Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Jingu Aipeleka Kampeni Ya Makazi Bora Monduli

Na Mwandishi Wetu Arusha
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amewataka wananchi kuhakikisha wanaboresha makazi yao kutoka makazi ya nyumba za nyasi na tembe kwenda nyumba za tofali na bati.

Aliyasema hayo leo Wilayani Monduli mkoani Arusha alipokuwa akitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyoamasishwa na wataalam kutoka Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli kwa kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika miradi ya Maendeleo.

Dkt. Jingu aliwataka wataalam wa Maendeleo ya Jamii nchini kuhakikisha wanakuwa chachu ya mabadiliko na wanawezesha jamii kuwa na mawazo chanya ya kujiletea maendeleo na kubadili changamoto kuwa fursa za kimaendeleo.

"Wataalam wa Maendeleo ya Jamii tuweke nguvu katika kuhakikisha tunabadili jamii zetu kuwa na mawazo chanja hasa ya kujitegemea na kujiletea maendeleo" alisema Dkt. Jingu.

Dkt. Jingu aliongeza kuwa Sekta ya Maendeleo ya Jamii inapaswa kuwa chachu ya maendeleo katika taifa letu hivyo Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vinatakiwa kutoa wataalam wenye weledi na stadi za kubwa za kuleta mabadiliko katika jamii.

"Vyuo vya Maendeleo ya Jamii tutoe wataalam wenye weledi  wa kuhakikisha tunatumia fursa zilizopo katika jamii kutatua changamoto zilizopo" alisema Dkt. Jingu.

Wakati huohuo akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli Dkt. Jingu amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuhakikisha wanatumia stadi watakazopata kubadilisha maisha yao na jamii kwa ujumla.

Dkt. Jingu aliwataka wanafunzi hao kuitumia bahati ya kuwa mmoja ya wanafunzi katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli kwa kuhakikisha wanafanikisha ndoto zao walizozilenga kuzitimiza katika maisha yao kwa kuzingatia masomo na nidhamu.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli Bw. Elibariki Ulomi alimuhakikishia Katibu Mkuu kuwa Chuo hiyo kitahakikisha kinashirikiana na wananchi wa Wilaya ya Monduli katika kutekeleza Kampeni ya Makazi Bora ili kuwawezesha wananchi kuboresha makazi yao na kuhakikisha kinatoa Wataalam wa Maendeelo ya Jamii watakosaidia kuleta mabadiliko katika taifa.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Monduli Bi. Rose Mhina alisema kuwa Halmashauri hiyo imeshaanza kutekeleza kampeni ya Makazi bora kwa kuipeleke ajenda hiyo kwa madiwani na kutoa michoro maalum kwaajili ya ujenzi wa nyumba bora za gharama nafuu.

Aliongeza kuwa Kampeni hiyo ya kuhamaisha ujenzi wamakazi bora itahamasishwa na katika jamii na maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka wilayani maoaka kwemye kata ili kuhakikisha wananchi wanajitoa na kuboresha makazi yao.

Kampeni ya Kuboresha makazi inalenga kuiwezesha jamii ambayo inaishi katika makazi yasiyo bora kuweza kuboresha makazi yao kwa kutumia ramani ziliziotolewa na Halmashauri walizopo zikiwa ni nyumba za gharama nafuu.

MWISHO.


from MPEKUZI

Comments