Upelelezi kesi ya kina Maimu haujakamilika

Upande wa Jamhuri kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA), Dickson Maimu na wenzake, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa kesi inayowakabili vigogo hao haujakamilika.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo  ni Meneja Biashara wa (Nida), Avelin Momburi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers,  Astery Ndege, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.

Wakili wa Serikali, Janeth Magoho, alieleza hayo juzi mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mmbando  wakati kesi hiyo ilipokuwa inatajwa na kuiomba Mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo, Hakimu Mmbando aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 28, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa tena.

Maimu na wenzake wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi pamoja na kuisabishia Serikali hasara ya Sh bilioni 1.175.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 100 kati ya hayo, 24 yakiwa ni ya utakatishaji fedha zaidi ya Sh bilioni 1.1,   23 ya kughushi nyaraka; 43 ni kiwasilisha nyaraka za uongo  kumdanganya mwajiri wao  na kuisababishia mamlaka hiyo hasara.


from MPEKUZI

Comments