Jeshi la Polisi Pwani Lamsaka Mwanamke Aliyempiga Hadi Kumuua Mwanae

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Jeshi  la polisi mkoani Pwani ,linamtafuta mwanamke ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja kwa tuhuma za kumpiga hadi kumuua mtoto  wake Halima Ramadhani (5) kwa tuhuma za kuunguza pazia la chumbani.

Kamanda wa polisi mkoani humo Wankyo Nyigesa alithitisha kutokea kwa tukio hilo la kusikitisha huko Kikongo wilaya ya Kipolisi Mlandizi wilayani Kibaha

Alisema mama huyo ,  alimuua mwanaye kwa kipigo akimtuhumu mwanaye huyo kuunguza pazia hilo kwa kutumia kibatari.

"Baada ya kukuta pazia hilo limeungua mama yake alimshambulia na kupelekea kifo cha mtoto huyo na alipoona hali mbaya alikimbia," alisema Nyigesa.

Alisema,mtoto huyo alifariki alipofikishwa katika kituo cha Afya Mlandizi siku hiyo hiyo majira ya saa nne usiku.


from MPEKUZI

Comments