Nick Minaj Azipa Kisogo tuzo za BET Pamoja na onyesho la BET Experience ....Kwa Nini, Tazama Hapa

Baada ya tuzo za Grammy kumalizika Februari 10, 2019, Rapa Nicki Minaj na Young Money, wametangaza rasmi kutoshiriki tuzo za BET na kutotumbuiza kwenye onyesho la BET Experience mwaka huu baada ya kutupiwa dongo lililotoka BET.

Kupitia mtandao wa twitter wa kituo cha televisheni cha BET nchini Marekani kilionekana kurusha dongo kwa Nicki Minaj baada ya Cardi B kuondoka na tuzo ya albamu bora ya hip hop (Invasion of Privacy) katika tuzo za Grammy na kauli hiyo ilimfanya Nicki kuchukua maamuzi hayo akiwamo Lil Wayne ambaye alitajwa kutumbuiza kwenye tuzo za BET Juni, 2019.

“Wakati huu Nicki Minaj amevuta na wigi lake,” kilisikika kikimponda rapa huyo.
Baada ya muda mfupi BET wameamua kumwomba msamaha Nicki Minaj kutokana na kauli yao waliyoitoa dhidi yake na kusema kuwa wanampenda na wamechukua hatua ya kuifuta tweet hiyo na wako tayari kwa lolote ili kuliweka tukio hilo sawa.

Rapa huyo ameahidi kuongea kila kitu kuhusu kushindwa kwake kupata tuzo kupitia radio yake ya Queen na kusisitiza kuwa mashabiki wanatakiwa kujua ukweli na pia Nicki alimaliza kwa kuwapongeza wale wote walioshinda tuzo za Grammy.


from MPEKUZI

Comments