Mvua Yasababisha Vifo vya Watu 13 Morogoro Wakiwemo wanafunzi 9

Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini zimesababisha vifo vya watu 13 Mkoani Morogoro huku kati yao watoto wakiwa ni tisa (miaka 11 hadi 15)

Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Wilbroad Mutafungwa amesema tukio la kwanza ni la watoto watano waliofariki baada ya kuzama Mto Mvuha uliopo kata Kibogwa

Watoto hao ni Neema Rajabu (10), Latifa Khalid (9), Munila Khalid (11), Omary Khalid (14) pamoja na Zanisha Adam (9) ambaye mwili wake bado haujapatikana na shughuli ya kumtafuta inaendelea.

Mutafungwa alibainisha kuwa Said Rajabu (11) mwanafunzi wa darasa la tatu aliyekuwa na wenzie waliokufa alinusurika na kujeruhiwa baada ya kuona maji yakizidi, alikimbia na baadaye alianguka na anaendelea na matibabu katika zahanati ya Kibogwa.

Wengine waliokufa ni wanafunzi wawili wa Shule ya Msingi Kibwaya Tarafa ya Mkuyuni, Rajabu Issa (11) na Shabani Msimbe (15), baada ya kutumbukia kwenye dimbwi la maji walipokuwa wakiogelea.

Wanafunzi wengine wawili waliokufa maji ni Karim Athuman (13) na Hussein Hassan (14) wa Shule ya Msingi Ulundo waliozidiwa na maji wakiwa wanaogelea mto Ngerengere.


from MPEKUZI

Comments