Serikali Kuanzia Mwakani Kuanza Kupima Ardhi Nyote Nchini

Na Ahmed Mahmoud Arusha
SERIKALI imesema kuwa kipindi cha miaka 10 ijayo kuanzia mwakani itahakikisha eneo lote nchini linapimwa na kutengenezewa misingi ya matumizi bora ya Ardhi kwa lengo la kuondoa migogoro na kuongeza thamani ya Ardhi sanjari na kutoa hati miliki.

Aidha zoezi hilo la kupanga matumizi sahihi ya Ardhi linaenda sambamba na kuowanisha sera za watumiaji wa rasilimali  mbalimbali kama vile misitu maji madini ambazo zote zipo kwenye Ardhi hivyo kuona umuhimu wa kupanga kwa ujumla matumizi sahihi ya Ardhi.

Akizungumza kwenye mkutano wa majadiliano ya mandhari ya mazingira na matumizi sahihi ya Ardhi kwa nchi za Afrika unaoshirikisha nchi zaidi ya 20 za bara la Afrika Waziri wa Ardhi nyumba na makazi William Lukuvi alisema kuwa mkutano huo ni muhimu na umekuja wakati muafaka serikali ikiwa kwenye mchakato wa kuandaa upimaji wa Ardhi nchini.

“Tumeshafanikiwa kwenye wilaya tatu nza mkoa wa Morogoro ambazo ni Malinyi Ulanga na Kilombero kupanga kila kipende cha Ardhi na kuwezesha kutoa hati zaidi ya laki tano za kimila kwa kipndi ncha miaka minne sasa tuaenda kwenye ajenda kubwa ya kupanga kupima na kumilikisha ardhi ya Tanzania” Alisema Lukuvi

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Tume ya Taifa mipango ya matumizi bora Ardhi chini ya wizara ya Ardhi Dkt.Steven Nindi alisema kuwa eneo la Tanzania lina ukubwa wa takribani kilomita za mraba zipatazo  milioni moja hivyo katika mkutano huu wanaangazia namna ya kupata rasilimali fedha na rasilimali watu ili kuharakisha zoezi zima la upangaji,usimamizi na utekelezaji wa matumizi bora ya Ardhi.

Alisema lengo ni kuhakikisha Ardhi nzima hapa nchini inapimwa na kupangwa matumizi bora na endelevu kwa maendeleo endelevu ya rasilimali za misitu maji madini kuhakikisha tunakuwa na sera moja itakayosaidia kuondoa wigo na kuhimiza fursa kwa matumizi bora ya rasilimali mbali za ardhi.

Nae Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya Mipango ya Matumizi  bora ya Ardhi ,Wakili Fidelis Mutakyamilwa  alisema katika muda wa miaka kumi Taznania itakuwa imekamilisha mpango wa matumizi bora ya Ardhi ambayo itasaidia kuondoa migogoro ya muda mrefu hapa nchini.

Amesema kuwa mkoa wa Morogoro na Arusha inaongoza kwa migogoro ya ardhi hususani Rasilimali mifugo kwa mkoa wa Arusha iliyopeleka migorogoro ya wafugaji na wakulima wakigombea malisho huku wengine wakiwa ndani ya hifadhi hivyo kuleta changamoto baina ya Tanapa NCAA na wafugaji.


from MPEKUZI

Comments