Waziri Jafo Atoa Rai Kwa Wazazi Kutowasumbua Watoto Kuwapeleka Shule Binafsi.

Na.Faustine  Gimu  Galafoni,Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)SELEMANI JAFO Amewataka wazazi kutowasumbua watoto wao kwa kuwahamisha shule za serikali na kuwapeleka shule binafsi.

Akizungumza   leo Julai 12,2019 na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma waziri Jafo  amesema   shule za serikali  zimefanya vizuri ikilinganishwa na ufaulu wa hapo nyuma ambapo kila mtu alizibeza

  Waziri Jafo  amebanisha  siri ya shule za serikali kufanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha sita mwaka 2019 kuwa ni kutokana na uwekezaji uliofanywa kwenye sekta ya elimu . 

Hivyo Uwekezaji huo umepelekea ufaulu kupanda kutoka asilimia 98.2 hadi 98.93,shule nne za serikali kuingia katika kumi bora ya kwanza na katika shule 100 bora mwaka huu shule 64 ni za serikali ambazo 52 ni za kata na 12 ni shule kongwe na vipaji maalum.
 
JAFO ametaja shule nne zilizoingia 10 bora kuwa ni Kisimiri, Mwandeti, Tabora boys na Kibaha.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo ameipongeza mikoa mitatu ambayo ni Arusha, Tabora na Pwani ambazo shule za serikali zimefanya vizuri kwa kuingia 10 bora. 

 Hata  hivyo,Waziri Jafo  ameagiza kufanyika  tathmini kwa mkoa wa Mara ambao takribani shule 3 zipo kwenye kundi la shule zilizofanya vibaya katika matokeo hayo.


from MPEKUZI

Comments