Kigwangalla Afafanua kuhusu Sanamu ya Baba wa Taifa Iliyozua Mijadala Mitandaoni

Baada ya uzinduzi wa hifadhi hiyo  Jumanne Julai 9, 2019 uliofanywa na Rais John Magufuli, mjadala uliibuka katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa sanamu haifanani na mwonekano wa Rais wa Awamu ya Kwanza.

Lakini Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema kama kuna upungufu wizara hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ndiyo wenye dhamana ya kuangalia kama ina kasoro ili ifanyiwe marekebisho.

Waziri huyo amesema wana wataalam watakaoitazama sanamu hiyo na kujua kama ina upungufu na kurekebishwa.

"Kwa nia njema kabisa Wizara yetu iliamua kumpa tuzo maalum Rais Magufuli ambayo ina maneno aliyoyasema Mwl. Nyerere mwaka 1961, lakini nimeona imezua mjadala sana kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii jambo ambalo ni zuri imeweka alama

“Hatuyapuuzi maneno na comment za Watanzania wenzetu ambayo yanahusiana na uumbaji wa lile sanamu,kama kuna mapungufu sisi ndio wenye dhamana ya kuangalia kama liko sahihi, Wataalamu tunao Serikalini tutawaita watuelekeze kama kuna mapungufu yatarekebishwa

“Vijana na Wanasiasa wanaozungumza kwenye mitandao tunawashukuru kwa comment zao na tunawatoa wasiwasi kuwa tutalishughulikia, jambo ambalo limenifurahisha ni kwamba vijana bado wanaikumbuka taswira halisi ya Mwl.Nyerere,ni jambo kubwa sana kwetu kama Taifa.”

“Nimefurahishwa pia na mjadala wa faru Rajabu ambaye pia yupo kwenye mikono salama ya TANAPA na anaendelea kufanya kazi yake vizuri kabisa bila shida, tutatafuta mtoto wake mmoja machachari tutamleta kwenye Hifadhi ya Burigi Chato" Amesema Kigwangalla.

==>>Msikilize hapo chini


from MPEKUZI

Comments