Waziri Mkuu Majaliwa Kufungua Mkutano Wa Maafisa Ustawi Wa Jamii

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kufungua mkutano wa siku tatu wa maafisa ustawi wa jamii mikoa 26 na halmashauri zote nchini wenye lengo la kujadili utendaji kazi, utoaji huduma za ustawi wa jamii na mifumo ya utendaji kazi.

Akizungumza na mwandishi wa habari jana jijini hapa, Mkurugenzi Msaidizi  wa Huduma za Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais Tamisemi, Rashid Maftaha, alisema kuwa  mkutano huo unatarajia kuanza Januri 29 hadi 31 mwaka huu jijini Dodoma.

Alisema kuwa  mkutano huo unatarajia kushirikisha washiri takribani 370 ikiwamo maafisa ustawi wa jamii wa mikao 26, halmashauri 184, wadau wa maendeleo, na wizara za kisekta ambazo zinahusiana na utoaji wa huduma za ustawiwa jamii, kama wizara ya elimu, afya, Katiba na Sheria, Viwanda na Biashara, madini na kilimo.

“ Unaweza jiuliza, Wizara ya Madini inahusikajie na huduma za ustawi wa jamii, hawa ni wadau muhimu, kwani kwenye migodi kuna utumikishwaji wa watoto, na hata watumishi wake wanakuwa wako mbali hivyo ni lazima wafikiwe na huduma za jamii, halii hii pia iko kwenye viwanda.

“Pia unaweza kujiuliza kwa nini wizara ya kilimo, lakini ukweli ni kuwa asimia 80 ya watanzania wanafanya shughuli za kilimo na asilimia 70 yao wako vijijini, na takwimu zetu zinaonesha kuwa watoto wengi walio katika mazingia hatarishi wanatoka vijijini ambaochanzo kikubwa na umasikini na jangwa la Ukwimi.

Maftaha aliongeza :” Tunashukuru wenzetu wa kilimo katika Mpango wa Maendeleo ya Kilimo kwa kwanza na huu wa pili ni jumuishi kwani kuna dirisha maalumu kwa ajili ya watu walio katika mazingira hatarishi wakiwemo, wenye ulemavu, wajane, wazee ambao wanapata pembejeo na wana uwakilishi katika kamati za ugawaji pembejeo

Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Weledi, uadilifu, uwajibikaji ni nguzo ya msingi katika kuleta usatawi wa makundi maalumu kuelekea katika uchumi wa kati wa viwanda.”

Maftah alisema kuwa : “ Tunaamini watendaji wetu kwenye halmashauri na mikoa wakifanya kazi zao kwa kuzingatia uadilifu, weledi, wakifuata sheria, kanuni na taratibu tunaamini makundi yenye uhitaji maalumu wanaweza kufikiwa inavyotakiwa hivyo mchango wao ukaongezeka katika uchumi wa viwanda,

Mkutano huu ni wa kwanza ikiwa ni takribani miaka 15 baada ya kutokea mabadiliko ya kimuundo kwa kuiondoa Idara ya Ustawi wa Jamii kutoka Serikali kuu kwenda Serikali za Mitaa.

Akifafanua zaidi, Maftaha alisema serikali ya Awamu ya Tano imekuwa ikifanya kwa vitendo katika kuwahudumia wananchi hususani wale wanyonge ikiwamo wazee, wenye ulemavu, watoto wa mitaani na wale wanaoishi katika mazingira magumu, wanawake wenye mahitaji maalumu kama wajane, wenye magonjwa sugu na walio katika kaya masikini.

Hata hivyo alisema kuwa  lengo la mkutano ni kuwakutanisha watendaji hao na kutoa mrejesho wa utekelezaji wa huduma za jamii katika maeneo ya serikali za mitaa, utendaji kazi na namna mfumo inavyofanya kazi.

“ Pia tutaangalia mafanikio na changamoto na kwa upamoja na kuja na mapendekezo ya kutatua changamoto stahiki za za kiutendaji na mfumo ili kusogeza na kuimarisha zaidi hudumua za ustawi wa jamii kwenye mamlaka ya serikali za mitaa. Kama kuna yale ambayo yatataka kuwepo mabadilko ya kisera basi tutafikisha katika mamlaka husika.

Aidha, Maftah alitumia fursa hiyo kuwaasa wananchi kuendelea kuwalinda watoto kwa kutoa taarifa haraka kwa mamlaka pale panapokuwa na viiashiria ay dalili au kitendo cha ukatili kwa mtoto.

Alisema kuwa pamoja na pamekuwa na changamoto ya ushahidi pale kesi zinapofika mahakamani au wahanga na mashahidi kubadili taarifa walizotoa awali, lakini ni vyama jamii ikaungana kutakabiliana na ukatili kwa watoto.

“Hatuwezi kukubali vitendo vya ukatili anavyofanyiwa mtoto alafu tuambiwe kuwa wamekubaliana pembeni hilo hatulikubali mpaka sheria ichukue mkondo wake.


from MPEKUZI

Comments