Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 44

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588 
ILIPOISHIA   
   
Tukaingia katika awamu ya pili ya mazoezi ya taikondo. Mazoezi haya hakika ni magumu kuliko hata kukimbia katika msitu wa eneo hili. Zaidi ya masaa mawili saa Jojo na Danya wakawa wanatufundisha mazoezi haya ambayo hakika hadi tunamaliza wote watatu viungo vyetu vimeorojeka kwa kuchoka na kuapa majera kadhaa yaliyo tokana na kukosa umakini.
“Camila”
Nilimuita Camila huku tukiwa ndani ya chumba chetu, kwa maumivu niliyo nayo nikajikuta hata nikishindwa kulala kitandani.
“Mmmmm”       
“Mimi nahitaji kutoroka, siwezi kuendelea kukaa hapa”
“Mmmm…….”
“Ndio nahitaji kutoroka, maisha gani haya ya mateso naomba ujumuike nami mke wangu na tutoroke wote”
“Umewasahaua wale Simba na wanayama wengine humu msituni ehee?”

ENDELEA   
Nikakaa kimya huku nikimtazama Camila usoni mwake. Ukiachilia Simba na wanyama wengine ambao wapo katika msitu huu, ila kusema kweli hatufahamu ni wapi tulipo.
“Mume wangu wewe ni mwanaume, hakuna haja ya kukimbia mazoezi, tena ikiwa wewe ni mchezaji mpira, tena mchezaji ambaye dunia kwa sasa ina kutazama. Tafadhali nina kuomba mume wangu tuwe wavumilivu, siku na muda wa kuondoka utakapo fika basi tutaondoka”
 
“Nimekuja huku ili niwe mtalii wa kujua mambo mbalimbali ila si kuja kuwa mwanajeshi?”
“Jamani mume wangu, umesahau tabu na ngija ngija tulizo pata na kama ingekuwa si Ethan, haki ya Mungu nina apia leo sijui tungekuwa wapi?”
“Kwa hiyo unahitaji tuendelee kuwa wanajeshi wa hiyari ehee?”
“Sio wanajeshi wa hiyari mume wangu ila tunajilinda sisi wenyewe bwana”
“Sawa”
“Usiseme sawa kinyonge jamani”
Camila alizungumza huku akinikumbatia, ila kwa maumivu makali ya mwilini mwangu nikajikuta nikimsogeza pembeni kidogo.
 
“Nini”
“Mwili wote unauma bwana mke wangu”
“Hahaa hata nikikupa sasa hivi utashindwa?”
“Ndio”
 “Hahaa kweli umeshindwa mume wangu”
Camila alizungumza huku akicheka sana jambo lililo nifanya nimtazame kwa macho ya masikitiko. Usingizi ukanipitia taratibu, alfajiri na mapema kama kawaida tukaamshwa ili kufanya mazoezi kama kawaida.
“Yule jamaa yupo wapi?”
Nilimuuliza Jojo mara baaya ya kujikuta tupo wanne tu katika uwanaja wa mazoezi.
“Yupo kazini”
“Kazini kivipi?”
“Ni mfanyakazi wa moja ya benk katika hii nchi, ila siku mbili hivi atarejea”
“Sawa”
Tukaendelea kufanya mazoezi japo siku ya leo hayakuwa m agumu sana. Baada ya masaa mawili ya mazoezi tukaruhusiwa kuendelea kwa mamabo mengine binafsi.
“Ninaweza kuzungumza na baba yangu?”
 
“Kwa kutumia video call au?”
“Kama itawezekana”
“Sawa twendeni huku”
Jojo alizungumza huku tukianza kumfwata kwa nyuma. Tukaingia kwenye moja ya chumba kama ofisi, tukakuta moja ya computer kubwa kiasi. Akaiwasha na akaanza kufanya mawasiliano na baba Camila, baada ya muda kidogo akapokea msaidizi wa baba Camila.
“Hei Jonson”
Camila alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana usoni mwake.
“Hei Camila vipi upo  wapi?”
“Mmmm, nipo mbali kidogo. Ninaweza kumpata baba”
“Yupo kwenye kampeni ana hutubia kama upo karibu unaweza kuwasha televishion kumtazama jinsi anavyo hutubia”
“Ohoo inachukua muda gani?”
“Kama dakika ishirini hivi”
“Ninaweza kumsubiri nina hitaji kuzungumza naye sana”
“Sawa, akitoka basi nitamfahamisha na atawasiliana nawe”
“Sawa sawa”
 
Tukaendelea kukaa ndani ya ofisi hii kwa zaidi ya nusu saa, ndipo baba Camila akapatikana.
“Habari zenu vijana wangu”
Baba Camila alizungumza huku akiwa amejawa na furaha. Jojo akatoka ofisi humu na kutuacha sisi wawili.
“Salama tu baba, vipi kampeni zako zinaendaje?”
“Zinakwenda vizuri na kupotea kwenu kunazidi kuwapa wananchi hasira ya kuhitaji mimi niiingie madarakani ili niweze kukomesha utekaji ambao unaendelea”
“Mmmmm watu wana masikitiko?”
“Yaa wana masikitiko makubwa sana”
“Muheshimiwa samahani kidogo kwa kuwaingilia mazungumzo yenu”
“Hakuna shida Ethan, zungumza tu”
“Vipi familia yangua umeweza kuitembelea au kuwajulia hali?”
 
“Ndio nilizunguza na Mery pamoja na bi Jane Klopp na wapo salama na niliwaeleza juu ya usalama wenu”
“Nashukuru sana baba”
“Vipi Ethan mbona uso wako kama una kovu kidogo hapo usoni mwako”
“Baba huku tulipo yaani ni zaidi ya jeshini”
“Jeshini”
“Hapana baba Ethan ni uoga wake tu baba”
“Hapana baba yaani huku tunapewa mafunzo makali kiasi cha kujikuta ninapachukia huku sana”
“Baba, mume wangu na umahiri wake wote uwanjani ila anaogopa sana. Baba niamini tupo sehemu salama, naamini tukirudi tutakuwa fiti zaidi ya fiti”
Nikamaki nikimtazama Camila kwa macho ya mshangao, tukamaliza kuzunumza na baba yake kisha tukatoka ofisini humu. Tukakuta Dany aiwa amesha kifungua kinywa. Akatukaribisha mezani na tukaanza kupata kifunga kinywa.
“Leo jiandaeni tunakwenda kutembea”
“Wapi?”
Niliuliza kwa shahuku nikimtazama Dany usoni mwake.
“Nitawaambia baadaye ila mujiweke tayari kwa safari”
“Sawa muheshimiwa”
 
Tukamaliza kupata kifungua kinywa na kurudi chumbani kwetu. Camila akaanza kuvua nguo zake huku akiwa amenipa mgongo.
                                                                                                                     ***
    Tukakapewa nguo za kuondoka eneo hili kuelekea kwenye safari ambayo Dany alituahidi kwamba tunaweza kuondoka. Tulipo hakikisha  kwamba tumemaliza kujianda safari ya kuondoka aneo hili ikaanza.
“Tunaelekea wapi?”
“Kuna jambo moja nahitaji kulifanya kwa ajili ya kipaji chako”
“Mmmm”
“Camila mbona unaguna?”
“Kama tunakwenda kwenye uwanja wa mpira nahisi ni jambo la hatari  sana”
 
“Kwa nini?”
“Maadui zetu wanatuwinda”
“Mukiwa nasi hakuna adui yoote ambaye atawadhuru”
Jojo alitujibu huku akitugeukia.
“Kivipi?”
“Musijali nyinyi kuweni na amani tu”
Safari hii ikatugarimu saa moja na nusu hivi, tukafika kwenye moja ya mji mmoja wenye milima mingi na ulio jengeka vizuri kiasi.
“Hapa ni wapi?”
“Hili  eneo linaitwa Lushoto, kuna timu ya taifa chini ya miaka kumi na nane wamekuja kuweka kambi hapa kijiandaa na michuano ya kombe la dunia chini ya vijana wenye umri miaka kumi na nane.”
Dany alizungumza huku akisimamisha gari hili kwenye jengo moja la hoteli.
“Unahitaji mume wangu achezee timu ya taifa ya Tanzania ikiwa ana uraia wa Ujerumani”
 
“Ethan sio mjerumani ni Mtanzania halisi, baba na mama yake ni Watanzania. Ameishi Ujerumani kwa ajili ya matatizo ya hapa na pale”
Camila akanitazama usoni mwangu huku akiwa na masikitiko kiasi kwani kucheza mpira katika timu ya taifa ya Tanzania, basi sinto weza kucheza tena katika nchi ya Ujerumani na hii pia inaweza kuathiri kampeni za baba Camila kwa maana hata tangazo nililo lifanya la kisiasa linaashiria kwamba mimi ni Mjerumani.
“Dany samahani kidogo naomba tuzungumze”
Nilimuambia Dany huku nikisogea pembeni kidogo huku nikimtzama usoni mwake. Dany bila kujali umri wangu akanifwata sehemu nilipo simama.
“Ndio Ethan”
“Natambua kwamba mimi ni Mtanzania”
“Ndio”
“Ila kichwa changu hakina kumbukumbu yoyote kuhusiana na hii nchi hususani familia yangu. Sasa itawezekaje niweze kuichezea hii nchi ikiwa sijakua nchini hapa?”
“Kukua au kuto kulia katika nchi hii hilo sio tatizo”
“Ila”
 
“Ila fwata chimbuko la wazazi wako”
“Mimi sina kumbukumbu yoyote juu ya wazazi wangu, nitafwata chimbuko langu kivipi sasa?”
“Huna kumbukumbu za wazazi wako?”
“Ndio”
Jojo akatufwata hapa tulipo simama huku akiwa na sura ya tabasamu.
“Ethan”
“Mmmm”
“Huna kumbukumbu yoyote na wazazi wako?”
“Ndio”
“Unahitaji kufahamu ni kitu gani kilicho wapata?”
“Ndio”
Jojo akanisogelea na kunishika kichwani mwangu, nikahisi ubaridi mkali ambao taratibu katika ufahamu wangu wa akili nikaanza kuona ngurumo za radi huku mvua nyingi ikinyesha. Kumbukumbu zangu zikazidi kusonga mbele na kumuona mzee mmoja akiwa amezungukwa na kundi kubwa la vijana huku  wakimshambulia kwa kumpiga kwa magongo pamoja na mateke huku wakihitaji afariki dunia.

ITAENDELEA KESHO


from MPEKUZI

Comments