Mo Dewji Aandika Ujumbe Mzito Twitter....."Anayekufanyia Mabaya Mlipe kwa Mema"

Ujumbe wa mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’ aliouweka katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter akizungumzia kutenda mema hata kama umefanyiwa ubaya umeibua mjadala mitandaoni.

Katika ujumbe huo Mo ambaye alitekwa na watu wasiojulikana Oktoba 11, 2018 na kupatikana  Oktoba 20, 2018 ameandika, “Hutofanya ubaya kwa aliyekufanyia ubaya, ila utamsamehe na kumfanyia ukarimu.”  Mtume Muhammad (S.A.W) JumaahKareem.

Baada ya ujumbe huo watu wa kada mbalimbali wametoa maoni yao akiwemo waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki aliyesema, “Hii ni imani ya ngazi ya juu sana.”




from MPEKUZI

Comments