Malkia Meno ya Tembo Ahukumiwa Jela Muaka 17

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu miaka 17 jela wafanyabiashara watatu akiwemo Raia wa China Yang Feng Glan 'Malkia wa Tembo' baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kufanya biashara haramu ya meno ya Tembo.

Kila mmoja atatumikia kifungo cha miaka 17 baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh13bilioni.

Mbali na Glan, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 21/2014  ni Salvius Matembo na Philemon Manase.

Hukumu hiyo umetolewa leo mchana Februari 19, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Huruma Shaidi baada ya kuwatia hatiani washtakiwa hao.


from MPEKUZI

Comments