Wamiliki wa Shule Binafsi Wakutana Dodoma

Na.Faustine Gimu Galafoni,DODOMA.
Mdhibiti mkuu wa Ubora wa Elimu Kanda kati ,Bw.Sospeter Magina    Jana Februari  19,2019  amefanya kikao na wamiliki wa Taasisi binafsi za Elimu  mkoani Dodoma  na kujadili Masuala mbalimbali ya kielimu ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kuzingatia maadili katika taasisi zao.
 
Akizungumza  Katika  kikao hicho kilichofanyika shule ya sekondari Dodoma ambacho kimekutanisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwamo maafisa elimu msingi na sekondari jiji la Dodoma,Bw.Magina alisema  suala la maadili ni la tangu zamani hivyo ni vyema  kila Shule ikazingatia kusimamia maadili ya wanafunzi na walimu.
 
“Suala la maadili halijawahi kubadilika  tangu nyaraka za miaka iliyopita tatizo ni usimamizi wa nyaraka hizo kuhusiana maadili ya  wanafunzi na walimu sio mzuri hivyo mnatakiwa kuzingatia kusimamia maadili ipasavyo”
 
Aidha ,Bw.Magina alizungumzia juu ya  suala la ufundishaji shuleni kwa kuzingatia Mtaala wa elimu  uliopo wakati mchakato wa  vitabu ukiandaliwa .
 
“Suala la mitaala ieleweke  wazi kuwa kulikuwa na shida ya vitabu  fulani vilivyokuwa vinaingia mashuleni  ,serikali  imechukua jitihada  kuhakikisha ya kwamba vitabu vipya vinaandaliwa .Taarifa nilizonazo kwa sasa karibu vinatoka ,muda wowote vinatoka .Walimu wanatakiwa kufundisha kwa kuzingatia syllabus wakati vitabu vipya vikiandaliwa.”
 
Hata hivyo Mdhibiti huyo wa ubora wa elimu kanda ya kati Dodoma alisema kuwa haiingii akilini shule za Dodoma haziingii kwenye kumi bora kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa hivyo kuna haja ya kufanya mabadiliko sasa ili mkoa huo ujipambanue vyema  na kufanya vizuri  katika masuala ya kielimu.
MWISHO.


from MPEKUZI

Comments