Moto wateketeza nyumba, Watano Wanusurika

Watu watano wamenusurika kifo baada ya nyumba wanayoishi kuteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Alhamisi Januari 25,2018 eneo la Mitondooni wilayani Magharibi B, Unguja.

Chanzo cha moto kinaelezwa kuwa ni hitilafu ya umeme ndani ya nyumba waliyokuwa wakiishi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali amesema moto ulitokea saa moja usiku.

Mayasa Makame aliyenusurika katika janga hilo amesema moto ulizuka ghafla walipokuwa wakipika.

Amesema wamepoteza kila kitu kilichokuwamo ndani.

Kuhusu chanzo cha moto imeelezwa huenda ikawa ni hitilafu ya umeme kwenye jokofu.

Mayasa ameiomba Serikali na wananchi kwa jumla kuwasaidia kwa kuwa hawana chochote kwa sasa.


from MPEKUZI

Comments