Waziri Jafo atoa siku 68 kwa halmashauri kurejesha fedha

Waziri  wa nchi,Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo ametoa siku 68 kwa halmashauri 4 za Kigoma Ujiji, Butiama, Liwale na Bahi kurejesha fedha za mradi wa elimu (Equip)zilizotumika kinyume na utaratibu.

Aidha ameelekeza mamlaka ya nidhamu kumchukulia hatua za kumuondoa kwenye nafasi yake afisa mipango wa halmashauri ya Bahi kutokana na kushindwa kutimiza wajibu wake.

Halmashauri hizo ni kati ya halmashauri 8 zilizotumia fedha  kinyume kiasi cha milioni 912.7 ambapo halmashauri 4 zilitekeleza agizo lake na kurejesha fedha.

"Halmashauri hizi wamenihuzunisha sana kwa kutotii maelekezo, naziagiza mpaka machi 28 mwaka huu wawe wamerejesha ili fedha hizo zitekeleze miradi iliyokusudiwa, "amesema Jafo

Mbali na hayo  amemuagiza  Naibu Waziri wake Mwita Waitara  kuwa mkali katika kusimamia miradi ya elimu agizo ambalo Waitara  ameahidi kulishughulikia.


from MPEKUZI

Comments