Wanafunzi wavalishwa maboksi Kichwani ili Kuzuia Wasiangaliziane

Chuo cha The Bhagat Pre-University College, kilichopo nchini India kimeomba msamaha kufuatia kitendo cha kuwavalisha maboksi, Wanafunzi ili kuzuia kupiga chabo wakati wa majaribio ya zoezi hilo.

Taarifa za chuo hicho kufanya tukio hilo, zilisambaa baada ya kupostiwa katika mtandao wa kijamii wa Facebook na mmoja wa wafanyakazi katika chuo hicho ambazo zilionesha wanafunzi wamevaa maboksi, huku sehemu ya mbele la maboksi hayo yapo wazi.

Msamamizi mkuu wa chuo hicho, MB Satish, amesema walitumia njia hiyo kukabiliana na udanganyifu wa kupiga chabo kwa wanafunzi na walifanya hivyo kama jaribio la muda tu kisha waliwatoa maboksi hayo kichwani.

"Hakuna mwanafunzi aliyelazimishwa kuvalia boksi kichwani. Kama unavyoona katika picha hizi kuna baadhi ya wanafunzi ambao hawajazivalia, Waliokuwa wamevalia pia baadhi yao walivua baada ya dakika 15, wengine baada ya dakika 20 na hata sisi wenyewe tuliwambia wazivue baada ya saa moja" amesema MB Satish

"Kati ya wanafunzi 72 ni 56 ndiyo walivaa maboksi kama sehemu ya majaribio, walisema wanajisikia vizuri na jaribio hilo na chuo hakijamsumbua mwanafunzi yeyote kuhusu suala la kuvaa maboksi hayo" ameongeza.

Mamlaka ya usimamizi wa shule nchini India iliamuru chuo hicho kutoa ufafanuzi wa maelezo na kuomba  msamaha juu jaribio hilo.


from MPEKUZI

Comments