Malawi Yakanusha Kuwa Na Mgonjwa Wa Ebola

Malawi imekanusha ripoti zilizoenea kwamba mtu mmoja amegunduliwa kuwa na Ebola kwenye eneo la Karonga linalopakana na Tanzania.

Hofu hiyo ilitokea Jumapili wakati wafanyakazi wa afya kwenye eneo hilo waligundua mwanamume mwenye umri wa miaka 37 kuwa na dalili za Ebola.

Afisa wa afya katika eneo hilo,  Louis Tukula amesema mtu huyo alikuwa na maambukizi ya bakteria na si Ebola.

Amesema eneo hilo limekuwa katika hali ya tahadhari tokea ugonjwa wa Ebola uripotiwe katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.


from MPEKUZI

Comments