza, akayakwepesha macho yake katika kunitazama usoni.Akanipiga busu la shavu na akatoka nje, nikajilaza kitandani huku amani ikiwa imenitoweka kwani sijui ni siri gani ambayo Rahma anataka kuniambia.Nikasikia kelele za watu wakishangilia kwa furaha, sikujua ni kitu gani ambacho Rahma alizungumza hadi kuwafanya watu kushangilia kwa furaha namna hii.Nikanyanyuka kitandani na kuanza kutembea tembea ndani ya nyumba kutazama ubora wa chumba chetu, kusema ukweli kimetengenezwa kwenye hathi ya halil ya juu, kila kitu kimewekwa kwenye mpangilio mzuri wa kuvutia kwenye macho ya kila ambaye ataingia ndani ya hiki chumba

Nikaingia bafuni,na kukuta bafu zima, kuta zake zimesilibwa na vioo vigumu sana, Nikajitazama sura yangu na kukuta kidogo ninamabadiliko, kwini hali ya ukijana imeanza kupotea kwa mbali
“Duuu, kweli nimekuwa sasa”
Nilizungumza huku nikijichunguza vizuri, sura yangu
“Ni wakati wa mimi kuwa baba, mwenye familia bora”
Nilizungumza huku nikitabasamu, nikavua shati langu, na kubaki kifua wazi.Hapa ndipo nikaona kovu lililopo nyuma ya mgongo wangu.Nikakumbuka mara ya mwisho nilitua kwenye kisiki cha mti wa mkoko kipindi ninapambana na Joka kubwa.Nikiwa ninaendelea kujitazama kwenye kioo, gafla nyuma yangu nikaiona sura ya Olvia Hitler ikicheka pasipo kuwa na mwili, nikageuka kwa haraka huku nikihema kwa wasiwasi, ila sikuona kitu cha aina yoyote.Nikataka kupiga hatua mbele nikastukia mlango ukifunguliwa, akaingia Rahma

“Baby kumbe upo huku?”
Rahma alizungumza huku akinitazama usoni kwa umakini
“Mbona upo hivyo Eddy, kuna tatizo lolote?”
“Haa, hapana”
“Mbona kama una wasiwasi?”
“Hakuna kitu mke wangu”
Rahma akanisogelea na kunikumbatia, huku akiniminya minya mgongo wangu kwa kutumia vidole vyake
“Haumii, nikikuminya hapa?”
“Kwa mbali ninahisi maumivu, ukiniminya kwa nguvu kwenye hilo kovu”
“Pole mume wangu”
“Asante”
“Watu wako, wamesha ondoka”
“Hawajakuletea tabu?”
“Hapana, ila nimewaambia waje kesho kutwa, nitaandaa kasherehe ka kukukaribisha nyumbani”
“Sawa, mke wangu”
“Pia, nimewaambia waandishi wa habari waje wazungumze na wewe”
“Sawa mke wangu”



from MPEKUZI

Comments