Ya Sanchez Kuhamia Man U Na Uchawi.

NA. DOKTA  MUNGWA  KABILI.....0744  000  473.
Ni  rahisi  sana  kwa  shabiki  kindakindaki  wa  mpira  wa  miguu  kuwa  mchawi  katika  maisha  halisi  kuliko  shabiki  kindaki  ndaki  wa  muziki. 

Hii ni  kwa  sababu  shabiki  wa  timu  moja  ya  mpira  wa  miguu   hawezi  kuwa  shabiki  wa  timu  nyingine  ya  mpira  wa  miguu  ambayo inashiriki  katika  ligi  moja  na  timu  yake .

Kwa  mfano  Shabiki  wa  Yanga  hawezi  kuwa  shabiki  wa  Simba   wala  kufurahishwa  na  mafanikio  ya  Simba  kama  ambavyo  Shabiki  wa  Simba  hawezi  kuwa  shabiki  wa  Yanga  wala  kufurahishwa  na  mafanikio  ya  Yanga. 

Shabiki  wa  Real  Madrid  hawezi  kuwa  shabiki  wa  Barcelona  wala  kufurahishwa  na  mafanikio ya  Barcelona  na  kinyume  chake.

Ili  hali  katika  upenzi  wa  muziki  hali  ni  tofauti  sana. Shabiki  wa  Msondo  Ngoma  ana weza  kupendezwa na  nyimbo  za  wana  Sikinde  Ngoma  ya  Ukae  kama  ambavyo  shabiki  kindakindaki  wa  wana  Sikinginde   Ngoma  ya  Ukae  anavyo weza  kufurahishwa  na  nyimbo  za  Msondo  Ngoma. 

Shabiki kindaki  ndaki  wa  Diamond  Platnumz  anaweza  kuwa  mpenzi mkubwa  sana  wa  nyimbo  za  Ali  Kiba  kama  ambavyo  Shabiki  wa  damu  wa  Ali  Kiba  anavyo weza  kuwa  mpenzi  mkubwa  wa   nyimbo  za   Diamond  Platnumz. 

Shabiki  kindakindaki wa  Davido anaweza  kuwa  mpenzi  wa  kutupwa  wa  nyimbo  za  Wizkid  kama  ambavyo  shabiki   wa  kutupwa  wa  Wizkid  anavyo weza  kuwa  mpenzi  mkubwa  wa  nyimbo  za  Davido.

Shabiki  kindaki ndaki w a  AKA  anaweza  kuwa  mpenzi  wa  kutupa wa  nyimbo  za  Casper  Nyovest  kama  ambavyo  shabiki wa  damu  wa  Casper  Nyovest  anavyoweza  kuwa  mpenzi  mkubwa  wa  nyimbo  za  AKA.

Shabiki  kindakindaki  wa  Tupac  Shakur  anaweza  kuwa  mpenzi  wa  damu  wa  nyimbo  za  Notorious  BIG  kama ambavyo  shabiki  kindakindaki  wa  Notorious BIG  anavyo weza  kuwa  mpenzi  wa  damu w a  nyimbo  za  Tupac  Shakur.

Lakini  hali ni  tofauti  sana  kwa  mashabiki  wa  mpira  wa  miguu. Ushabiki  wa  mpira  wa  miguu unapo tamalaki  unaweza  kunmfanya  shabiki  husika  akawa  na  tabia  ama  hulka ambazo  hazina  tofauti  na  hulka  za  wachawi.

Kitendo  cha  shabiki  wa  timu  moja  kutofurahishwa  na  mafanikio  ya  timu  nyingine  ambayo  haya  iathiri  timu  yake   hakina  tofauti  yoyote na  mchawi  ama  mshirikina  ambae  anaumizwa  kwa  sababu  mtoto  wa  jirani yake  amefaulu  na  kuchaguliwa  kujiunga na  chuo  kikuu.

Mfano  mzuri  ninao kwa  shabiki  mmoja  wa  mpira  wa miguu   ambae  jina  na  mahali  anapotoka  nina  muhifadhi. 

Shabiki  huyu  alinipigia  simu  yangu  juzi  na  kunieleza  kwa  uchungu  mkubwa  sana  kuwa  yeye  ni  shabiki wa  kufa  wa  klabu ya  Arsenal  na  kwamba  ameumizwa  sana  na  kitendo  cha  mchezaji  Sanchez  kuuzwa  kwenda  Manchester    United. 

Shabiki  huyo  akaendelea  kunieleza  kama  ifuatavyo :

   "NATAKA UMFUNGE  SANCHEZ. FUNGA  MIGUU  YAKE, AKIENDA MAN U  ASIFUNGE   HATA  GOLI  MOJA.  FUNGA  AKILI  YAKE  AKIWA  UWANJANI  ASAHAU  KAMA  YUPO  UWANJANI . FUNGA  KUMBUKUMBU  ZAKE   AKIFIKA  GOLINI  ASAHAU  GOLI  LILIPO.   MTIE  MALIENGE  KWENYE  MACHO  YAKE  AKIWA  NA  MPIRA  AWE  ANAONA  GOLI  LIKO  PEMBENI  APIGE  PEMBENI  NA  KUKOSA  GOLI.  GOLI  PEKEE  AMBALO  ATATAKIWA  KUFUNGA  LIWE  GOLI  LA  KUJIFUNGA  MWENYEWE  NA  SI  VINGINEVYO.

MFARAKANISHE  NA  WACHEZAJI  WENZAKE,  KOCHA  WAKE  NA  MASHABIKI  WAKE.  NA  MWISHO  WA  SIKU  ATUPIWE  VIRAGO  NA  KUONDOKA  KWA  AIBU..  MFICHE   UWANJANI  ASIONEKANE  UWANJANI. AU   MTIE  MAJERUHI , AUMIE  KWENYE   MAZOEZI  KABLA  YA  KUANZA  KUITUMIKIA  KLABU  YAKE  AKAE  AKIWA  MAJERUHI  KWA  MSIMU  MZIMA  NA TIMU  YAKE  IMCHOKE  NA  KUMTUPIA  VIRAGO ..ASIONEKANE  UWANJANI  NA  KAMA  IKITOKEA  BAHATI  MBAYA  AMEONEKANA  UWANJANI  BASI  AONEKANE  AKIWA  AMEKAA  KWENYE   BENCHI NA IKITOKEA  AKICHEZA  MECHI  BASI  TIMU  YAKE  IFUNGWE  MAGOLI MENGI  NA  AWE  NI  MTU  WA  KUKOSA  MAGOLI  MARA  ZOTE… NIPO  TAYARI   KWA  LOLOTE  DOKTA . NINAKUOMBA  SANA  DOKTA  UNISAIDIE  KWA  HILO”

Shabiki  huyu  aliongea  mambo  mengi  sana   kwa  uchungu  mkubwa sana.

Maneno  ya  shabiki  huyu  wa  mpira  wa  miguu  yalinirudisha   miaka  sita  nyuma. Nikakumbuka  mwaka  2012   Robin Van Persie  alivyo  hamia  Man  U  kutoka  Arsenal, mashabiki  wengi  sana  wa  Arsenal  hawakufurahishwa  na mmoja  kati  ya  mashabiki  hao  alinitafuta  na  kuniambia  :

“    DOKTA. , MIMI  NI SHABIKI  MKUBWA  SANA  WA  ARSENAL. MIMI NI MFANYAKAZI,. OFISINI  KWETU  KUNA WAFANYAKAZI WENZETU  WAWILI  MASHABIKI  WA  MAN  U  AMBAO  WANA  DHARAU  SANA NA  MANENO  YA  KEJELI  SANA  HASA TIMU  YANGU  YA  ARSENAL  INAPOKUWA  IMEFUNGWA.  MIMI  NINAOMBA  UFANYE  DAWA  ZAKO  HAWA  JAMAA  WAFUKUZWE  KAZI   AU  WAHAMISHIWE  KWENYE  MIKOA  YA  MBALI  KABISA. ILI  NISIWAONE  WAKIWA  WANAFURAHIA  MAGOLI YANAYO  FUNGWA  NA  VAN PERSIE  AKIWA  AMEVAA  JEZI  YA  MAN  U.

NINAJUA  VAN PERSIE  NI MCHEZAJI  HATARI SANA  NA  SITAKUWA  TAYARI  HATA  KIDOGO KUWAONA  FULANI  NA  FULANI  ( ANATAJA  MAJINA  YAO  )  WAKIWA WANAFURAHIA  USHINDI W A  TIMU  YAO  KWA  MAGOLI  YALIYO FUNGWA  NA  VAN PERSIE. NITAUMIA  SANA  “

Kwa  Mifano  hiyo  miwili   unaweza  kuona   mahali  ambapo  ushabiki  wa  mpira  wa  miguu  una weza  kukufikisha.

Katika  ulimwengu  wa  michezo  ni jambo  la  kawaida  sana  kwa   shabiki  wa  timu  Fulani  kutofurahi  pindi  timu  yake  inapo fungwa  au  kupata  matokeo  mabaya . SIna  tatizo  katika  hili.

Ninacho kisema  hapa  ni  pale  wewe  shabiki  wa  mpira  wa  miguu unapofikia  hatua  ya  kuichukia   timu pinzani  kiasi  cha  kutofurahishwa  na  mafanikio  ya  timu  hiyo pinzani  hata  kama  haya  kuathiri  au kuiathiri  timu  yako  kwa  chochote. 

Hiyo  ndio tunayo  ita  roho  ya  kichawi na  uchawi.

Mfano  mzuri  ni  huu  hapa.  Wewe  ni  shabiki  wa  Arsenal, timu  yako  imefuzu  kuingia  NNe  bora na  umesha  maliza mechi  zako  zote.  Wapinzani  wako  Man  U  wamebakiza  mechi  moja  tu  na wanatakiwa  wapate  pointi  tatu  ili  nao  waweze  kufuzu  kuingia  nne  bora. Bahati  nzuri Man  U wanashinda  na  kuingia  nne  bora. Wewe  shabiki  wa Arsenal  unachukia na  kukasirika  kabisa   kwa  sababu  Man  U na  wao  wamefuzu  kuingia  nne bora.  Unapofikia  katika  hatua  hii  ndipo  unapokuwa  katika  levo  moja  na  wachawi  kwa  sababu  wachawi  pia  hawapendi  kuuona  mafanikio  ya watu wengine  hata  kama  hayawa  athiri kwa chochote..

Ukitafakari  suala  hili  kwa  jicho  la  tatu  utagundua  kuwa chuki  uliyo nayo  dhidi  ya  mafanikio ya  timu  pinzani  mara  nyingi  huwa ni chuki  dhidi  ndugu, jamaa, na  marafiki  zako.  Hii  ni  kwasababu  ifuatayo :

“  MARA  ZOTE  SHABIKI  WA  TIMU  FULANI  ANAPO  CHUKIZWA  NA  MAFANIKIO  YA  TIMU  PINZANI  HUWA  ANAKUWA   HACHUKIZWI  NA  MAFANIKIO  YA  WACHEZAJI  AU  TIMU  HIYO  PINZANI  BALI  HUWA  ANACHUKIA  KUONA  JIRANI, JAMAA, AU NDUGU  NA  MARAFIKI  ZAKE  AMBAO  NI  MASHABIKI  WA  TIMU  HIYO  PINZANI  WAKIWA  WANAFURAHIA  MAFANIKIO  YA  TIMU  HIYO  PINZANI  NA  SI  VINGINEVYO “

Kwa  hiyo  chuki  yako  wewe  sio chuki  dhidi  ya  timu  pinzani, ila ni  chuki dhidi ya jirani  yako unaeonana  nae  kila siku  ambae  ni  shabiki  wa  timu  pinzani. Hutaki kumuona  akiwa  anafurahia  na  unafurahia  kumuona  akiwa  anahuzunika  pindi  timu  yake  pinzani  inapo  pata  matokeo  mabaya.

Roho  au  hulka  hiyo  haina  tofauti  na  roho  ya  kichawi. Mfano, mwanzoni  mwa  miaka ya  tisini  kuna  kijana  mmoja  kutoka  mkoa  mmoja  wa  hapa  hapa  Tanzania, baada  ya  kuhitimu  masomo  yake, alipangiwa  kufanya  kazi  kwenye  tarafa  moja  iliyopo  katika  mkoa  mwingine  hapahapa  nchini.

Tarafa  hiyo  inasifika  kwa  kuwa  na  idadi  kubwa  ya  magwiji  wa  uchawi  na  ushirikina  na  ipo  tofauti  kabisa  na  kata  nyingine zote  zilizopo  katika  mji  huo  ambao  ni  miongoni  mwa  miji  yenye  maendeleo makubwa  hapa  nchini.

Wazazi  wa  kijana  huyo  walimuhasa  atakapo  fika  katika  tarafa  hiyo, awe  na  nidhamu  na  heshima  ya  hali  ya  juu  sana. Awaheshimu  watu  wote  bila  kujali  hali  zao  kimaisha  au  umri
wao  na kikubwa  zaidi, awaheshimu  sana  wazee.

Huyo  kijana  baada  ya  kupangiwa  kazi  kwenye  tarafa  hiyo, wazazi wake  walimuhasa  akifika  katika  tarafa  hiyo  awaheshimu  watu  wote, wakubwa  kwa  wadogo, asiwe  na  dharau  na  kikubwa  zaidi awe na  ukaribu  sana  na wazee.

Hao wazee  ndio watakuwa  baba  zake  ambao  watamlinda na kumuongoza  na   kumfanya  aishi  salama  katika  tarafa  hiyo. ( KATIKA  TARAFA  HIYO WAZEE  WANAHESHIMIKA  SANA  NA  HUWA  HAWAITWI “BABU”  BALI  BABA )

Kijana  alipofika  katika  tarafa  hiyo  akaanza  kufuata maelekezo aliyo  elekezwa  na wazazi. Alikuwa  na  heshima  ya  hali  ya  juu  sana.  Ndani  ya  muda  mfupi  tu  akawa  ameshajulikana  kwa  magwiji wa  tarafa  hiyo. Kijana  alikuwa  akipata  mshahara wake, atanunua  sukari, chumvi, mchele , sabuni  na  vitu  vingine na  kuwagawia   magwiji wa  tarafa hiyo. Nadhani alikuwa  muumini  wa  methali  isemayo  “  Mchawi  mpe  mwana  akulelee “, isipokuwa  tu  yeye  aliamua  kujikabidhi yeye  mwenyewe  wamlee.  “

  Kila  siku jioni  ilikuwa lazima  aende  kuripoti  kwa  wazee  hao kama  ishara  ya  kuonyesha  heshima, adabu na  utiifu  kwao. Siku ambayo hakuripoti  basi kulikuwa  na  sababu  isiyo weza  kuzuiliwa  na  binadamu na  akionana  nao  kesho  yake  lazima  awaombe  radhi.

Kijana  huyu  alikuwa mjasiriamali pia. Akiwa  katika  tarafa  hiyo  akagundua  fursa  kubwa  ya  biashara  ya  mbao  na  vifaa  vya  ujenzi  pamoja  na  udalali  wa  viwanja  na  mashamba kwa  sababu  mji  ulikuwa  unapanuka  na watu wengi  walikuwa  wana  jenga  kwa  kasi.

Jamaa  akaenda  kuchukua  mkopo benki na  kuingia  kwenye  biashara  ya  mbao  ambayo haikuchelewa  kuanza  kumlipa.

Kijana  akawa  anatengeneza  pesa  za  kutosha  na  hata  matunzo  kwa  wale  ‘magwiji’ yakaongezeka.

Baada  ya  kipindi  kichache  Yule  kijana  akaanza  kuwaambia  magwiji  hao  sentensi  ambazo  hawakuzipenda.

 Hawakupendezwa  na  sentesi  hizo  kwa  sababu  zilikuwa  na  maana  mbaya  sana  katika  tafsiri  ya  kamusi  ya  kichawi.

  Labda  tu  kwa  wasio  fahamu, wachawi  wana  kamusi  yao.  Moja  kati  ya  kazi  za  kamusi  ya  kichawi  ni  pamoja  na kutafsiri  maneno, ishara  na  vitendo  mbalimbali  vinavyo  fanywa  na  watu  mbalimbali.

 Nyuma  ya  kila  sentensi  unayo  izungumza, huwa  kuna  sentesi  nyingine  ya  kichawi.  Nyuma  ya  kila  kitendo  unacho  weza  kukifanya  huwa  sentensi  ya  kichawi.

Kwa  mfano :  “ A “ ni  Kijana  mwenye  umri  wa  miaka  25. Kijana  huyu  amezaliwa  na  kukulia  kwenye  kijiji   “ X “. Kijiji    hiki  ni  kijiji  ambacho  wakazi wake  wengi  ni  wachawi na  washirikina.

Ndani  ya  kijiji  hiki  hakuna  maendeleo. Watoto  wa  kike  na  kiume  kutoka katika  kijiji  hiki  wote  wameharibikiwa  na  hakuna  alietoka  katika  maisha  hata  mmoja. 

 Kwa  bahati  nzuri  au  mbaya  huyu  kijana “ A “ baba  ake  alikuwa  na  mwamko w a  elimu, akampeleka  “ A “ kwenye  shule  za  bweni  ambako  ameweza  kusoma  kuanzia  shule  ya  msingi  hadi  chuo  kikuu. Alikuwa  anarudi  kijijini  kimya  kimya  kusalimia  kisha  anarudi  mjini  kuendelea  na  masomo yake.

Baada  ya  kuhitimu  Chuo  Kikuu, siku  moja  “ A “ anaenda  kutembelea  kijijini  kwao. Na  kwa  bahati  mbaya  au nzuri  “  A “  anakutana  na  mzee  “ Y “. Huyu   ni mzee  ambae  anaheshimika  na  kuogopeka  sana  hapo  kijijini  kwa  sababu  "ugwiji " na  “ A “ anamfahamu  fika  mzee  huyu  tangu  akingali  mdogo.

Kwa  sababu  kijana  “  A “ amelelewa  katika mazingira  ya  heshima, anapokutana  na  mzee  “ Y “  kijana  huyu  anamsalimia  kwa  heshima  na  adabu  zote  na  kama  hiyo  haitoshi,  A  anamsaidia  mzee  “ Y “  kubeba   mzigo  wake  ,  hadi  nyumbani  kwa  mzee  “ Y “

Hapo  Kijana  “ A “ atafarijika  moyoni   kwamba  nimetengeneza  sifa  ya  kuwa  kijana   mzuri  kwa  adabu  na  heshima  niliyo  muonyesha  mzee  huyu.

"  A " anajiona  yupo salama  na  kwamba  ametengeneza  urafiki  na  mzee  " Y " .

Lakini  kwa  mzee  “ Y “ ambae  ni mchawi  na  mshirikina  yeye  atakitafisiri  kitendo  cha  kijana  “A “   kwa  namna  tofauti  sana. Akitafsiri  kwa  kutumia  kamusi ya  wachawi.

Atakitafsiri  kitendo  cha  kijana  “ A “  kama  ifuatavyo :

“  DUH! YANI  HUYU  KIJANA WA MZEE  “ X “ PAMOJA  NA  KUWA  NA  UMRI  WA  MIAKA  25  LAKINI  AMENIONYESHA  HESHIMA NA  ADABU  YA  HALI  YA  JUU  KIASI  HIKI? 

HAIWEZEKANI  HATA  KIDOGO. KIJANA  WA  MIAKA  25 ANANIONYESHA  HESHIMA  NA  ADABU  KUBWA  KIASI  HIKI.  INA  MAANA  BADO  TU  HAJAHARIBIKIWA?!!!  INA  MAANA  HAVUTI  BANG1!!!  SIO  MLEVI  WALA  HANA  MAKUNDI!!!  HAIWEZEKANI !!!  SIWEZI  KUKUBALI  UPUUZI  HUU  HATA  KIDOGO!!!

 MIMI   AMBAE  SIO  BABA  AKE  WALA  SINA  UNDUGU  NAE  AMENIONYESHA  ADABU  NA  HESHIMA  KUBWA  KIASI  HICHO, WAKATI  WATOTO WANGU   WA  KUZAA  MWENYEWE   WENYE  UMRI  SAWA  NA  WAKE, WAKIKUTANA  NA  MIMI  WANANIPIGA  VIKUMBO, KAMA  HIYO  HAITOSHI  HUWA  WANANITUKANA  HADI  TUSI  LA  MAMA  NA KIPIGO  JUU!!!.INA  MAANA  HUYU  KIJANA” A” BADO  HAJA  HARIBIKIWA ? KAMA  MIMI  TU  AMBAE  SIO  BABA AKE  AMENIONYESHA  HESHIMA  KUBWA  NAMNA  HII,  VIPI  KUHUSU  BABA  AKE? SI  ITAKUWA  MARADUFU!!! HAIWEZEKANI HUYU  MZEE “  X “ HAWEZI  KUFURAHIA  HESHIMA  YA  MTOTO  WAKE  WAKATI  MIMI  KILA  SIKU  NALIA  NA  UCHUNGU  KWA  USHENZI  NINAO  FANYIWA  NA WANGU   WA  KUWAZAA  MWENYEWE !!!  LAZIMA  NIMROGE  HUYU  KIJANA  NA  LAZIMA  NIMRIPOTI  KWENYE  KIKAO!!!!

Baada  ya  hapo  Mzee  “  Y"atakacho  kifanya  ni  kwenda  kumripoti  kijana “ A “ kwa  mkuu  wa  kilinge.( , VILINGE   VYA  WACHAWI  HUWA  VIPO KARIBU  KATIKA  KILA  SEHEMU  NA    MARA  NYINGI  HUWA  VINAKUWA  KWENYE  MITI  MIKUBWA NA  HUWA  VINAKUWA  MAJINAAMBAYO  MARA  NYINGI  HUBEBA  MAJINA  YA  MAENEO. MFANO “ Mbuyuni”, “Mwembeni” “Mkuyuni”” Mwembe ….” Nakadhalika.

Kitakacho  tokea  baada  ya wiki  au  miezi   kadhaa  wazazi wa  kijana  “ A “  wataanza  kumuona  kijana  wao  amebadilika  kitabia  katika  namna  ambayo  hawakuitegemea  wala  kuitarajia.

 Kijana  msomi  wa  chuo  kikuu utamsikia  anazungumza  maneno  ya  ovyo    kama   vile “  Oyaa  Bi. Mkubwaa“,  au “ Mshua unazingua !!“ na  maneno  mengine  kama  hayo pamoja  na  kufanya  vitendo  vya  kilofa  kama kuvalia  suruali  chini  ya  makalio, kunyoa  viduku, kunywa  viroba,kushinda   bar  anapiga  story  na wahuni  na  mwisho  wa  siku  hayo  ndio  yanakuwa  maisha  yake .

Washirikina na wachawi huwa wanaishi maisha ya hovyo sana sema tu huwa wanajikaza mambo yao yasijulikane. Ubaya wanao wafanyia watu wengine huwa unawarudiaga wao wenyewe saba mara sabini hata baada ya miaka mingi.

 Mchawi anapokufanyia ubaya huwa ni kama anajiwekea mwenyewe akiba ya ubaya ambao utakuja kumtokea baadae kabla ya muda wake wa kuishi haujamalizika hapa duniani. Kwa hiyo usishangae mzee Y anapo kasirika kusalimiwa kwa heshima na adabu na kijana A .

Katika uhalisia hayo ndio maisha ya wachawi katika levo ya familia. Kuna kisa kimoja kilitokea mwishoni mwa miaka ya themanini katika tarafa hiyo hiyo niliyo itaja hapo juu. Alihamia mtendaji mpya wa mtaa kutoka mkoa mwingine, baada ya kama wiki mbili hivi ikaletwa kesi ofisini kwake,. Kuna mzee mmoja gwiji amepigwa kwa mabapa ya mapanga na mtoto wake wa kumzaa mwenyewe alieitwa Kulwa . Mzee alishachukua PF3 tayari na kwenda kutibiwa polisi, jalada lilishafunguliwa kituoni na huyo Kulwa yupo ndani . Sasa mzee gwiji ameingiwa na huruma ya uzazi anataka kwenda kumdhamini mahakamani mtoto wake japo yeye ndio muhanga wa tukio la uhalifu lililo fanywa na mwanae. Kwa kuwa mzee alikuwa anajisikia vibaya hawezi kwenda ofisini kwa mtendaji kuchukua karatasi ya dhamana, akamtuma shemeji yake, yaani mdogo wa kiume wa mke wake.

Shemeji mtu alipofika kwa mtendaji na kumsimulia kilicho tokea, mtendaji alisikitishwa sana.. “ Alihoji inakuwaje mtoto unampiga kwa mapanga baba ako mzazi! Dunia imekwisha “ . Wakati mtendaji ana saini karatasi za dhamana, akawa ana mdadisi yule shemeji mtu “ Imekuwaje kuwaje mpaka huyo kijana akampiga mapanga baba ake mzazi ?”.. Shemeji mtu akajibu “ Bwana we mambo ya kifamilia ndugu yangu !|. Mtendaji akasema “ Mambo ya kifamilia?!! Yani mambo ya kifamilia ndio mtu ampige mapanga baba ake mzazi ?!! DU sijawahi kusikia hiyo ndio naisikia mara ya kwanza”. “ Ila vyovyote vile, tuchukulie kwamba kweli huyo kijana aliudhiwa na baba ake kiasi cha kuamua kumshambulia kama njia ya kumaliza hasira zake. Kwanini basi asinge mpiga u hata ngumi, kwa sababu hayo mapanga si angeweza kumuua kabisa!! Na angemuua tungekuwa tunaongea habari nyingine tena “

Shemeji mtu akajibu “ Kulwa ampige ngumi baba ake ? Kulwa hanaga muda wa kurusha ngumi kumpiga baba ake. Kulwa yeye huwa anampigaga na mapanga tu au silaha yoyote ile itakayo kuwa karibu nae. Mwenye muda wa kurusha ngumi ni dotto. Dotto ndio huwa anampigaga ngumi baba ake. Aaaaaah huwa anampiga sana tena sana. Na kizuri baba mtu mwenyewe analitambua hilo. “ Shemeji mtu akaendelea kusema “ Lakini hata hivyo pamoja na kwamba Dotto huwa anampiga baba ngumi baba ake mzazi lakini huwa zinakuwa ngumi kali kweli kweli, unajua Dotto ni mtu wa mazoezi sana na ana maguvu sana. Mtoto kidogo mwenye afadhali ni kaka yao mkubwa na kina Dotto yeye huwa anamtia bakora tu baba yao. Yeye hanaga muda wa kushika silaha wala kumpiga ngumi, yeye huwa ni bakora tu. Na baba mtu anajua, kaka yao mkubwa akiwepo kama kuna sehemu ya kuchuma fimbo karibu , huwa hafanyi kabisa ujinga ujinga, kwa sababu anajua kijana wake atamtandika na bakora “

Mtendaji  akataka  kujua  sababu  inayo  wafanya  vijana  hao  wawe  wanamkosea  baba  yao  mzazi  kwa  kumpiga. Shemeji  mtu  akajibu, huyu mzee  huwa  anampigaga  sana  mama  yao  akitoka  kwenye  ulevi  halafu  akiwaga  na  hela  huwa  anaenda  kuzimalizia  kwa  michepuko  huko. Sasa  vijana  huwa  wakisikia  mama  yao  kapigwa  au  katukanwa, na  wao  huwa  wanampiga  baba  yao. Wakimkuta  na  mchepuko  pia  huwa  wanampa  kisago  baba  yao.

Yule mtendaji alilewa na kubaki kusema “ Du ! Yani huyu mzee watoto wake wote huwa wanampiga . Dunia imekwisha “
Hao Kulwa na Dotto wakati wanafanya ujinga huo wa kumpiga baba yao walikuwa na miaka 37 na kaka yao alikuwa na miaka 40.

Katika mzingira kama hayo mzee kama huyu ambae watoto wake wa kuzaa mwenyewe wanampiga ngumi, mapanga na fimbo, hawezi kufurahishwa na heshima au adabau kutoka kwa kijana mtoto wa jirani yake . Huwa wanaumia sana.

Ndio maana miaka ya nyuma, vijana walishauriwa na kuambiwa kama hawana kinga ya wachawi wasi jipendekeze kabisa kwa wachawi kama alivyo fanya kijana A. Kuliko kujipendekeza ni bora wakae nao mbali kabisa. Kuliko kuonyesha wao ni vijana wenye adabu, bora wajifanye kujitoa akili pindi wanapo kutana na wazee wa aina hii hususani katika maeneo kama vile misibani nakadhalika. Huambiwi uwatukane, hapana, wewe kaa kimya na kama utalazimika kuzungumza basi zungumza mambo yanayo onyesha una maisha magumu, huna matumaini na umeharibikiwa kimaisha. Unatumia hiyo kama njia ya kuwapumbaza watu wabaya.

Jambo  lingine  ambalo  ni  la  kawaida  sana  katika  ulimwengu  wa  nyama  lakini  lina  maana  mbaya  sana  kwenye  kamusi  ya  wachawi  ni   “ Sauti ya  mtoto  mchanga  akilia “. Hakuna  jambo  lenye   maana  mbaya  katika  ulimwengu  wa  wachawi  kama  kusikika  sauti  ya  mtoto  mchanga  akilia,na mbaya  zaidi  sauti  hiyo  itokekwenye  nyumba  ya eidha  watu  wa  swala  au  ibada  au  ambao  wamefunga  ndoa  halali.

Hakuna  jambo  linalo  wakera  kama  kusikia  sauti  ya  mtoto  mchanga  akilia kutoka  katika  familia  ambayo  mke  na  mume  wameoana  kwa  ndoa  rasmi.

Nirudi  tena  kwa  kijana  wetu.
Kijana  huyu  alianza  kuwapigia  wazee  hao  stori  kama  vile  “  Nimepata  kiwanja  sehemu  Fulani “.  “ Nimeanza  kufyatua  matofali   “  mara  aanze kuwaambia  “    Nimetoka  kumpeleka  fundi  saiti   kwangu “  au  “ kesho  nitaenda  mjini  kuchukua  mabati, mbao “ na  hadithi  zinazo  fanana  na  hizo.

Kijana  huyu  alikuwa  anawaeleza  wazee  hao  mipango  yake  kwa  nia  njema  kabisa.

Aliwachukulia  kama  wazazi  wake  na  alikuwa  akiwaambia hivyo  ili   labda  wampe  ushauri  wa  kufuata  hususani  katika  suala  zima  la  “ ulinzi  wa  kiroho “

Ambacho  hakukijua  kijana  huyo  ni  kwamba, sentensi  alizo  kuwa  anazitamka kwa  wazee  hao, zilikuwa  na  maana  mbaya  sana  katika  kamusi  ya uchawi.

“ Sisi  tunaishi  kwenye  nyumba  za udongo. Si  watoto  wetu  wala  wajukuu  zetu  ambao  wamewahi  kuwa  na  nyumba  zao  wenyewe  achilia  mbali nyumba  ya  kisasa  kama  anayo  taka  kuijenga  kijana  huyu..  Haya  ni  matusi  makubwa  sana  kwetu.Hatuwezi  kukubaliana  na  upumbavu  kama  huu!!! “

Wazee  walicho  kifanya  wakaamua  kumtia  nuksi  kijana  huyo. Kwanza  akafukuzwa kazi. Akashindwa    kulipa  mkopo benki, nyumba  yake  aliyokuwa anaijenga  ambayo  ndio  kwanza  ilikuwa  imefikia  kwenye  lenta,ikapigwa  mnada  (  NYUMBA  NYINGI  KATIKA  TARAFA  HIYO  HUWA  ZINAISHIA KWENYE  LENTA  HUKU  WAMILIKI  WAKISALIA  KUWA  WALEVI  WAKUPINDUKIA  ).

Biashara  yake  ikafa.  Akaingia  kwenye  ulevi  wa  pombe  ulio   pindukia.

Hapa  kwenye  ulevi  wa  pombe  walimuacha  kwa  sababu  alikuwa  bado ana  vihela  hela, hivyo  walimuacha  ili  hela  alizo  kuwa  amebaki  nazo  azimalizie  kwenye  ulevi abaki  hana  kitu  kabisa.  Na  kweli  baada  ya  muda mfupi  akawa  ameishiwa  hela. Kichwani  mawazo, kazi  hakuna, biashara  imekufa, aibu  mtaani, maneno  yameanza  kuzungumzwa.

Jamaa  akaamua  kuingia  kwenye  ulevi  wa  gongo  ili aweze  kusahau  matatizo  yake. Baada  ya  kama mwezi  mmoja  hivi  jamaa  akawa   mlevi  wa kupindukia  anashinda  kwenye  vilabu  vya  gongo. Akawa  anaonekana  hajali  tena  kama aliwahi  kuwa  na  kazi, biashara  na  maisha  mazuri.

Wale  magwiji  hawakupendezwa  na  hali  hii,kwa  sababu  wao  walitaka  kijana  huyo  baada  ya  kutiwa  nuksi  hiyo  auone  uchungu  wa  kuishimaisha  ya  kilofa  na  umasikini  ulio  tukuka  na  kibaya  zaidi  wakamfunga   asiondoke  kijijini  hapo  ili  wawe  wanamuona  anavyo adhirika.

Taarifa  za  ulevi  wa  gongo  wa  kijana  huyo  hazikuwafurahisha  hata  kidogo,.Kwa  sababu  zilikuwa  na  maana  mbaya  sana  katika  kamusi  yao.

Walicho  kifanya  wazee  hao  wakamtafuta  kijana  huyo  na  kumpa 

dawa  ya  kuacha  pombe..

Dawa  hii  ni  tofauti  na  ile  inayo  changanywa  na mayai  ya  ndege  mmoja  mweusi  anaepaa  au  ile  inayo  changanywa  na  mavi  ya  ndege  mmoja  mweupe  afugwae.

 Hiidawa  inatokana  na  mizizi ya  mti  mmoja  wa  porini  wenye  jina

 linalo  fanana  na  jina   la  wilaya  moja iliyopo  kusini  mwa  Tanzania.  Huwa  ni  mwiko  kwa  mwanamke  mjamzito  kuuruka  mzizi  wa  mti  huu  kwa  sababu  akifanya  hivyo, mimba  itaharibika.

Katika  baadhi  ya  jamii za  kiafrika, mtu anapokufa  kwa  kujiua  mwenyewe,maiti  yake  huwa  haingii  ndani  na  kipande  cha  mzizi  wa  mti  huu huwa  kinachomekwa  kwenye  makalio  ya  mwili  huo ili kuvunja  roho  ya  kujiua  katika m familia na ukoo huo.

Huwa  unachukuliwa  mzizi  wa  mti  huo  ambao  umekufa  wenyewe, kisha  unasagwa  halafu  anapewa  mlevi.

Kijana  huyo  alipopewa  dawa  hiyo  alitapika  sumu  zote  na  toka 

siku  hiyo  alichukia  kabisa  pombe na  ulevi  wa  aina  yoyote  ile.

Kilicho  fuatia  baada  ya  hapo,  kijana  huyo  akawa  anafanya  kazi 

ambazo  haziendani  na  elimu  yake.

Kwanza  akawa  anabeba  mizega  ya  maji, mara  anazibua  vyoo, mara  anauzakaranga  ilimradi   watu  wamuone  anavyo  adhirika.   Wao  hwafaidiki  na  chochote  lakini  wanafurahia kumuona  kijana   huyo  akiwa  anateseka  na  kudhalilika.

Kuhusu matumizi  ya  uchawi na  ushirikina  katika  mchezo  wa  mpira  wa  miguu, Dokta  Mungwa  anasema,mambo  hayo  siku  hizi  hayafanyiki kama  ilivyo  kuwa  inafanyika  zamani.  Siku  hizi  mambo  yamebadilika  tofauti  na  ilivyo  kuwa  zamani.    Mambo  yamebadilika  sana  siku  hizi. Kwanza  siku  hizi  vijana  wanacheza  mpira  wa  kulipwa  tofauti  na  ilivyo  kuwa  zamani  ambapo  watu  walikuwa  wanacheza  mpira  wa  ridhaa  na kwa  mapenzi  ya  timu  husika.

Zama  hizo  watu  walikuwa  wanatumia  sana  uchawi  katika  mpira. Kila  namba  ilikuwa  na  uchawi  wake  na  uchawi  ulitofautiana  kutoka  timu moja  na  nyingine.

Kwa  mfano, kwenye  nafasi  ya  kipa

kipa  ilikuwa  kilikuwa  kinachukuliwa  kipande  cha sanda iliyo  tumika  kumvesha  maiti, kisha linachukuliwa karatasi  jeupe  ambalo  yanaandikwa  majina  ya  wachezaji  wote  wa  timu  pinzani  kisha  unawekwa  unga  wa kisiki  ambacho  watu  wakipita  njiani wanajikwaa  kwaa  na  vitu  vingine  viwili  ambavyo  sita  vitaja  hapa.  Baada  ya  hapo  ilishonwa  azima  ambayo  alipewa  kipa  na  kutakiwa  kuvaa kwenye  mguu  au  mkono  wowote.

 Ndumba  hii  iliaminika  kumsaidia  kipa  kuwa  na  uwezo  mkubwa  wa  kudaka  mipira  awapo  golini  na  pia kuwafanya  wachezaji  wa  timu  pinzani  kuwa  wanajikwaa  kwaa  na  kuanguka  wenyewe  kila  wanapo  karibia  lango.

Kwa  wachezaji  wanao cheza  namba  2,3,4  na 5  ilichukuliwa  mizizi  ya  nturantura  kisha  zinachongwa  mpigi  4  ambazo  kila  moja itafungwa  au kushonwa  na nyuzi nyeusi  kisha  wanapewa  wachezaji  wa  namba  hizo  na  kuzivaa, baada  ya  kuzikaanga  zote na  majina  ya  wapinzani kwenye mafuta  maalumu  pamoja  na  dawa  inaitwa  Tunda  la  Jini  au  Tufahal Jinni. Dawa  hizo  zilimwagiwa  kwenye  kigae  cha  chungu  kilicho  vunjika wakati  kikiwa  kimebeba  maji  yaliyo  chotwa  kisimani. Baada  ya  hapo  yaliandikwa  majina  ya  wapinzani  wote  kwenye  sahani  maalumu  nyeupe kwa  kutumia  zaafarani  nyekundu  na  baadae  kufutwa  kwa  kutumia  vidole.  Kila  mchezaji  alipewa  mpigi 4  ambazo  zilifungwa  kwenye  azima  na kuzivaa.

Ama  kwa  upande  wa viungo  na  washambuliaji, wao  ilichukuliwa  mizizi  ya  miti mitatu mkuyu, Mzungupori  na Mtundaugoro,ambayo  ilisagwa  na kuchomwa  pamoja  hadi  kuwa  unga  au  majivu  laini  sana.  Baada  ya  hapo  ulichukuliwa  upinde  ambao  ulitumika  kuua  nguruwe  pori,upinde huo  ulisagwa  pia  na  kuchomwa  hadi  kuwa  majivu,vyote  hivi  vilichanganywa  na  mafuta  maalumu  na  kisha  wachezaji  hao  walipakwa  au kuchanjiwa.

Wakati  mwingine  ulitumika  uchawi  wa  kuroga  timu  pinzani, kufanya  wachezaji  wote  wa  timu  pinzani  wakose  pumzi  wakiwa  uwanjani, ambapo  alikuwa  anatumika  mnyama mmoja  na kamba  maalumu.

Wakati  mwingine  mchezaji  wa  timu  moja  angeweza  kufanya  uchawi  wakuwaroga  wachezaji  wenzake  wanao  gombania  namba  na  kumfanya aonekane  yeye  ndio  zaidi  ya  wenzake. Mfano  mshambuliaji  aliweza  kufanyiwa uchawi, magoli  yote  afunge  yeye  mwenyewe  au  mafowadi wenzake  wafunge  kwa  kupitia  miguu  yake.  Fowadi huyu  alinuiziwa  kuwa  goli  lolote  kutoka  kwenye  timu  yake  lisifungwe  hadi  lipitie  kwanza kwenye  mguu wake  au  kichwa  chake.

Miaka hiyo ya zamani, uchawi na ushirikina kwenye mpira ulifanyika kama sehemu ya burudani ya mpira. Waganga walitumia michezo ya mpira wa miguu kushindanisha nguvu zao.

Wachezaji wali waogopa zaidi wachawi kutoka nje ya uwanja kuliko wachawi wa ndani ya uwanja.

Mchezaji wa mchangani alikuwa akipata nafasi ya kwenda kucheza kwenye timu kubwa basi ilifanywa siri hadi atakapo anza kuichezea rasmi timu hiyo kubwa.

Mwishoni mwa miaka ya themanini, kuna kijana mmoja katika kitongoji kimoja cha kwenye mkoa mmoja unaopatikana mashariki wa Tanzania alikuwa kiungo mshambuliaji hatari sana. Alikuwa anachezea timu mmoja iliyo kuwa inashiriki ligi daraja la tatu kipindi hicho. Basi mabosi wa timu moja kubwa wakamuona, wakawa wamemkubali sana, wakamfuata kuzungumza nae ili akasajiliwe kwenye timu hiyo kubwa, bila kuchelewa kijana akakubali na mipango ya kumchukua ikaanza kufanyika.

Alikuwa anatakiwa akaripoti klabuni siku ya Jumatatu kwa ajili ya kwenda kusaini mkataba mnono pamoja na kujiunga na wenzake kambini. Baba wa kijana huyo kwa furaha ya mtoto wake kusajiliwa kwenye timu kubwa akaanza kuwaambia, ndugiu, jamaa, majirani na marafiki. Habari zikawafikia magwiji na kama ilivyo tazamiwa,. Hazikuwapendeza. Magwiji wakaunda kamati ya kumuwekea zuio kijana huyo asiweze kwenda katika timu hiyo kubwa.

Ilikuwa siku ya Ijumaa, wazee wa mtaa wakamwambia baba wa kijana kuwa wameandaa sherehe maalumu ya kumuaga na kumpongeza kijana wao kwa sababu ameleta heshima kubwa sana kwenye mtaa wao. Kijana akatakiwa na yeye kuhudhuria. Baba mtu akakubali kwenda ili isionekane amekataa kwa sababu anaringa mtoto wake amesajiliwa kwenye timu kubwa. Kaka wa baba mtu ( Yani baba mkubwa wa kijana yule mchezaji ) nenda kwenye sherehe ila kijana asiende kwa sababu wanaweza kumlisha uchawi kwenye chakula atakacho kula. Baba mtu akasema “ Nisipoenda na huyu kijana itaonekana kijana amedharau wito wa wazee, ngoja niende nae tu, cha msingi sitaruhusu ale chakula kwenye sahani yake mwenyewe. Nitahakikisha chakula kinaletwa kwenye sahani ya kula watu wote kwa pamoja na ikiwezekana tule pamoja na wazee walio tualika “. Kaka mtu akamwambia “ WACHA UPUMBAVU BWANA MDOGO.. DAWA HUWA ZINANUIZIWA. MNAWEZA KULA WOTE CHAKULA KWENYE SAHANI MOJA LAKINI AKADHURIKA MTU MMOJA KWA SABABU ANAKUWA AMENUIZIWA MTU HUYO HUYO MMOJA, KWA HIYO CHA MSINGI HAPA .. KIJANA ASIENDE KABISA. WAAMBIE ANAUMWA NA KICHWA “

Baba wa kijana hakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na ushauri wa kaka ake. Kijana kweli hakwenda kwenye hiyo sherehe kwa madai kwamba anajisikia kichwa kinamuuma. Mchana wa siku iliyo fuata sasa yani Jumamosi , kijana akaanza kulalamika kichwa kinamuuma, kichwa kinamchemka.

“ Baba kichwa kinauma, baba kichwa kinachemka !”. Inaelezwa kuwa joto la kijana huyo lilipanda kwa kasi ya ajabu katika namna ya kutatanisha. Inaelezwa zaidi kuwa kichwa cha kijana kilichemka kiasi kwamba ungeweza kuweka mtungi au sufuria la maji kichwani kichwani kwa kijana huyo yakachemka ndani ya muda mfupi kwa kiasi ambacho ungeweza kunyonyolea kuku !

Baba wa kijana hakuwa na jinsi zaidi kuwahisha kijana wake hospitali. Kufika hospitali madaktari kumpima wakakuta mtu alisha ondoka duniani toka enzi za Pontyo wa Pilato.

Nirudi kwa jamaa anaetaka Sanchez atupiwe uchawi wa kumfanya ashindwe kun'gaa kwenye timu yake mpya. Mawazo kama hayo yanaweza kukaa na kuishi ndani ya akili za wachawi tu. Hutakiwi kabisa kuwa na mawazo kama hayo.

Unamchukia mtu ambae hakujui wala hajui kama unamchukia na aathiriwi na chochote kuhusu chuki yako. Unadhani nani anae umia hapo kati yako wewe na Sanchez ?

Kumchukia mtu ambae hakujui wala hajui kama unamchukia, ni sawa na kuwapangisha kwenye nyumba yako, wapangaji ambao hawakujui na hawajui kama umewapangisha halafu wewe ndio unawalipa wao kodi. NI uwendawazimu.

Nafsi yako ni nyumba yako uliyo pewa na Mungu. Ndani ya nafsi yako unatakiwa uwapangishe wapangaji watakao kulipa kodi nzuri. Pangisha, furaha, amani, upendo, matumaini, imani nakadhalika. Ukipangisha chuki , husda na choyo, wewe ndio utakae umia. Utaishia kuvuna magonjwa kama presha, shinikizo la damu au kiharusi na kuvuta mapepo yatakayo endelea kukuletea nuksi kwenye maisha yako.

Kingine, unatakiwa kujua kuwa uchawi au uganga ni tofauti na mazingaombwe. Lazima uwe na sababu ya msingi na yenye akili. Hii ni kwa sababu uchawi ni gharama sana. Unahitaji vitu vingi ili jambo lililo kusudiwa liweze kutokea.

Ndio maana basi hata wachawi wenyewe wanapo taka kumroga mtu huwa wanaanza na njia za kawaida kwanza ambazo hazihusishi uchawi zikishindwa ndio wanaingia vitani rasmi kwa kuhusisha uchawi.

Kwa mfano wachawi wanataka kuwatenganisha mke na mume au mtu na mchumba wake. Kwa kuanza wataanza na umbea kwanza. Wanachukua maneno kwa mwanamke wanapeleka kwa mwanaume, wanachukua maneno kwa mwanaume wanapeleka kwa mwanamke. Wakiona mpango wao umeshindikana, hapo ndio wanatumia uchawi.

Ndio maana miaka ya nyuma watu walio kuwa wanaenda kwa waganga kutafuta suluhisho kwa mambo ya kipuuzi walikuwa wanaishia “kulaaniwa wao wenyewe “ na waganga hao.

Kwa mfano kulikuwa na baadhi ya wanaume, anaenda kwa mganga na kusema “ MGANGA NAOMBA UNIFANYIE DAWA ILI MKE WANGU ASIWE ANANIOMBA HELA YA MATUMIZI. ASAHAU KABISA KUHUSU KUNIOMBA HELA YA MATUMIZI HADI SIKU ANAINGIA KABURINI “

Mwanaume kama huyu ni mwanaume asie faa, kwa lugha nyingine anaweza kuitwa “ Khanithi “ . Mwanume wa hivi, kwanza alikuwa analazwa dhakari yake kwa kutumia akili yake ambayo imelala, halafu anafungwa kuzaa kabisa ili asirithishe upumbavu wake kwa watoto atakao wazaa... Na mwisho wa siku alitupiwa uchawi unaitwa “ SUNKHWA “ ama “ FUKUZA “ ambao ungemfanya aondoke kabisa kijijini hapo na kwenda kulowea kusiko julikana. Baadae lingefanyika tambiko maalumu la kutakasa kijiji hicho dhidi ya najisi ya mwanaume huyo.

Nimetoa maelezo haya ili kuwasaidia pia baadhi ya mashabiki wa Arsenal ambao wanaweza kuwa wameumizwa na kuondoka kwa Sanchez na ambao pia wanaweza kuwa na mawazo kama ya jamaa aliye taka nimroge Sanchez ili asipate mafanikio kwenye timu yake mpya.

Kama upo kwenye kundi hilo, huu ni ushauri wangu kwako :

1. JIPE MUDA UTASAHAU : Hakuna dawa nzuri ya kusahahu kitu au jambo unalo lipenda kama MUDA. Mwanzoni unaweza kuumia kumuona Sanchez akishangilia baada ya kuifungia timu yake mpya magoli kwenye mechi mbalimbali. Baada ya muda utazoea na utaona kawaida kabisa.

2. USIANGALIE MECHI ZA MAN U : Usiangalie mechi za Man U. Wewe subiri tu kuambiwa matokeo.

3. JITENGE : Siku ambayo Arsenal watacheza na Man U usitazame mpira pamoja na jamaa zako ambao ni mashabiki wa Man U. Nenda kaangalie mpira sehemu ambayo haujulikani.

4. HAMA MTAA UNAOISHI : Kama unadhani hauwezi kuwakwepa jamaa zako mashabiki wa Man U ambao watakua wanakuja kukukera wakishangilia namna Sanchez anavyo funga magoli, hama kabisa mtaa unaoishi/

5. BADILISHA NAMBA ZAKO ZA SIMU : Kwa sababu jamaa zako watakuwa wanakukera kukupigia simu kukwaambia kuhusu namna Sanhez anavyo fanya vitu vyake. Badilisha namba zako za simu ili wasikutafute kabisa.

6. BADILISHA OFISI AU ACHA KAZI KABISA : Kwa sababu si unasema wafanyakazi wenzako ofisini watakuwa wanakukera na habari za Sanchez. Basi kama ni mfanyabiashara, tafuta eneo jipya la biashara, au kama una ofisi yako, tafuta ofisi mpya au kama umeajiriwa, basi kazi kabisa ili uwe mbali nao.
7. HAMIA MAN U : Kwa sababu unampenda na unamkubali sana Sanchez na Sanchez ndo hivyo tena amehamia Man U. Kitu cha kufanya hapo wewe hamia Man U ili ukaendelee kuburudishwa na uchezaji wake.

8. JIFANYE HUJUI KAMA SANCHEZ ALIWAHI KUCHEZEA MAN U

9. FANYIWA TAMBIKO MAALUMU LA KUSAHAU KUHUSU SANCHEZ : Badala ya kuomba Sanchez asahau magoli, wewe ndio ufanyiwe tambiko maalumu la kusahau kuhusu Sanchez. Ukimuona Sanchez umuone kama takataka vile. Usikumbuke kama aliwahi kuchezea Arsenal.

10. 8. Kama unaona ushauri huo hapo juu ni UPUMBAVU basi kumchukia Sanchez kwa sababu kahamia MAN U pia ni UPUMBAVU ZAIDI.
 
Kitu  kingine  unacho  takiwa  kufahamu  ni  kwamba, Sanchez  anatafuta  maisha  yake. Man  U  wamempa  ofa  ya kumlipa Pauni  500,000/=  kwa  wiki  ambacho  ni  kiasi kikubwa  sana  cha  pesa.  Ni mpumbavu  tu ndio  anae  weza  kukataa  ofa  nzuri  kama  hiyo. HAKUNA  MTU ASIEPENDA  PESA.   HATA  WAZAZI  WENU  WANAWEZA  KUWA  WANAWAPENDA  SAWA  SAWA  WAKATI  MKIWA  WATOTO  WADOGO.  LAKINI  PINDI  MTAKAPO  ANZA  KUJITEGEMEA  WATAMPENDA  NA KUMBARIKI ZAIDI MTOTO WAO ANAEWAJALI NA KUWATUNZA KWA  KUWAPA  PESA  KULIKO  WEWE  AMBAE  PESA  ZAKO  UNATUMIA  KUFANYA  STAREHE  NA  HUPELEKI MATUNZO  KWA  WAZAZI  WAKO.

Imesimuliwa  na  DOKTA.  MUNGWA  KABILI....0744  000  473.


from MPEKUZI

Comments