Magunia 45 Ya Korosho Yakamatwa Pwani Yakisafirishwa

Na Mwamvua Mwinyi,pwani
Jeshi la polisi mkoani Pwani wanalishikilia lori dogo kwa tuhuma za kukutwa na korosho magunia 45 yenye uzito wa kilogramu 81 .
 
Korosho hizo zinadaiwa zilikuwa zikisafirishwa kwenda kwenye chama cha msingi cha ushirika kinyume na agizo la Rais Dk John Magufuli kutaka korosho zote kusafirishwa na magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
 
Kamanda wa polisi mkoani Pwani ,Wankyo Nyigesa alisema ,gari hilo linahisiwa kusafirisha korosho hizo kuwa hazijapatikana kihalali.
 
Alieleza, tukio hilo lilitokea novemba 16 mwaka huu ambapo askari kwa kushirikiana na Mrajisi Msaidizi mkoa wa Pwani Angela Nalimi.
 
“Gari hilo aina ya Canter lenye namba za usajili T 731DGG lilikuwa likizipeleka korosho hizo zikiwa kwenye magunia yenye nembo ya chama kikuu cha ushirika mkoa wa Pwani (CORECU) kwenda chama cha ushirika cha msingi cha Misugusugu wilayani Kibaha,” alisema Nyigesa.
 
Baada ya uchunguzi kukamilika watuhumiwa na gari lao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili ikiwa watabainika walikuwa wanunuzi wasio ruhusiwa na serikali.


from MPEKUZI

Comments