Askofu Ruwa’ichi Aondolewa Mashine

Hali ya Askofu Mkuu wa Jimbo la Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Yuda Ruwa’ichi, inaendelea kuimarika baada ya kutolewa katika mashine iliyokuwa inamsadia kupumua na kuendelea kufanya mazoezi.

Askofu Ruwa’ichi alifikishwa Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Muhimbili (Moi) akitokea Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro (KCMC) Jumatatu saa tano usiku ambako alifanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo kwa saa tatu.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Moi, Patrick Mvungi jana alisema  kuwa jopo la wataalamu wa afya saba wanafuatilia hali ya Askofu Ruwa’ichi kila baada ya saa moja.

“Kwa sasa Askofu bado yuko ICU, lakini hatumii mashine ya kusaidia kupumua, hii inaonyesha dalili nzuri na pia wataalamu wameanza kumfanyisha mazoezi ya viungo akiwa kitandani, hivyo watu wasiwe na wasiwasi kwa sababu afya yake inaendelea kuimarika siku hadi siku.

“Baada ya mazoezi ya kitandani ataanza mazoezi ya kutembea na baada ya afya yake kuimarika zaidi  atahamishiwa High Depend Word (HDU). Hii wodi ni maalumu kwa ajili ya wagonjwa ambao afya zao zimeimarika,” alisema Mvungi.


from MPEKUZI

Comments