Serikali yatoa sababu ya kuvunja mkataba na kampuni ya kununua korosho kutoka Kenya

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda amesema Kampuni ya Indo power ya Kenya iliyokuwa imeingia mkataba wa kununua korosho tani 100,000 ilistahili na ilkuwa halali.

Kakunda ameyasema hayo wakati akihitimisha hotuba yake ya bajeti bungeni jana, Mei 15, ambapo alisisitiza kuwa kampuni hiyo inatambulika nchini Kenya, Afrika Mashariki na dunia nzima.

Alisema kilichosababisha Tanzania kuvunja mkataba huo ni baada ya kampuni hiyo kuchelewa kukamilisha taratibu kadhaa walizokubaliana.


from MPEKUZI

Comments