Kesi ya Kusambaza Picha za Uchi za Wema Sepetu kusikilizwa tena Januari 28, 2019

Kesi ya kusambaza picha za utupu inayomkabili Miss Tanzania 2016, Wema Sepetu imetajwa leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam.

Upande wa Jamhuri umedai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Hayo yamedaiwa leo Decemba 12 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili wa Serikali, Mosia Kaima, wakati kesi hiyo ilipotajwa mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde kwa ajili ya kutajwa.

Kaima aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kuitaja ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Hakimu Masonde baada ya kusikiliza maelezo hayo aliiahirisha kesi hiyo hadi Januari 28 mwakani, itakapotajwa tena.

Katika kesi hiyo, Wema anadaiwa kuwa Oktoba 15, mwaka huu katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam alichapisha video ya ngono na kusambaza katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram.


from MPEKUZI

Comments