Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 33

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA     

“Unaweza kufungua tu hiyo bahasha”
Nikaifungua bahasha hii, nikakuta picha nne ndani ya bahasha hii, nikaanza kutoa moja baada ya nyingine. Picha hizi zinamuonyesha mwana mama wa kiafrika akiwa amefungwa mikonono yake pamoja na mdomo wake na pembeni yake kuna wanaume wawuli walio shika mitutu ya bunduki.
“Hizi picha za nini kwangu?”
Mzee huyu akatabasamu huku akinitazama usoni mwangu.
“Huyo ni mama YAKO MZAZI, ana siku ya tatu toka vijana wangu wamshikilie. Biashara iliyopo hapa ni ndogo sana. Boksi jeusi, kwa uhai wa mama yako mzazi”
Maneno ya mzee huyu yakanitusha sana, nikazitazama picha hizi kwa umakini sana, taratibu taswira ya sura yangu nikaanza kuiona kwa mwanamama huyu jambo lililo nifanya nistuke huku mwili wangu ukisisimka hadi vinyweleo vyangu vya mwili vikaanza kunisiamama kwa mstuko huu nilio upata.

ENDELEA
“Mama yangu!!?”
Nilimuuliza mzee huyu huku nikimtazama kwa mshangao. Akanijibu kwa kutingisha kichwa, ila kila ninavyo jaribu kukumbuka kwamba nishawahi kuwa na mama katika maisha yangu, sina kumbukumbu hiyo.
“Nashukuru sana na sifahamu boksi hilo lililopo”
Nilipo maliza kuzungumza maneno hayo nikamsogezea mzee huyu picha zake pamoja na bahasha.
“Muda mwengine usinijaribu kwa mambo ya kijinga na kipuuzi kama haya”
Nilizungumza kwa msisitozo kisha nikanyanyuka na kaunza kuondoka.
 
“Kesho nitakuletea kidole chake”
Neno la mzee huyu likanifanya nisimame kwa muda kidogo, nikamgeukia na kumtazama kwa umakini sana kisha nikaendelea na safari yangu. Nikajumuika na wachezaji wezangu kwenye mazoezi ya asubuhi.
“Ethan mbona unaonekana huna raha?”
Kocha aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.
“Hapana kocha nipo sawa”
“Una uhakika?”
“Ndio nipo sawa”
Hata uchezaji wa uwanjani haukuwa mzuri kabisa, kwani mawazo ya maam mzazi yamenichanganya kabisa. Ila jambo ambalo lina nitatiza ni kwamba sina kumbukumbu ya aina yoyote inayo husiana na mama wala baba yangu mzazi, japo ninatambua kwamba mzee Klopp na bi Jane Klopp ni wazazi wangu.
 
“Kocha nakuomba nipumzike kidogo”
Nilimuomba kocha huku nikimtazama usoni mwake.
“Hakuna tatizo, pumzika”
Nikatoka nje ya uwanja na Camila akanikabidhi kitaulo kidogo cha kujifutia jasho mwilini mwangu.
“Mbona kama una mawazo mpenzi wangu”
“Akili yangu haipo sawa”
“Kuna nini kinacho kutatatiza?”
“Hembu twende huku”
“Mazoezi una acha?”
“Nitashiriki jioni, twende huku”
 
Nilizungumza huku nikianza kutembea kuelekea katika eneo ambalo nilikaa na mzee yule. Tulipo fika tukakua kuna watu wengine ambao walio kaa. Watu hawa wakajawa na furaha kubwa sana mara baada ya kutuona. Kila mtu akaanza kutamani tupige picha ya mapamoja.
“Tupige tu mpenzi wangu”
Camila aliniambai kwa sauti ya chini kiasi, tukaanza kupiga picha kadhaa na watu hawa kisha tukawaaga na kuondoka.
“Tunakwenda wapi Ethan?”
“Nahitaji kuingia kwenye chumba kinacho ongoza kamera za ulinzi katika hii hoteli”
“Mmmm niambie mume wangu kuna jambo gania mbalo lina endele?”
 
“Nitakueleza naomba uniazime simu yako”
Camila akanipatia simu yake, nikampigia mwana sheria wa kampuni na kumuomba aweze kufika hotelini hapa. Kutona sehemu hii tulipo ni mbali na mjini, ikamlazimu mwana sheria kupanda helicopter ya kampuni yake na kufika katika hoteli hii.
“Ethan naomba uniambie ni jambo gani linalo endelea au huniamini?”
Camila alizungumza kwa kulalama.
“Nitakuambia mpenzi wangu, nakuomba uweze kuwa mvumilivu katika hili ninalo kwenda kulifanya sawa”
“Sawa”
Camila alinijibu kwa unyonge, nikampokea mwana sheria na moja kwa moja tukaongozana naye hadi kwenye ofisi ya meneja wa hii hoteli. Meneja huyu akafurahi sana kuniona ofisini kwake.
 
“Ndio Ethan niwasiaidie nini?”
“Nahitaji kwanza ulinzi wa wachezaji wezangu, na sisi uweze kuongezwa”
“Kwa nini unazungumza hivyo Ethan?”
“Kuna hali ya hatari ambayo nimekutana nayo masaa kadhaa hapa hotelini kwako. Jambo hili litanifanya niweze kuiondoa timu yangu hapa. Nakuomba sana meneja uweze kufanya hivyo”
“Sawa, tutaongeza ulinzi, ila ningependa kufahamu ni hatari gani ambayo ulikutana nayo”
 
“Nakuomba twende kwenye chumba cha kuongozea kamera”
Meneja huyu akatafakari kwa sekunde kasha akisha akakubali. Tukatoka ofisini hapa huku mwanasheri na Camila wakionekana kujawa na shahuku ya kuhitaji kufahamu ni kitu gani ambacho kinaendelea kwangu. Tukaingia katika chumba hichi kikubwa ambacho kina tv nyingi sana ambapo kila tv inaonyesha video ya kamera inayo rekodi eneo hilo.
“Karibuni, hichi ndio chumba chetu cha kuongozea kamera zote”
Meneja huyu wa hoteli alizungumza.
“Nashukuru. Nakuomba uweze kuonyesha video iliyo rekodiwa katika eneo lile ambalo lipo pembezoni mwa swimming pool”
 
“Turudishe majira ya saa ngapi?”
“Saa moja na nusu hivi asubuhi leo”
Kijana huyu ambaye tumemkuta ndani ya chumba hichi, akafanya kazi niliyo muagiza. Video ya mimi na mzee huyu wa kichina ikaanza kuonekana.
“Hembu hiamihshie kwenye tv kubwa”
Meneja alizungumza na video hii ikaanza kuonekana kwenye tv kubwa kupita zote iliyopo katika chumba hichi. Nikaonekana jinsi ninavyo fungua bahasha na kutoa picha hizo.
 
“Hembu zoom kwenye hizo picha”   
Nilimuambia kijana huyu na akafanya hivyo na picha hizo zikaonekana vizuri sana. Watu wote wakaonekana kustuka sana kwani hizo picha zinaonyesha mwanamke huyo akiwa ametekwa.
“Nahitaji hizo picha na pia sura ya huyo mzee”
“Sawa Ethan”
“Baby kwani alikuambia yeye ni nani?”
“Hakuniambia yeye ni nani aliniwekea hizo picha……”
Mwanasheria akanitazama kwa macho yanago nikataza nisizungumze kitu cha aina yoyote kwa maana kuna watu hapaswi kufahamu nilicho kizungumza.
 
“Je munaweza kumsaka mzee huyo taarifa zake”
Camila alizungumza huku akimtazama kijana huyu.
“Ndio inawezekana”
“Basi ninaomba muweze kunisaidia katika hilo”
Kijana huyu akaanza kazi hiyo ambayo haikuchukua muda mrefu sana akafanikiwa kupata taarifa muhimu za mzee huyu. Taarifa zinaonyesha kwamba mzee huyu uraia wake ni nchini China, na inaonyesha kwamba ametokea nchini Nigeria na kufika hapa Ujerumani, wiki moja iliyo pita. Taarifa zikaonyesha kwamba alingia nchini kama mfanya bishara kutoka katika shirika moja la simu lililopo nchini Nigeria.
“Makazi yake yapo nchini Nigeria?”
 
Kijana huyu alizungumza.
“Inabidi tuwataarifu askari”   
“Hapana, tusiwaafahamishe askari kwa sasa. Tunahitaji kuzungumza na Ethan mara moja ndio tuamue”
“Musimpeleke polisi, naomba hizo taarifa zake, umtumie Camila hapa kwenye simu yake pamoja na hiyo picha.”
“Huoni kwamba anaweza kukudhuru?”
“Tutajua nini cha kufanya, kesho atakuja aliniahidi hivyo. Hakikiseni kwamba kesho akija tu basi macho yenu yanakuwa makini kuhakikisha kwamba muna mpata”
“Sawa”
 
“Hili swala ni sisi watu watano munalifahamu, nawaomba wewe na kijana wako musiweze kutoa siri yoyote?”
“Hatuwezi kuvujisha sira muhimu kama hizi na kesho asipo kuja basi muna haki ya wewe kututulia mashaka juu ya hili”
“Ninashukuru sana”
“Karibu sana Ethan”
Tukatoka chumbani humu na moja kwa moja tukaeleka katika chumba changu na Camila, ambacho tutakitumia hapa hadi pale mashindano yatakapo kwisha.
“Wamekutumi hizo taarifa na picha?”
“Ndio mume wangu”
Nikaichukua simu ya Camila na kumtazama mzee huyu, nikarudi kumtazama mama huyu anaye onekana kwenye picha kisha nikampatia mwana sheria.
“Alikuwa anakuambiaje?”
“Aliniambia kwamba huyo ni mama yangu na wamemteka.Hivyo ameniagiza kwamba nichague kati ya boksi jeusi au uhai wa mama yangu”
“Mmmmm”
 
Camila aliguna aliguna huku akinitazama usoni mwangu.
“Ndio maana yake”
“Hivi hilo bosky jeusi Ethan ndio nini?”
Camila aliniuliza kwa shahuku kubwa na kumfanya mwanasheria kunitazama machoni mwangu kwa macho ya kunikataza nisizungumze chochote.
“Hata mimi sifahamu”
“Ethan hili swala nitalishuhulikia, hadi inafika usiku kila kitu kitakuwa kimekamilia, nipe mchana huu”
“Sawa”
“Utatumia simu hii, nikifika mjini nitakupigia niweze kukufahamisha ni kitu gani ambacho kinaendelea”
“Sawa, ila hakikisha kwamba huyu mzee munamkamata, nina hitaji kuonana naye kabla ya yeye hajanifwata kesho”
“Sawa mkuu”
Mwanasheria akaniaga na akaondoka, kabla hata sekunde stini hazijaisha, meseji ikaingia kwenye simu hii aina ya iphone seven. Nikaifungua meseji hii na kukuta imetoka kwa mwanasheri.
 
‘USIMUAMINI CAMILA KWA KILA JAMBO’
Baada ya kuisoma meseji hii nikaifuta na kumtazama Camila kwa tabasamu kubwa sana, kwa maana hapo awali alisha nisaliti na isitoshe alisha nichoma kisu kwa madai anahitaji kufanya mwenyewe.
“Tutafanyaje Ethan?”
“Usijali kila jambo litakwenda vizuri”
“Au nimuambie baba atusaidie katika kumtafuta?”
“Hapana usimbebeshe mzee mizigo mingi sana. Tunaweza kulifanya kazi hii sisi kama sisi”
 
Taratibu Camila akanikumbatia kwa hisia kali sana.
“Ninakupenda sana mume wangu”
“Ninakupenda pia mke wangu”
Mlango ukagongwa, tukaachina na Camila na nikaufungua, nikamkuta Frenando ndio anaye bisha hodi.
“Vipi Ethan una umwa?”
“Hapana ndugu yangu, karibu ndani?”
“Shem yupo?”
“Ndio”
“Basi siingii. Shem”
Frenando aliita kwa sauti ya juu kidogo.
“Beee”
 
“Naomba nimuibe mumeo kidogo”
“Usijali wewe muibe ila umrudishe akiwa salama kama ulivyo mchukua”
“Usijali shemeji yangu”
Nikarudi chumbani na kumnyonya Camila lipsi zake kidogo, ikiwa ni ishara ya kumuaga.
“Uwe makini mpenzi wangu”
“Usijali, ninakuja”
“Poa”
Nikatoka chumbani humu.  Nikaongonzana na Frenando hadi kwneye moja ya bustani ya kupumzikia, kwa maana huyu ni rafiki yangu na ni mtu ambaye ana fahamu siri zangu nyingi, nikaona sio mbaya nikamshirikisha matatizo yangu. Hadi ninamaliza kumuadisia, macho yakwa yamemtoka sana.
 
“Kaka kwa matatizo yako una haja ya kupata muda wa kupumzika, uwanjani si unafahamu kwamba mtu hutakiwi kuwa na mambo mengi kichwani”
“Usijali nitacheza, ila tambua watu ninao waamini kwa sasa ni wachache sana.”
“Pole sana ndugu yangu, ila kama alivyo kuambia mwana sheria wako, usimuamini Camila kama alikufanya yale yote na bado akaamua kurudi basi kuwa makini”
“Kweli, hapa ni mwendo wa kuchezeana akili, akileta ujinga sasa hivi nakuapia haki ya Mungu, nitahakikisha kwamba ninamuua kwa mikono yangu mimi mwenyewe.”

==>>itaendelea kesho


from MPEKUZI

Comments