PICHA: Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa atembelea makaburi ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini Yaliyopo Morogoro

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa leo Ijumaa Agosti 16, 2019 ametembelea makaburi ya wapigania uhuru wa nchi hiyo yaliyopo eneo la Mazimbu mkoani Morogoro.

Akiwa na mwenyeji wake waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, rais huyo amefika eneo hilo linaloitwa Solomon Malangu, ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipochaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa nchi hiyo.

Ameonyeshwa nyumba ambayo wapigania uhuru hao walikuwa wanazikwa kijeshi, pia amepanda mti, kuweka shada la maua katika mnara wa mashujaa uliojengwa eneo hilo.



from MPEKUZI

Comments