PICHA: Marais 11 kati ya 16 Wahudhuri Mkutano wa SADC Tanzania

Marais wa nchi 11 wamehudhuria mkutano wa kilele wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) unaofanyika jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Agosti 17, 2019 na kesho.

Mkutano huo umeanza saa 3:49 asubuhi na kuhudhuriwa na marais na mawaziri kutoka nchi wanachama, marais wastaafu, viongozi na washiriki mbalimbali.

Marais hao ni John Magufuli (Tanzania),  Cyril Ramaphosa (Afrika Kusini), Azali Assoumani (Comoro),  Danny Faure (Shelisheli),  Joao Manuel Goncalves (Angola).

Wengine ni Edgar Lungu (Zambia), Felix Tshisekedi (DRC),  Andry Rajoelina (Madagascar), Emerson Mnangagwa (Zimbabwe), Filipe Nyusi (Msumbiji) na Dk Hage Geingob (Namibia).

Nchi  ya Eswatin imewakilishwa na waziri mkuu,  Ambrose Dlamini;  Lesotho pia imewakilishwa na waziri mkuu, Motsahai Thabane  huku Malawi ikiwakilishwa na makamu wa rais sambamba na Botswana na Mauritius zilizotuma wawakilishi.

==>>Walioshiriki Mkutano huo ni pamoja na;
1. Wakuu wa nchi  (Marais) 11
2. Wawakilishi wa Wakuu wa Nchi 5
3. Rais na Makamo wa Rais wa Zanzibar
4. Makamu wa Rais  na Waziri Mkuu ambao wamewakilisha nchi zao
5. Wamo Marais wastaafu wa Tanzania na Zanzibar
6. Wamo Mawaziri Wakuu Wastaafu
7. Mawaziri wa SADC 

8. Ujumbe wa  Benki ya Maendeleo Afrika -AfDB_Group
9. Wakuu wa Mikoa
10. Katibu Mkuu Kiongozi na Wastaafu wengine
11. Makatibu Wakuu
12. Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na wastaafu


Idadi ya watu ndani ya  ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC)  ni kubwa  kiasi kwamba baadhi wamekosa  sehemu za kukaa.


from MPEKUZI

Comments