AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 150 na 151 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
 ILIPOISHIA   

“Hii kazi nitaifanya mimi mwenyewe, ninakuomba uniandalie usafiri ambao utanifikisha nchini Marekani kisiri pasipo mke wangu kujua wala serikali ya Marekani kufahamu.”
“Jene……”
“Meja fanya hivyo, hiyo ni amri na si ombi”
Nilizungumza kwa sauti nzito huku nikimtazama meja usoni mwake na kumfanya atingishe kichwa kukubaliana kwa kile nilicho kizSungumza kwani hata akikataa hawezi kupinga maamuzi yangu kwani mimi ndio mkubwa wake wa kazi japo kiumri yeye ndio mkubwa.
       
ENDELEA   
Taratibu nikaanza kuondoka kuelekea ofisini kwangu huku kichwani mwangu mawazo mengi sana. Dalili ya maisha yangu kufikia ukingoni ninaianza kuiona mbele yangu. Kwa sasa kusema kweli sinto hitaji mwanamke yoyote kunipenda na kulia kwa ajili yangu kwani ninatambua mwisho wa mapenzi yetu ni kuingia matatizoni na anaweza kupoteza maisha kama ilivyo kuwa kwa mwanamke ninaye mpenda Cajol.
“Mkuu”
Sauti ya Martin ilinistua, taratibu nikageuka nyuma na kumtazama usoni mwake.
“Kama huto jali ninakuomba nifahamu ni kutu gani kinacho endelea kwa sasa”
Nikamtazama Martin usoni mwake, kiumri nahisi nitakuwa nimempita miaka michache sana. Nikatabasamu huku mkono mmoja nikimshika begani mwake.
“Martin kuwa kiongozi lazima ni mambo mengi yanatokea, kwa hiyo usijali mdogo wangu”
 
“Ila mkuu ulisema kwamba utaniamini, tafadhali ninakuomba uniambie kwa maana naona kuna siri kubwa inayo endelea kati yako na meja na huitaji ni hata mke wako ajue. Mkuu kumbuka nilikuambia kwamba nipo tayari kufa kwa ajili yako na nipo tayari kubeba siri zako na matazo yako vyovyote itakavyo kuwa nitahakikisha ninafanya hivyo. Tafadhali mkuu naomba uniambie”
Maneno ya Martin yakanifanya mwili wangu wote kunisisimka na kujikuta machozi yakinilenga lenga usoni mwangu. Nikatamani kuzungumza ila nikajikuta nikishindwa kabisa na nikaanza kutembea kuelekea ofisini kwanbu na kumfanya Martin kunifwata kwa nyuma, kabla sijafika kwenye mlango wa ofisini Martin akanishika bega langu la upande wa kulia na kujikuta nikisimama.
“Mkuu mimi ni msaidizi wako”   
“Nimekuelewa Martin nitakuambia badae sawa”
“Sawa mkuu”
Nikafungua mlango na kuingia ndani, nikamkuta Yemi akiwa hayupo. Ikanibidi kutoka tena ofisini kwangu.
“Vipi mkuu?”   
“Mke wangu hayupo?”
“Labda atakuwa amerudi ndani?”
 
Tukaanza kuongozana na Martin hadi kwenye nyumba ninayo ishi, nikaingia chumbani kwangu na kumuacha Martin sebleni. Sikumkuta Yemi zaidi ya nguo zake zikiwa kitandani, nikasikia maji yakimwagika bafuni, nikajikuta nikianza kutembea taratibu hadi bafuni, nikafungua mlango wa bafuni, cha kushangaza sikumkuta Yemi, zaidi ya maji ya bomba la mvua yanayo mwagika. Kwa haraka nikafunga bomba hili la maji na kutoka hadi sebleni.
“Mke wangu hayupo ndani”
Nilizungumza huku mapigo ya moyo yakinienda kasi kwani, nimesha anaza kupata hisia mbaya hukusiana na kutoweka kwa Yemi ambaye alisha niahidi kwamba hii vita ni lazima ataiingilia.
 
Waambie wanajeshi wote kwamba mke wangu hayupo wahakikishe wanamtafuta ndani ya hii kambi sawa”
“Sawa jenero”
Martin akatoka kwa kasi humu ndani na kuniacha sebleni nikiwa nimechanganyikiwa. Nikarudi chumbani tena, katika kutazama tazama juu ya meza nikaona karatasi nyeupe kwa haraka nikaichukua na kukuta maandishi yaliyo andikwa kwa kalamu ya wino mweusi.
‘Mume wangu Dany/Peter, natambua kwamba haya ni maamuzi magumu niliyo yachukua ila nimefanya hivi kwa sababu ninakupenda mume wangu. Sihitaji kuona damu yako inamwagika kwa ajili ya mtoto ambaye sio damu yako. Natambua kwamba unanipenda na unanijali ila nimejitolea maisha yangu kwa ajili ya jambo hilo. Ninakuomba sana unisamehe mume wangu. Kwaheri’
 
Nikajikuta nikifinyanga finyanga karatasi hii kwa nguvu huku nikilia kwa uchungu mkubwa sana. Nikajifuta machozi yangu usoni kisha nikaanza kutembea kuelekea nje huku hasiri niliyo nayo sijawahi kuipata tangu kuzaliwa kwangu.
“Mkuu”   
Niliisikia sauti ya meja akiniita huku akiingia kwenye mlango wa kuingilia hapa sebleni. Kwa macho niliyo mtazama nikamuona meja akikaa kimya kwa sekunde kadhaa. Sikuzungumza kitu chochote zaidi ya kumtazama usoni mwake.
 
“Nimesikia mke wako ametoweka?”       
Nikamkabidhi meja karatasi niliyo ifinyanga, akaifungua taratibu na kuanza kuisoma, nikamuona meja akishika kichwa chake huku akionekana kupatwa na mshangao mkubwa sana.
“Waambie wahakikishe kwamba wanamleta mke wangu hapa. Kwa garama ya aina yoyote ninamuhitaji mke wangu”
“Sawa mkuu nitahakikisha kwamba mke wako  hatoke ndani ya nchi hii ni lazima tumrudishe hapa”
Martin akaingia na kutufanya mimi na meja kumtazama.
“Mkuu nina habari mbaya”
“Habari gani?”
Martin akanikabidhi simu yake nikaanza kuiona video inayo muonyesha Yemi akijisalimisha mikononi mwa wanajeshi wa kimarekani, akishuka kwenye helicopter ambayo ina chata la jeshi langu.
 
“Aliiba helicopter moja na kuondoka nayo”
Nikajikuta nikipepesuka huku miguu ikiniishiwa na nguvu kabisa. Martin na meja wakaniwahi kunishika na kwa haraka wakanikalisha kwenye sofa. Macho yangu yakaanza kububujikwa na machozi huku nikiitazama video hii iliyo chukuliwa na simu, nikawaona wanajeshi Wakimarekani jinsi wanavyo mvisha pingu Yemi.
“Amejisalimisha kwenye kambi ndogo ya jeshi iliyopo hapa nchini Nigeria”
Martin alizungumza huku akinitazama usoni mwangu. Kwa ishara meja akamuomba Martin asizungumze chochote kwani akili yangu kwa sasa haipo vizuri. Nikairudia tena kuitazama video hii nikashusha pumzi nyingi huku nikijitahidi kuizuia hii hali ya kupoteza nguvu mwilini mwangu. Nikaka zaidi ya dakika kumi nikiitazama hii video. Taratibu nikasimama wima, nikamkabidhi Martin simu yake.
“Kambi ipo wapi?”
“Abuja”
“Niandalieni vikosi kabla hawajamsafirisha mke wangu kumpeleka Marekani”
“Ila mkuu unaweza kuwa ni mtego wa kuhitaji kukupata wewe kirahisi”
“Meja unataka kuniambia kwamba mke wangu ni msaliti si ndio?”
“Hapana jenero”
“Ila…”
“Nimekushauri tu mkuu, kwa maana lengo la Wamarekani wanakuitaji wewe”
“Wakinikamata basi ila ninahitaji muandae vijana, nipeleke kwenye ghala la silaha”
“Sawa mkuu”
 
Martin alizungumza na kuanza kunifwata kwa nyuma, meja naye akaanza kutufwata.
“Jenero nina imani kwamba ushauri wangu kwa muda mwengine unakwenda tofauti na maamuzi yako, ila ningekuomba hili tuweze kulifikiria mara mbili mbili. Ninaimi hii ni njia rahisi sana Wamarekanani wanaweza kuitumia kupata wewe ukitegemea kwamba wewe ndio mkuu wa hili kundi hili. Ukiondoka unahisi ni nani atakaye ongoza hili jeshi?”
“Wewe ndio utaongoza”
“Jenero umri wangu kwa sasa umekwenda, nimesha kuwa mzee sana, muda wowote ninaweza kuondoka duniani, jeshi linahitaji vijana ambao ndio nyinyi. Tafadhali ninakuomba niandae kikosi cha kwenda kumuokoa mke wako”
“Meja una mke?”
Nilimuuliza meja huku nikisimama na kumtazama usoni mwake kwa hasiria. Taratibu meja akajibu kwa kutingisha kichwa chake.
“Unajua uchungu wa mke?”
“Hapana mkuu”
 
“Kaa kimya katika hili, hili ni tataizo la kifamilia na si tatizo la jeshi lako ninacho kiangalia hapa ni mke wangu kuwa salama sawa meja?”
“Nimekuelewa mkuu samahani kwa ushauri wangu kwako”
“Ninakuomba uniandalie wanajeshi wanne, ninakwenda kuivamia hiyo kambi ya Wamarekani”
“Wanajehshi wanne?”
“Ndio”
Meja akatazamana na Martin, kisha meja akaondoka eneo hili. Nikaanza kutembea kuelea kwenye ghala la kuhifadhia silaha pamoja na nguo za kijeshi. Tukaingia kwenye ghala hili ambalo linalindwa sana na wanajeshi kwani hapa ndipo kwenye silaha zote za kundi hili. Wanajeshi wote wakanipigia saluti huku wakisimama kikamavu.
“Nahitaji nguo zitakazo nitosha mimi”
“Zipo  meja”
Nilimuambia mmoja wa watunzaji wa nguo katika ghala hili. Nikaingia katika ukumbi wa kuhifadhia silaha, nikaanza kuchukua bastola mbazo ninaimani zitanisaidia katika kupambana kwangu. Martin naye nikamuona yupo katika harakati ya kuchukua silaha zinazo mfaa yeye.
 
“Unafanya nini Martin?”
“Mkuu ninahitaji kwenda na wewe”
“Martin hii vita itakuingiza kwenye matatizo”
“Mkuu najua upo juu yangu ila hili sio ombi kwako. Ninaifanya kazi ambayo umenikabidhi nitahakikisha kwamba ninakwenda na wewe sehemu yoyote utakapo kuwa, iwe kwenye shida ama raha ni lazima niwe na wewe jenero”
Nikamtazama Martin usoni mwake, sikuhitaki kumzuia, tukaendelea kuandaa silaha zetu. Nikamuona Martin mara kwa mara akiwa ameweka mkono wake wa kushoto kwenye sikio lake la upande wa kushoto.
“Una kinasa sauti cha nini?”
Swali langu likamfanya Martin kustuka na kubaki akinitizama kwa maana nina ujuzi sana na mtu aliye vaa kinasa sauti sikioni kwani walinzi wote mara nyingi huvaa vinasa sauti kwenye masikio yao ili kuhakikisha kwamba wanapena taarifa zozote zinazo endelea katika eneo ambalo wapo.
“Mkuu nilimuweka meja kinasa sauti kwenye mfuko wa koti lake la jeshi ili kila mazungumzo yenu munayo yazungumza nipate kuyasikia kwani nilihitaji kufahamu ni kitu gani kinacho endelea”
 
“Kwa hiyo una tupeleleza?”
“Hapana mkuu, nimefanya hivi kwa ajili ya usalama wako, kumbuka mimi kwa sasa ndio mtu wako wa karibu pasipo kufanya hivi nitakuwa nipo nyuma ya muda na maamuzi ya kuhakikisha kwamab mkuu wangu unakuwa salama”
Nikamtazama Martin usoni mwake, nikamuona Martin akiongeza usikivu katika kusikiliza.
“Nini?”
“Mkuu unatakiwa kusikia hichi”
Martin akavua kinasa sauti chake na kunikabidhi mimi, nikakivaa katika sikio la upande wa kulia.
‘Hakikisheni kwamba jenero haendi popote, ikiwezekana hata kwa kumchezea rafu ya kumchoma sindano ya usingizi. Sawa?’
Niliisikia sauti ya meja ninaimani anazungumza na wanajeshi ambao nimempa kazi ya kuniandalia
‘Sawa mkuu ila hili ni hatari sana na endapo jenero akijua ninaimani kama alivyo sema atatuua kwa mana sisi tutakuwa ni wasaliti wa amri yake.’
 
‘Kwani kuna mmoja wenu ambaye anaweza kuitoa hii siri?’
‘Hakuna meja, sisi ni vijana wako’   
‘Sawa fanyeni hivyo, yote ninafanya kwa ajili ya kumlinda jenro sihitaji aondoke kwenda popote, kwani bado tunamuhitaji kwenye hili jeshi’
‘Sawa mkuu’
Nikavua kinasa sauti hichi huku nikiwa nimejawa na gadhabu kubwa sana kwani meja anajaribu kunizuia kwa kile ambacho nimekiamua na hafahamu ni ukweli gani ulipo katikati ya hili tatizo ambalo pasipo kuwa makini litayagarimu maisha ya watu wengi wasio na hatia ikiwa mimi mwenyewe ninaweza kulishuhulikia na kulimaliza hata kama ni kwa kupoteza maisha yangu ila litakuwa limeisha nahalito endelea kwenye uso wa dunia.

AISIIIII……….U KILL ME 151



“Tutakwenda peke yetu”
Nilizungumza huku  nikimtazama Martin usoni mwake.
“Mkuu sa…..”       
“Hawa ambao meja ananiletea ni wasaliti katika hili swala na hakuna hata mmoja anaye tambua ni kity gani kinacho endekea kati tangu na Marekani. Sinto hitaji msaadawa wa mtu mwengine zaidi yako sawa?”
 
“Sawa mkuu”
Tukamaliza kujiandaa, meja akaingia huku akiwa ameongozana na watu nilio muomba aweze kunichagulia na kuniletea.
“Mkuu vijana hawa hapa wamekamilika kila idara unaweza kwenda nao”
Nikamtazama meja kisha nikawatazama vijana hawa kwa macho makali hadi wakajistukia na kuanza kutazamana. Nikachukua bastola moja iliyopo juu ya meza, nikaikoki vizuri na kmnyooshea mmoja wa kijana huku macho yangu nikiendelea kumkazia.
“Unaweza kufanya alicho kuambia meja wako?”
Kijana huyu akaanza kutetemeka mwili wake wote. Nikaielekezea kwa kijana mwengine huku naye nikiwa nimemkazia macho.
“Unaweza kufanya alicho kuagiza meja kukifanya?”
Kijana huyu naye hakunijibu kitu chochote zaidi ya kukaa kimya huku akinitazama.
“Meja, hili ulio lifanya leo siku nyingine ukirudi nitakuchukulia hatua za kisheria kali, Tumeelewana?”
“Mkuu sijakuelewa unamaanisha nini?”
Nikamsogelea meja nikaingiza mkono kwenye mfuko wa kulia wa koti lake sikukuta kitu chochote, nikaingiza kakatika mfuko wa upande kushoto, nikatoa kifaa kidogo ambacho ni kinasa sauti, nikamkabidhi mkononi mwakae na kumfanya meja kushangaa sana.
“Meja kumbuka maisha yangu na uongozi wagu ninatumia akili, unapo fanya vitu na wewe tumia akili sana kwa maana siku nyinine utafeli sawa. Hawa vijana wako siwahitaji kwenye opareheni hii, nitakwenda na Martin sisi wawili na tutajua ni nini cha kufanya”
 
“Samahani sana jenero kusudio langu halikuwa baya sana kwenye hili swala”
“Natambua ila unatakiwa kusirikiza amri ya mkuu wako na si kupinga amri yake hata kama kuna faida nzuri itapatikana kwa kuzuia amri yake”
“Sawa jenero”
Tukabeba kila tulicho kusudia kukibeba na Matrin, tukaelekea katika uwanja wa helicopter.
“Tunahitaji rubani?”   
“Hakuna haja mkuu, ninajua kuendesha helicopter”
Martin alizungumza huku akifungua mlango wa helicopter moja, tukaingia ndani, sikuhitaki kubisha. Taratibua Martin akaanza kuwasha helicopter hii ambayo haikuchukua muda mrefu sana ikashika kasi katika banka lake. Martin taratibu akaanza kuinyanyua helicopter hii kwenda juu.
“Mkuu vaa hizo earphone”
Martin alizungumza huku akinionyesha earphone kubwa zilizopo pembeni yangu, nikazichukua na kuzivaa masikioni mwangu, huku na yeye akivaa earphone zinazo fanana na hizi.
“Hapa tunaweza kuwasiliana na watu walipo  kambini?”
“Sawa sawa”
“Mkuu inabidi kuomba muongozo wa watu walipo chumba cha mawasiliano ili iwe rahisi kwa sisi kuweza kuivamia kambi hiyo”
“Unafahamu ilipo kambi?”
“Ndio ninaifahamu ila itakuwani kambi ambayo ina ulinzi mkali sana ambao unaweza kutukamata mapema sana”
“Wasiliana na watu wa chumba cha mawasiliano”
“Sawa”
“Mia moja kumi na moja, Erick ninazungumza hapa”
“Ndio tunakupata Erick?”
“Nipo na jenero Peter tunaomba msaada wa kuweza kuingia katika kambi ya Wamarekani”
“Nimesha weza kuhaki mfumo mzima wa ulinzi wa kamera katika kambi hiyo na kila kitu kinacho endelea kwenye hiyo kambi tunakiona”
 
“Vipi mke wangu yupo?”
“Ndio mkuu mke wako bado yupo kwenye hiyo kambi”
“Naomba muhakikishe kwamba munanieleza kila kitu ambacho kinacho endelea katika kambi hiyo sisi tukiwa njiani”
“Sawa mkuu, yupo kwenye moja ya chumba, na tunaweza kutumia njia ya chini ya ardhi kuweza kufika katika chumba hicho”
“Hiyo njia ipo wapi?”
“Mita mia tisa kabla ya kufika kwenye kambi hiyo”
“Ila mita mia tisa ni nyingi sana na tukishuka kwenye helicopter hii si tutapoteza mawasiano nanyi”
“Ndio mkuu hiyo ndio nyia rahisi ya nyinyi kuingia katika kambi hiyo na kumkomboa mke wako”
Nikaka kimya huku nikitafakari kitu cha kufanya.
“Mkuu”   
“Tuelekezeni hiyo sehemu ipo wapi?”
“Ni kwenye moja ya mnara wa simu, pembeni yake kuna mfuniko wa chuma mukiingia humo munaweza kuingia na kwenda moja kwa moja hadi kwenye sehemu kilipo chumba hicho.
 
“Sawa nimekuelewa, meja yupo humo ndani?”
“Ndio jenero nipo?”
“Tofauti tuziweke pembeni, ninahitaji kikosi kitakacho kuja nyuma yangu, na ninahitaji kikosi cha anga ninahitaji kuiteketeza hiyo kambi nzima”
“Sawa mkuu nimekuelewa nitaanzaa vikosi viwili, kikosi cha anga na kikosi cha ardhini”
“Shukrani, Martin unafahamu sehemu ulipo huo mnara?”
“Ndio ninafahamu muheshimiwa”
“Sawa fanya hivyo”
Tukatumia dakika kama dakika kumi na tano kufika katika mnara wa simu tulio elekezwa, taratibu Martin akaitulisha hii helicopter hii. Akaizima, kisha tukashuka kwenye hii helicopter. Haikutuchukua muda kuupata mfuniko huu  wa chumba, taratibu tukashirikiana kuufungua kwa maana ni mzito sana.
 
Martin akatoa kitochi kidogo na kumulika ndani kwa maana kuna giza, tukaona ngazi za chuma zinazo elekea chini, Martin akawa wa kwanza kushuka kisha nikafwatia mimi kushuka, tukaanza kutembea kuelekea mbele kwa kutia mwanga mdogo wa hii tochi.
   Tukazidi kusonga mbele kila mmoja akiwa ameshika bastola yake mkononi, ikatuchukua zaidi ya nusu saa tukawa tumefika kwenye sehemu ambayo tumekuya ngazi za kuelekea juu. Taratibu Martin akaanza kutembea kupandisha ngazi hizo hadi tukafanikiwa kufika juu ambapo napo kuna mfuniko.
“Vipi?”
“Ni mzito kama ule wa kule”
“Duu sasa tunaweza kuufungua?”
“Huu ubara wake ni kwamba umefungwa kwa nati na ili kuufungua ni lazima mtu uwe kwa juu”
“Mmmm kwa hiyo kazi yote tuliyo ifanya ni bure?”
“Hapana mkuu tunaweza kuvunja hili eneo kwa kutumia bomu la kutega”
“Ila si umeambiwa kwamba mke wangu yupo kwenye hicho chumba hapo juu”
 
“Ndio mkuu ila hatuna jinsi ya kufanya zaidi ya kufanya hivyo”
Martin akashuka kwenye ngazi na kusubiria jibu langu ili apande kuweka bomu ambalo litakwenda kuchangua eneo hili la mfuniko.
“Mkuu hiyo ndio njia ya pekee ambayo tumebakiwa nayo”
“Weka bomu”
Martin akafungua begi tulilo hifahidhia baadhi ya mabomu, akatoa bomu moja, akatega dakika tano, kisha akapanda kwa haraka na kulitega sehemu ambayo kuna mfuniko, akashuka na tukaanza kukimbia kurudi sehemu tulipo tokea kwani mlipuko wake unaweza ukawa ni mkubwa. Tulipo fika umbali ambao tukahisi kwamba mlipuko huo hautoweza kutuathiri, tukasimama. Mlipuko mzito ukatoke katike ene hilo na vipande vizito vizito vya matofali vikaangukia humu ndani. Tukaanza kurudi eneo hilo huku tukikimbia kwa kasi. Kwa haraka Martin akapanda kwenye kifusi hichi cha matofali yaliyo angukia humu ndani, akafanikiwa kufika kutoa juu. Na mimi kwa haraka nikapanda kwenye kifusi hichi na kutokea katika chumba ambacho tulitarajia kumkuta Yemi ila hatujampata kabisa.
 
“Hayumo humu?”
Nilizungumza huku nikisikilizia ving’ora vya tahadhari vinavyo endelea kulia katika eneo hili. Nikaufungua mlango wa chumba hichi na kuchungulia nje nikakuta wanajeshi wangi wakikimbia kwa kasi wakija katika hii kordo.
Kwa haraka nikaanza kuwashambulia kwa risasi, kwani hii ndio njia ya pekee ya sisi kuwazuia wanajeshi hawa. Tukaanza kupeana zamu na Martin katika kuwashambulia wanajeshi hawa.
“Naomba Granade”
Nilizungumza huku nikiwa nimejibaza, Martin akachomoa bomu la mkono ambalo ameninginiza kwenye mkanda wa kiunoni mwake. Akanikabidhi bomu hilo, nikachomoa kipini cha bomu hilo na kulirusha sehemu walipo jificha wanajeshi hawa, na kusabisha mlipuko mkubwa.
“Tutoke humu”
Nilizungumza huku nikianza kutoka kwenye hichi chumba na kuanza kusonga mbele kuhakikisha kwamba tunatafuta ni sehemu gani alipo Yemi. Mashambulizi ndani ya hili jengo yakazidi kupamba moto kwani kadri muda ulivyo zidi kwenda ndivyo jinsi tulivyo kutana na wanajeshi ambao wanazidi  kuongezeka kuhakikisha kwmba hatutoke ndani ya kambi yao.
“Mkuu”
“Ndio”
“Risasi zimeniishia”
Martin alizungumza huku akinitazama na kujikuta nikimtazama huku macho yakinitoka, nikajipapasa kwenye mfuko wangu na kukuta nina magazine moja tu. Nikachomoa magazine iliyopo kwenye bastola yangu nikakuta nayo ina risasi nne zilizo salia na mbaya wanajeshi wanzidi kumiminika na sehemu tuliyo jificha kusema kweli wakiamua kurusha bomu la mkono tunakufa.
“Hakikisheni tunawakamata wazima”
Nilisikia sauti ya mmoja wa wakuu wa hili jeshi, hapo ndipo nikafahamu kwamba kazi imezidi kuwa ngumu kwetu.
“Dany tunajua upo hapa, na umekuja kumuokoa mke wako. Jisalimishe mikononi mwetu la sivyo tunamuua mke wako”
“Dany!!?”
Martin aliniuliza kwa mshangao huku akinitazama usonim wangu.
“Ni jina langu usishangae”
“Ila mkuu huwezi kujisalimisha kirahisi namna hii?”
“Inabidi kufanya hivi, nikijisalimisha mchukue mke wangu na kuondoka naye sawa”
“Mkuu jukumu langu ni kukulinda hadi mwisho wa maisha yangu, tutakufa pamoja”
 
“Martin hili sio ombi ni amri sawa, ninajisalimisha mchukue mke wangu na uondoke naye hapa na lengo langu kubwa kuja hapa ni kujisalimisha kumalizana na hili jambo linalo jitokeza hapa”
“Mkuu hapana”
Martin alizungumza huku akiniomba magazine yangu ya risasi.
“Hatuwezi kutoka humu ndani Martin na sipendi ubishane na amri yangu”
“Kwa nini wanakutaka wewe?”
“Nilikuwa ni mpelelezi wa Kimarekanai, wamenisaliti na nikaamua kuwasaliti. Ila huu sio muda wa kupiga story ninakuomba mke wangu mchukue na kuondoka naye hili eneo”
Martin hakuwa na jambo la kujibu zaidi ya kukaa kimya.
“Ninahitaji kumsikia mke wangu kwanza”
Nilizungumza kwa sauti ya juu huku nikiendelea kujibanza kwenye hili eneo.
“Dany usitoke mume wangu”
Niliisikia saauti ya Yemi akizungumza huku akilia.
“Yemi”
“Ndio mume wangu kwa nini umenifwata jamani”
“Usijali mke wangu. Ninahitaji mumuachie mke wangu na ninajitokeza”
 
Nilizungumza huku nikimkabidhi Martin magazine iliyo salia, kisha taratibu nikanyanyuka kutoka katika eneo hili niliko jificha huku bastola yangu nikiwa nimeinyoosha kwa juu. Nikamuona Yemi akiwa amehishikiliwa na wanajeshi hawa wa Kimarekanani ambao idadi yao kwa haraka haraka inaweza kufika mia moja.
“Muachieni mke wangu, nipo tayari kujisalimisha mikononi mwenu”
Taratibu wakamuachi Yemi aliye anza kutembea kwa mwendo wa taratibu akija eneo hili nilipo, na mimi nikaanza kutembea kwa mwendo wa taratibu huku nikiwatazama wanajeshi hawa walio ninyooshea mitutu ya bunduki zao na endapo nitafanya kosa lilote wataniua mimi na Yemi jambo ambalo sihitaji litoke mbele ya macho yangu.
 
ITAENDELEA
“Haya sasa Dany ameamua kujitoa muhanga na kujisalimisha mikononi mwa maadui zake, je ni kitu gani kitatokea mbeleni, usikose sehemu inayo fwata ya story hii ya kusisimua”


from MPEKUZI

Comments