Polisi Arusha Wafanikiwa Kukamata Bunduki Mbili Za Kivita Na Nyara Za Serikali

Na Ahmed Mahmoud Arusha
JESHI la polisi mkoani hapa limefanikiwa kukamata bunduki mbili za kivita pamoja na nyara za serikali ambazo ni nyama ya twiga pamoja na vipande viwili vya meno ya tembo sanjari na silaha za jadi yakiwemo mapanga,sime na visu.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa,Jonathan Shana alizitaja silaha hizo kuwa ni AK 47 yenye namba 174364 ikiwa na risasi 6 kwenye magazine na G3 yenye namba A36011858 ikiwa na risasi 9ndani ya magazine na kwamba zilikamatwa katika eneo la Naani lililopo katika mpaka wa Tanzania na Kenya tarafa ya Loliondo Mkoani hapa.

Alisema kukamatwa kwa silaha hizo kunatokana na ushirikiano kati ya jeshi la polisi,Tanapa,Hifadhi ya Ngorongoro,kikosi dhidio ya ujangili(KDU)Kanda ya kaskazini na kikosi kazi cha taifa kinachopambana na ujangili kanda ya ziwa katika operesheni inayorndelea huko Loliondo.

“Bunduki hizo zilipatikana baada ya majibizano ya risasi baina ya kikosi kazi hicho kabambe na majangili mara baada ya kuona mashambulizi yamezidi majangili hao walitelekeza silaha hizo na kukimbilia nchi jirani,hata hivyo kikosi kikosi hicho kilifanikiwa kumjeruhi kwa risasi jangili mmoja ambaye pia alifanikiwa kukimbia huku akivuja damu”alisema Shana.

Kamanda huyo wa polisi aliongeza kuwa mnamo tarehe 10 mwezi wa 11 mwaka huu katika eneo la Oleng’usa kijiji na kata ya oloipiri ndani ya eneo la pori tengefu la Loliondo walifanikiwa kukamata watu wawili wanaojihusisha na ujangili ambao ni Yamhanga Mwita(19)na Chacha
Marwa(20) wakazi wa Serengeti Mkoani Mara wakiwa wameuwa Twiga.

Alisema kuwa watuhumiwa hao walikutwa wakiwa wanaendelea kuanika nyama hizo porini kwa ajili ya kusafirisha baada ya kuwa wamezikata vipande vipande ambapo ndio waliokutwa na panga,sime mbili,kisu tochi pamoja na nyaya za kutegea wanyama zikiwa katika mafungu saba.

Kuhusu meno ya tembo alisema kuwa tarehe 10 mwezi wa 11 mwaka huu majira ya 17:40,maeneo ya mbuyuni wilayani Arumeru waliwakamata watu watano wakiwa na meno hayo pamoja na pikipiki mbili aina za Kinglion namba T917 BUA na Sunlag namba MC 819 ACD ambapo walitokea wilayani Simanjiro mkoani Manyara walipokuwa wameyahifadhi na kwamba walikuja
Mkoani hapa kwa ajili ya kuyauza.

Kadhalika Kamanda Shana alisema kuwa polisi inawashikilia Juma Yahaya(33)na Amani Mbise(32) wanaojishughulisha na kusajili laini za simu,wakazi wa jijini hapa kwa tuhuma za kutumia jina la Gavana wa benki kuu ya Tanzania(BOT)Profesa Frorence Luoga katika mitandao ya kijamii na kuwatapeli watu mbalimbali kwa kutumia jina hilo ambapo baada ya upelelezi wamekiri kosa hilo.

“Baada ya kuwapekuwa watuhumiwa tuliwakuta na simu 6,mashine mbili ya kusajili kwa alama za vidole,laini mbalimbali,vitambulisho 9 ya wateja ambao walishawasajilia laini zao za simu na kwamba tumebabaini mtuhumiwa huyu anamiliki jumba la kifahari eneo la Sombetini jijini hapa hali ambayo aiendani na kipato chake”alisema

Aliongeza kuwa pia jeshi la polisi kwa kushirikiana na Idara ya ya ustawi wa jamii jiji la Arusha imefanya operesheni ya kuwaondoa watoto wadogo wanaofanya biashara mbalimbali ikiwemo kubebeshwa mizigo kati masoko mbalimbali ya jijini hapa ambapo waliwakamata watoto 105 ambapo kati yao 46 wana umri chini ya miaka 18 na 59 wana umri wa zaidi ya
miaka 18.


from MPEKUZI

Comments