Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 31

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA      

Tukatoka nje na kukutana na kundi la waandishi wa habari ambao wanamuhoji Camila na wazazi wake. Waandishi wa habari walipo niona mimi wakakimbilia wote kwangu na wakanizingira huku kila mmoja akihitaji kunihoji swali lake. Sikuwajibu kitu chochote hawa waandishi wa habari, nikatembea hadi walipo simama Camila na wazazi wake.
 
“Mume
nionyesha uhalisia halisi wa familia yenu nawashukuru sawa. Ila CAMILA kuanzia hivi sasa sahau kama kuna mwanaume ulisha wahi kumpenda anayeitwa Ethan. Na mzee ninatoa asilimia zangu za mchango nilizo kuchangia kwenye kampeni zako tusijuane kuanzia hivi sasa. Asanteni”
Mara baada ya kuzungumza maneno hayo huku mwanasheria wangu akiwa amesimama nyuma yangu tukaondoka eneo hili na kumuacha Camilia akiangua kilio kizito sana ambacho sikuhitaji kukijali kwani alicho kua anakitafuta kwangu tayari amesha kipata.
   
ENDELEA
Tukaingia ndani ya gari la mwana sheria na kuondoka katika eneo hili.
 
“Una simu ya ziada ambayo huitumii?”
“Ndio ninayo”
“Naomba uniazime kwa muda”
Mwanasheria wangu akanikabidhi simu yake. Nikaingia katika mtandao wa Twitter na kuandika neno kwamba ‘MIMI NA WEWE, IMEKWISHA’
Ndani ya dakika mbili, nikapata ujumbe wa maswali mengi sana, kwani watu wengi nimewaacha njia panda. Wapo walio hisi labda matatizo yatakuwa yamekwisha na wapo walio hisi kwamba mimi na Camila mahusiano yetu yamekwisha. Sikuhiyaji kujibu swali la mtu yoyote na nikaawacha hewani. Tukafika nyumbani, na kuwakuta dada Mery na mama wakiwa wamekaa sebleni. Kidogo bibi Jane Klopp macho yake hayaoni vizuri, ila ni mtu makini anaye ifahamu harufu yangu. 
 
“Ethan mwanangu”
Bibi Jane Klopp alizungumza huku akiitanua mikono yake, nikamfwata alipo kaa na nikamkumbatia kwa nguvu.
“Pole sana mwanangu”       
“Asante sana mama”
Dada Mery akanitazama kwa macho makali sana.
“Ethan naomba tuzungumze”
Dada Mery alizungumza huku akinyanyuka kwenye sofa alilo kalia. Tukaongozana hadi chumbani kwake.
“Ethan ni kitu gani ambacho kinaendelea.”
Dada Mery alizungumza huku akiwa amenikazia macho. Nikaka kimya huku nikijifikiria ni kitu gani ambacho ninaweza kumuambia dada Mery akakielewa.
 
“Sijakuelewa?”
“Ethan kuna mambo yametokea kwenye masaa kadhaa hapa nyuma, sijaelewa na sijui ilikuwaje hembu niambie”
“Kuna mambo yanayo endelea, ila nakuomba unipe muda kila jambo likikaa vizuri basi nitakujulisha”
“Ethan nahitaji kujua sasa hivi”
Akatokea Ethan ndini ya chumba hichi na kumfanya dada Mery kupiga kelele, ila nikawahi kumziba mdomo wake ili kelele zake zisimstue mama aliye kaa sebleni. Dada Mery macho yakamtoka kwa maana katika maisha yake hakuwahi kuona mtu akijitokeza gafla mbele yake.
“Nakuomba utulie dada”
“Halooo Mery”
Ethan alizungumza huku akikaa kwenye moja ya kiti humu ndani huku akiwa amevalia suti ya dhahabu.
 
“Wewe ni nani?”
Dada Mery alizungumza huku akiutoa mkono wangu mdomoni mwake.
“Ni wajina wa mdogo wako”
“Wajina ndio nini?”
“Ninaitwa Ethan, nimekuwa na urafiki na mdogo wako toka kipindi alipo kuwa mtoto mdogo na nimekuwa ni msaada mkubwa sana kwake”
“Shindwa na ulegee kwa jina la Yesu?”
“Kumbuka hata mimi nina mfahamu Yesu na tumepewa mamlaka ya hapa Duniani. Siwezi kushindwa pale ninapo kuwa na nia nje kwako”
 
Ethan alizungumza kiustarabu huku akiwa amejawa na tabasamu pana. Muonekano wa Ethan wa leo kidogo ni wa tofauti. Umri wake unaendana na dada Mery tofauti ni siku nyingine anavyo nijia katika makamu yangu. Amependeza sana kwa muonekano wake ambao hakika una mvutia dada Mery.
“Dada zungumza naye mimi ninakuja”
Dada Mery akataka kunifwata ila Ethan akamnyooshea mkono na kumtuliza na kumfanya ashindwe kwenda popote, taratibu dada Mery akamfwata Ethan sehemy alipo kaa na wakaendelea kuzungumza. Nikafika sebleni na kumkuta mwanasheria wa kampuni akizungumza na mama.
“Ethan kuna habari njema”
“Habari gani?”
“Wanafunzi wameokolewa ma majeshi ya Marekani, Ufarana an Uingereza”
Mwanasheria alizungumza huku akinionyesha picha za matukio hayo kwenye simu yake.
“Hawa walio pigishwa magoti ndio watekaji?”
Nilizungumza huku nikimtazama mpiganaji mmoja baada ya mwengine wa kundi hili la Al-Shabab.
 
“Ndio”
“Mmmm ni wengi aisee”
“Yaa ni wengi, sana. Watoto wa kike wanapandishwa kwenye helicopter ya jeshi. Watapelekwa Afrika kusini. Wanafanyiwa uchunguzi wa kiafya kisha wataletwa huku Ujerumani”
“Mungu ni mwemama kwa kweli. Je hawa wapiganaji nao wanapelekwa wapi?”
“Hayo ni mambo ya kijeshi, sijaweza kufahamu kwa kweli.”
“Ethan”
“Naam mama”
“Naomba tuzungumze”
Taratibu nikakaa pembeni ya mama. Nikamuomba kwa ishara mwanasheria atupishe na atangulie katika ofisi katia jengo moja nje ya jumba hili.
“Ndio mama”
 
“Umesha wahi kuzungumza na dada yako, kuhusianana swala lake la kuolewa?”
“Hapana mama, sijawahi kuzungumza naye”
“Hembu basi jaribu kuzungumza naye. Unajua umri wa dada yako unakwenda sasa. Hajapata mtoto wala hajawahi niletea mwanaume wa kunitambulisha au anataka nife ndio azae”
“Nitazungumza naye mama yangu, wala usijali”
“Hembu ongea naye bwana, nahitaji kufa nikiwa nimemshika mjukuu wangu. Au kama yeye ana chelewa muwahi basi. Umpatie Camila ujauzito”
Kauli hii ikanifanya nikae kimya kwa muda kdigo. Nikatazama katika mlango wa kuingilia humu ndani, nikamuona Camila akiwa amesimama kwa unyonge sana huku mikononi mwake akiwa ameshika kipocho kidogo.
 
“Huyo ni Camila?”
Bibi Jane Klopp aliniuliza huku akinitazama. Nikamkazia macho kamila, kwa maana mimi na yeye tayari mahusiano yetu yalisha kwisha.
“Ndio mama”
“Ohoo karibu mkwe wangu”
Camila akaanza kutembea kwa unyonge hadi alipo mama, akamkumbatia na kuanza kuangua kulia jambo lililo nifanya nizidi kukasirika.
“Unalia nini mwanangu”
“Mama ni Ethan”
Camila aliendelea huku akiendelea kumkumbatia bibi Jane Klopp. Nikatamani kuwaachanisha, ila nikashindwa kufanya hivyo, kwani sihitaji bibi Jane Klopp afahamu kwamba mimi na Camila tuna tofauti kati yetu.
 
“Amefanyaje Ethan?”
“Camila njoo tuzungumze”
“Ethan mbona sauti yako imebadilika, umegombana na mwenzako?”
Bibi Jane Klopp alizungumza kwa upole huku wakiachiana na Camila.
“Hapana mama ni mambo ya kawaida?”
“Mbona mwenzio analia, sijamzoea kumuona Camila akiwa hivi na amekuwa mnyonge sana. Eti Camila niambie ni kitu gani kimetokea”
Camila akanitazama kw amacho ya woga huku akijawa na wasiwasi mwingi sana. Macho yangu ninayo mtazama nayo, dhairi yanaonyesha kwamba nimekasiria na ninamzuia kwa ishara ya macho kuto kumuambia bibi Jane Klopp kitu cha aina yoyoye.
 
“Ethan……”
Camila akaka kimya mara baada ya kukiweka kidole changu kimoja mdomoni na kumuashiria kwamba akae kimya.
“Amefanya nini?”
“Mama nilimuambia Camila kwamba nina acha kucheza mpira maisha mwangu na ninataka kusimamia biashara za baba, ndio maana kitu hicho kimemuumiza”
Ilibibi niongopee ili mradi kuficha tofauti zetu mimi na Camila, kwani bibi Jane endapo atafahamu juu matatizo yanayo endelea hivi sasa, nina imani kwamba ndio utakuwa mwanzo wake wa kufa kwa presha.
 
“Kwa nini Ethan, ikiwa marehemu baba yako alikuwa ni mchezaji mzuri. Hembu fwata nyayo zeka bwana usiwe hivyo. Uje ni wengi utawaumiza, si yeye tu hata wale mashabiki wako Ethan”
“Kweli mama, nilsha muambia hilo, na timu yake imekataa kuingia uwanjani kwa mechi zilizo baki kwa ajili yake, wanahitaji arudi uwanjani”
Camila naye aliendeleza uongo wangu, ili mradi kumfunga akili bibi Jane Klopp.
“Ohoo Ethan sio vizuri bwana, kumbuka hizi kampuni zina wasimamiaji. Hembu sikiliza kilio cha mpenzi wako, na fanya maamuzi ya kuto kumuumiza Camila. Tambua kwamba Camila anakupenda na kukuhiji ndio maana ana umi sana kwa maamuzi yako sawa mwanangu”
Bibi Jane alizungumza kwa suati ya upole na iliyo jaa hekima ndani yake.
 
“Sawa mama”
“Unajua siku ambayo baba yako alikuwa ana stafu kucheza mpira. Tulilia sana, nilisha zoea kukaa uwanjani na kumshangilia, nilijisikia furaha zaidi pale alipo kuwa akifunga goli. Hivyo natambua maumivu ya kama mke wa mchezaji mpira. Ethan mwanangu, ninakupenda sana tena sana. Hembu jaribu kufurahisha moyo wa mpenzi wako sawa mwanangu”
“Sawa mama nimekuelewa sana na ninakuahidi nitahakikisha kwamba nina rudi uwanjani”
“Kweli mume wangu?”
Camila alijaribu kuzungumza huku akiwa na furaha ya uongo.
“Ndio mke wangu”
Nilizungumza neno hilo huku moyo wangu ukiwa umejawa na hasira na maumivu makali sana.
 
“Haya nyanyukeni mukatafute mtoto”
Bibi Jane Klopp alizungumza maneno yaliyo mshangaza sana Camila, ila sikuhitaji kumuonyesha Camila sura ya furaha. Tukiwa kwenye kordo ya kueleka chumbani kwangu, kwenye mlango wa dada Mery nikasikia miguno ya kimahaba, nikajikuta nikitabasamu tu, kwani Ethan naye anafanya mambo yake. Nikaingia chumbani kwangu na Camila akaingia na kufunga mlango kwa ndani. 
 
Camila akapiga hatua moja mbele kisha akapiga magoti chini huku machozi mengi yakiwa yanamwagika usoni mwake.
“Nimevumilia japo kukaa kwa nusu saa peke yangu na kujiaminisha kwamba sina mwanaume ninaye mpenda kwneye maisha yangu, ila nimeshindwa Ethan”
Camila alizungumza huku nikiwa nimekaa kitandani na kumtazama usoni mwake.
 
“Ni bora ningekuwa nimewahi kuwa na mwanaume mwengine zaidi yako, ningesama basi acha niende kwake nitulize moyo wangu. Ila Ethan sina, Ethan ninakupenda sana mume wangu, nakuhitaji sana mpenzi wangu. Nilihisi njia niliyo itumia itakuwa ni rahisi kwangu kujua ni wapi lilipo boksi jeusi, ila kumbe ndio ninakupoteza Ethan. Ninakupenda sana”
“Ndiovyo jisni baba yako alivyo kutuma ili nisitoe asilimia thelathini ya pesa zangu nilizo wekeza kwenye kampeni zake si ndio?”
Nilizungumza kwa sauti nzito iliyo jaa mikwaruzo kadhaa inayo dhihirisha kwamba nina hasira.
 
“Ethan, sipo hapa kwa ajili ya baba yangu. Nipo hapa kwa ajili ya upendo wangu kwako. Kumbuka nilisha weka ahadi kwenye maisha yangu. Nikikukosa wewe ni lazima nitajiua. Kumbuka siku nilipo hitaji kujitupa gorofani kwa ajili ya penzi lako”
“Ungejitupa tu. Sasa hivi tungekuwa tumesha kusahau wewe”
Nilimjibu Camila kwa dharua iliyo changanyikana na hasira. Camila akanitazama kwa macho yaliyo jaa huruma huku akionekana ni mtu anaye jutia kwa maamuzi yake.
 
“Ulinishika bastoka kama jambazi. Ulinidhalilisha na walinzi wako. Walinipiga wakanifunga pingu pasipo huruma ya aina yoyote. Nilikupa kipimo kidogo kama mwanamke kwenye maisha, nikihitaji kufahamu je nina mwanamke sahihi kwenye maisha yangu kumbe hapana. Umenionyesha moyo wa kishetani ambao hata mtu wa kawaida anashangaa kwa kweli, kwani nini lakini eheee?”
Nilizungumza huku machozi ya hasira yakinimwagika usoni mwangu. 
 
“Mangapi ambayo tulifanya siri Camila, mangapi ambayo  tulipanga kwenye maisha yetu. Okay kwa mfano sasa mimi ni gaidi, na wewe mke wangu umeulizwa na polisi ni wapi nilipo, kwa hiyo ungewapa ushirikiano wa kunikamata si ndio?”
Camila akatingisha kichwa akimaanisha kwamba asinge wapa ushirikiano polisi.
“Acha unafki mtoto wa kike. Umenionyesha  dhairi kwamba wewe sio mwanamke wa kuoa. Umenibagua kirangi na kuniiita sokwe. Sawa mimi ni sokwe, nakuomba usinipende na usokwe wangu. Nitatafuta sokwe mwazangu, niishi naye na nitavumiliana naye kwenye shida na raha, tabu na majanga kama uliyo nifanyia leo. TOKA NYUMBANI KWETU”
 
Nilizungumza kwa kufoka sana hadi mishima ya damua ikavimba katika mikono yangu. Camila taratibu akasimama na akaanza kunifwata kwa hatua za taratibu, jambo lililo nifanya niamke kiatandani na kumfwata sehemu nilipo, ili nimrudishe mlangoni n aondoke zake. Kitendo cha kumshika mkono wake, akachomoa  kisu cha kukunjua ndani ya kipochi chake.  Akanichoma kisu cha tumboni mwangu, jambo lililo nifanya nihisi maumivu makali sana ambayo toka kuzaliwa kwangu sikuwahi kuyapata.
 
“Ni bora tufe wote kuliko kuendelea kukukosa wewe”
Camila mara baara ya kuzungumza maneno hayo, akakichomoa kisu hicho kwa nguvu tumboni mwangu kisha naye akajichoma tumboni mwake na akawa wa kwanza kuanguka chini huku nami nikianguka pembeni yake.

==>>ITAENDELEA KESHO


from MPEKUZI

Comments