Vigogo Wawili wa ACACIA Wakamatwa na TAKUKURU

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imewakamata aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Acacia, Deo Mwanyika na Mshauri wa Serikali ndani ya kampuni hiyo, Alex Lugendo.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo alisema wanawashikilia watu hao tangu juzi, na kwamba leo wanaweza kufikisha mahakamani kufunguiwa mashtaka kwa tuhuma zinazowakabili.

“Mwanyika na Alex tuliwakamata kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi katika nyanja ya madini. Wakiwa viongozi waandamizi walishindwa kusimamia nchi ipate mapato kama ilivyotakiwa kwa mujibu wa sheria.

Deo Mwanyika alijiunga na Acacia mwaka 2001 akiwa ameitumikia kwa miaka 17, alitangazwa kujiuzulu Agosti 24 kwa barua ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Acacia, Peter Galeta kwenda kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo.


from MPEKUZI

Comments