Tazama Hapa tarehe na sehemu itakayofanyika Fiesta baada ya kuahirishwa

Uongozi wa Clouds media group umetangaza upya tarehe na sehemu itakayofanyika Fiesta kabla ya mwaka mpya baada ya mara ya kwanza kuahirishwa katika viwanja vya Leaders jijini Dar Es Salaam.

Ikumbukwe kwamba Fiesta ilifanyika karibia mikoa 15 nchini Tanzania lakini ilipofika wakati wa kufanyika hapa Dar Es Salaam ambayo ndio ilikuwa inafunga msimu mpya wa Fiesta ilisitishwa kwa madai kwamba sehemu ambako ingeenda kufanyika ingeleta taharuki kutokana na kelele zitakazojitokeza mahala hapo.

Uongozi wa CGM umetangaza tarehe mpya na sehemu ambako Tamasha hilo litafanyika

"Tarehe 22 Disemba kwenye Viwanja vya Posta DSM, Machampion wote wa nchi wanakwenda kutoa shukrani moja kubwa na kushangalia mafanikio ya mwaka huu. 

Ni mara 2 ya tulichokimiss: stage ya viwango, sound kubwa kuliko, bata la kihistoria na list ndefu ya machampion. . #TigoFiesta2018 ". Wameandika Clouds Media



from MPEKUZI

Comments