Watoto Watatu Wabakwa Jijini Mbeya....Wahamiaji Haramu 10 Watiwa Mbaroni

JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAWASHIKILIA RAIA 10 WA NCHINI ETHIOPIA KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI KINYUME CHA SHERIA. PIA KATIKA MISAKO MBALIMBALI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU KADHAA.

KUPATIKANA NA MALI IDHANIWAYO KUWA YA WIZI.
Mnamo tarehe 10/02/2019 majira ya saa 15:45 Alasiri huko maeneo ya Mapelele, Kata ya Nsalala, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya vijijini, Mkoa wa Mbeya askari Polisi wakiwa kwenye msako walifanikiwa kukamata mali mbalimbali zinazodhaniwa kuwa ni za wizi ambazo ni:-

  1.     Meza moja ya TV,
  2.     TV moja aina ya zec inch 21,
  3.     Radio moja subwoofer aina ya kodjec,
  4.     Speaker nne,
  5.     Deck aina ya ailiang,
  6.     Extention moja,
  7.     Godoro moja la futi 5 x 6 super banco
Mali hizo zilikutwa nyumbani kwa AUGUSTINO GODFREY. Pia katika msako huo ilipatikana meza moja ya kioo na extention moja mali ambazo zimetambuliwa na mlalamikaji HERMAN PELLO kuhusiana na kosa la kuvunja nyumba usiku na kuiba. Upelelezi unaendelea ikiwa ni pamoja na msako mkali wa kumkamata mtuhumiwa.

KUPATIKANA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.
Mnamo tarehe 07/02/2019 majira ya saa 1700 jioni huko Mapelele, Kata  ya Nsalala, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini na Mkoa wa Mbeya askari Polisi walimkamata mtu mmoja aitwaye ANASTAZIA KALINGA [32] mfanyabiasha na mkazi wa Iwambi akiwa na pombe kali zilizopigwa marufuku nchini aina mbalimbali:-

  1.     Pombe kali aina ya fedor chupa 18,
  2.     Prince chupa 03,
  3.     Veve chupa 18,
Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani.

KUINGIZA BIDHAA NCHINI BILA KIBALI.
Mnamo tarehe 16.02.2019 majira ya saa 21:00 usiku huko Mwakapangala, Kata ya Nsalala, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakifanya upekuzi katika magari mbalimbali walimkamata PRISCA PETER [32] mfanyabiashara, mkazi wa Uyole akiwa na:-

  1.     Pombe aina ya Prince chupa 20,
  2.     Kinywaji aina Power asili chupa 60,
  3.     Maziwa aina ya Super shake chupa 12,
  4.     Biscuits aina chiko dazan 2
Bidhaa hizo zote hazikulipiwa ushuru akiwa anazisafirisha kwa kutumia coaster ya abiria kutoka tunduma kuja Mbeya. Chanzo cha tukio hili ni kujipatia kipato kikubwa kwa kukwepa kulipa kodi ya mapato.

Mbinu iliyotumika ni kununua bidhaa hizo huko eneo la Black nchini Zambia katika duka la mtu mmoja raia wa Zambia [Jina linahifadhiwa] na kuvusha kwa njia za panya kwa kumtumia bodaboda ambaye husafirisha bidhaa hizo mpaka eneo la Sogea Stand alafu hupakia bidhaa hizo katika gari za abiria aina ya coaster na kuzipeleka wanakopanga kuzipeleka kwa wateja mbalimbali.

Mtuhumiwa amehojiwa na kukiri kufanya biashara hiyo. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika atafikishwa Mahakamani.

KUINGIA NCHINI BILA KIBALI [WAHAMIAJI HARAMU].
Mnamo tarehe 19/02/2019 majira ya saa 18:15 jioni huko kijiji cha Mpakani kilichopo Kata ya Lugelele, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali na Mkoa wa Mbeya katika barabara itokayo Njombe kuelekea Mbeya askari Polisi wakiwa doria waliwakamata wahamiaji haramu kumi (10) wote raia wa Ethiopia wakiwa wanatembea kwa miguu pasipokuwa na vibali vya kuishi nchini.

Wahamiaji hao wamefahamika kwa majina ya:-

  1.     FREDIT ZILITA [18]
  2.     MURUNA ELIGETE [19]
  3.     NESENETA ETORE [19]
  4.     ABDALAHMAN ISSAYA [20]
  5.     TASFEI TILIKASO [21]
  6.     DEUD DEGU [20]
  7.     BAZABU WAVANO [27]
  8.     TEKA JILLE [30]
  9.     ALDUNAR TAVARA [25]
  10.     SHAMSON RULLO [25]
Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa Mahakamani.

KUBAKA – WILAYA YA MBEYA VIJIJINI.
Mnamo tarehe 16.02.2019 saa 08:00 asubuhi huko maeneo ya Lumbila, Kata ya Utengule, Tarafa ya Utengule Usongwe, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi na Mkoa wa Mbeya.  Binti aitwae HIDAYA HABIBU [15] mwanafunzi kidato cha tatu Shule ya Sekondari Malenga alikamatwa kwa nguvu kisha kuingiliwa kimwili na babu yake mzaa mama yake aitwaye ALINANI MWAKIFUNA [59] mkazi wa Chapakazi ambaye ni Mwalimu Mkuu katika Shule ya Msingi Mwaselela.

Chanzo cha tukio hilo ni tamaa ya ngono. Mbinu iliyotumika ni kumshawishi amsindikize shambani kwake huko lumbila na kumuingiza ndani ya banda analo tunzia majembe na vifaa vya kilimo kisha kumlaza chini na kumuingilia kimwili. 


Muhanga kwa kuwa anaishi na babu yake huyo ambaye ndiye mtuhumiwa aliogopa kumjulisha mama yake ambaye ni mkazi wa huko chapakazi na ambaye alikuwa amefanyiwa upasuaji mkubwa wa tumbo mpaka tarehe 18.02.2019 saa 22:00 usiku babu yake huyo alipomtaka tena kingono ndipo alipolazimika kumjulisha kaka yake aitwaye OMARY HABIBU, mkazi wa Uyole kwa njia ya simu ndipo kaka yake aliamua kumjulisha mama yake. Mtuhumiwa amekamatwa. Upelelezi unaendelea.

KUBAKA – WILAYA YA KYELA.
Mnamo tarehe 16.02.2019 saa 20:00 usiku huko maeneo ya Kilasiro, Kata ya Ikimba, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Mtoto aitwaye JOYCE SAMWEL [09] Mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Kilasiro alibakwa na SAMWEL MSUKILA [22] mkazi wa Kilasiro. Taarifa kituoni tarehe 19.02.2019 na BHAJILE ISAME ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo. Mtuhumiwa amekamatwa. Upelelezi unaendelea.

KUBAKA – WILAYA YA MBEYA VIJIJINI.
Mnamo tarehe 19.02.2019 saa 18:00 jioni huko mtaa wa Mapelele, Kata ya Nsalala, Tarafa ya Utengule – Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya. Mtoto aitwae IRENE EZEKIA [03] alikamatwa kwa nguvu kisha kubakwa na mtu aitwae CHARLES KAKOLA [30] mkazi Iwindi. Chanzo cha tukio hili ni ulevi wa pombe. 


Mbinu iliyotumika ni kumvizia akiwa anacheza mazingira ya nyumbani kwao kisha kumbeba na kumuingiza ndani ya shamba la mahindi na kumbaka. Mtuhumiwa amekamatwa na kukiri kuhusika katika tukio hilo. Muhanga amepatiwa matibabu na kuruhusiwa kurudi nyumbani. Mtuhumiwa amekamatwa na upelelezi unaendelea.


from MPEKUZI

Comments