AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 67 na 68 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA-
ILIPOISHIA  

Tukiwa katika hali ya kutambulishana, alama nyekundu kwenye hichi chumba iliyo kwenye ukuta ikaanza kupiga.
“Nini?”  
Nilimuuliza Mariam kwa wasiwasi, aliye anza kuchomoa bastola yake.
“Kuna meli ya maharamia wa Kisomali wanao teka meli za mizigo inatusogelea, sasa leo hawa wameingia choo cha kike”
Mariam alizungumza huku akitoka katika chumba hichi na kuniacha na hawa manahodha ambao nao pia kila mmoja akaanza kuchomoa bastola yake tayari kwa mashambulizi ambayo kwa haraka haraka yanaonekana ni mashambulizi makubwa, kwa maana kila mmoja yupo tayari kufa au kupona.

ENDELEA  
Sikuona haja ya mimi kuendelea kukaa katika eneo hili, nilicho kifanya na mimi ni kutoka katika chumba hichi cha manahodha na kuanza kumfwata Mariam kwa nyuma.
“Ni mpango gani unafanyika?”
Nilumuuliza Mariam kwa sauti ya juu kwa maana king’ora hichi kinatoa sauti kubwa sana, na tunapishana pishana na wafanyakazi wa hii meli wakikimbia huku na kule kujipanga na mashambulizi.
“Mipango gani Dany?”
“Juu ya hawa maharamia?”
“Mipango ni kuwazuia, tukishindwa wao ndio watatuua sisi, tutafute sehemu ambayo tunaweza kujibumashambulizi yao”
Marima alizungumza huku akitembea kwa mwendo wa haraka. Tukaingia kwneye moja ya chumba cha kuhifadhia silaha. Marima akachukua  bunduki zenye uwezo zaidi ya bastola yake, hata mimi nikachangamkia uchukuaji wa silaha.

“Dany kumbuka, hii ni mali ya baba yako na wote humu ndani watakufa kwa ajili ya mali ya baba yako. Pambana na ninatambua kwamba wewe ni mpambananaji”
Mariam alizungumza huku akinitazama usoni mwangu. Nikatabasamu kwa maana kitu  anacho kizungumza Mariam ninakielewa vizuri. Tukatoka katika chumba hichi na kupandisha juu  kabisa ya meli na kutafuta sehemu iliyo kaa vizuri na kujificha. Hatukukaa hata dakika mbili tukaona meli boti mbili za maharamia hawa wa Kisomali zikija kwa kasi katika eneo la meli yetu.

 Nikaishika vizuri bunduki yangu huku nikiwa ninatazama boti hizo jinsi zinavyo kuja. Mariam akaanza kushambulia boti hizo, jambo ambalo lilinifanya na mimi nianze kushambila boti hizi.
Hali ya sauti katika meli hii ikabadilika kabisi, haikuwa ya king’ora kinacho lia ila ni sauti ya milio ya bunduki hizi za kila aina. Maharamia nao wakajitahidi kujibu mashambulizi, ila hali ikawa mbaya kwao kwa maana watu zaidi ya mia moja wanawashambulia wao tu.
    Boti moja ya maharamia, ikalipuka hata kabla hawajafika kwenye meli yetu. Mashabulizi yakahamia kwenye boti hii ya pili ambayo baada ya kuona mashambulizi yamezidi  kuwa makali, wao wenyewe wakaamua kugeuza na kuandoka. Watu weoye kwenye meli wakashangilia kwa furaha kutokana na ushindi ambao tumeupata.



from MPEKUZI

Comments