Breaking News:Mbowe na Viongozi wengine CHADEMA wamefikishwa Mahakamani

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na vigogo wengine wanne wa chama hicho wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo baada ya kuwekwa Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.

Viongozi wengine waliofikishwa mahakamani hapo ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji; manaibu katibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar) na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Esther Matiko.

Februari 20, 2018 Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa viongozi saba waandamizi wa Chadema, siku chache baada ya tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.

Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi Februari 16 akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo vya mawakala wao.


from MPEKUZI

Comments