Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 10

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588 
ILIPOISHIA           

“Bora na wewe umeona, wezako hapa wana shangaa. Sasa tuzungumzeni biashara, munamsajili au niondoke na kijana wangu akawe zao la timu nyingine”
“Weee tukikataa nahisi tutakuwa wendawazimu, mtu unaona kwamba tumeletewa Mess alafu tumkatae. Klopp mimi nipo tayari mkusajili”
“Kiwango cha chini ni paund milioni kumi kama munapesa tuingie mezani, ila kama hamuna kesho nina panda naye ndege ninaelekea naye Hispani na huko munafahamu kuna mapapa wakubwa R. Madrid na Bacelona”
“Klopp kumbuka wewe hapa una heshima, usitufanyie hivyo bwana?”
“Nina heshima, ila huku anakwenda kuvunja rekodi na heshima yangu, siwezi kumuachia bure kwa maana ni zao langu hili na si lenu”
Mzee Klopp aliendelea kushikilia msimamo wake wa kuhitaji kuniuza katika timu hii jambo ambalo ni jema sana kwenye maisha yangu ya mpira nikiwa bado ni kijana mdogo wa miaka saba.

ENDELEA   
Viongozi hawa wa hii timu ya Dotmund wakaa kimya huku wakitutazama mimi na mzee Klopp.
“Basi tutalizungumza mzee Klopp”
“Sawa, munamruhusu kijana wangu akaendelee na mazoezi yenu au tuondoke?”
 
“Muache tu aendelee na mazoezi hakuna tabu”
Kocha wa timu ya vijana alizungumza huku akiwa na tabasamu sana. Nikarudi uwanjani na nikaendelea kuonyesha uwezo wangu mara mbili hata na mara ya kwanza nilipo kuwa nikicheza kwa maana nimesikia kiwango cha pesa kilicho tajwa kwa ajili ya mimi kununuliwa. Hadi tunamaliza mazoezi tayari nimefunga goli nane peke yangu huku nikitoa mchango wa goli mbili. Kila mchezaji akatokea kunipenda huku wachezaji wengine wakubwa wakiomba kupiga nami picha. Hapa ndipo nilipoa anza kuigundua nguvu niliyo nayo kwa maana wachezaji vijana wao ndio huwaomba wachezaji wakubwa kupiga nao picha, ila kwangu imekuwa tofauti ya hivyo. Nikapiga picha na wachezaji karibia wote huku wengine wakinionyesha video za magoli ambayo nimeyafunga.
 
“Hei Ethan”
Mchezaji mmoja mkubwa aliniita na akasogea na mimi pembeni.
“Unajua nini juu ya hii Club?”
“Hii Club alicheza baba yangu mzee Klopp yule pale”
“Hilo ndio unalo lijua?”
“Ndio”
“Una kipaji kikubwa sana, tena sana mdogo wangu. Ninacho kushauri usikubali kusajiliwa katika timu hii, ligi yetu ya hapa Ujerumani bado haijapata nguvu kama ligi ya nchini Uingereza na Hispania. Mshauri baba yako akupeleke ukafanye tena majaribio kwenye timu kubwa kama Liverpool, Man City, Man United, Arsenal, Madrid au Bacelona. Nakuhakikishia baada ya miaka mitano mbeleni utakuwa bilionea sawa”
“Sawa kaka”
“Liweke hilo akilini na usimuambie mtu mwengine zaidi ya baba yako”
“Sawa”
 
Mchezaji huyu akanikunjia ngumi mkono wake wa kulia, nami nikakunja nguni na kuzigonganisha, kisha kaniruhusu kuelekea kwa baba yangu mzee Klopp.
“Ethan”
“Ndio baba”
“Una kipaji sana leo umenitoa kifua mbele kwenye hii club”
“Asante sana baba”
“Mazoezi mengi, kujituma na heshima hilo ndio jambo kubwa na la muhimu sana kwenye mpira wa miguu. Zingatia hayo pasipo kumuangalia mtu wala pasipo kupenda umaarufu. Si unaona watu wanakufwata wenyewe?”
“Ndio baba”
“Ukijitahidi katika hayo, kila jambo litakwenda kufanikiwa kwa upande wako sawa”
“Sawa baba”
“Sanamu ambayo nilikuwa ninaizungumzia muda ule ndio hii hapa”
Mzee Klopp akanionyesha sanamu moja kubwa sana inayo fanana na yeye, ila hii inamuonyesha enzi zake akiwa mchezaji.
 
“Aliye ichonga hii sanamu ni nani?”
“Ni mmoja anaitwa Karius, ila kwa sasa ni marehemu, yeye ndio aliitengeneza hii sanamu na kuiuza kwenye hii Club, ni heshima kubwa sana kwangu kuwekwa kama hivi. Naamini kwamba na wewe siku moja ukiwa mtu mwenye makamu kama yangu basi nawe utawekwa kama hivi”
“Nitahakikisha baba, sanamu langu linakuwa kubwaaaa kupiga hata hili la kwako”
“Hahaaa hilo ndio jambo ninalo hitaji kulisikia nahitaji uvunje rekodi ya mchezaji mmoja hapa duniani ambaye hadi sasa hivi haijawahi kuvunjwa”
“Mchezaji gani baba?”
 
“Anaitwa Edson Arantes do Nascimento”
“Heee ndio nani huyo!?”
Niliuliza huku nikiwa nimejawa na mshangao mkubwa sana.
“Jina lake maarufu anaitwa Pele. Ni mchezaji maarufu duniani kwa kipindi chote toka karne ya ishirini hadi sasa. Hakuna mchezaji ambaye aliweza kuivunja rekodi yake ya magoli”
“Kwani amefunga magoli mangapi?”
“Magoli elfu moja na sabini na nne”
“Mmmmm”
“Ndio kwa umri wako unaweza kuyafikia. Hakikisha kwamba una yafikia na kuyapita”
 
“Baba ila magoli elfu ni mengi sana”
“Nalitambua ila kila mechi ukiweka wastani wa kufunga magoli matatu. Ukicheza mechi mia tatu hamsini na nane utakuwa umeyafikisha hayo magoli.”
“Duu”
“Yaa unajua mpira ni kama familia. Jinsi unavyo panga idadi ya watoto wako unao wataka kuzaa na kuwalea ndivyo jinsi utakavyo panga jinsi ya kufunga. Hakikisha kwamba kila unapo ingia uwanjani unaweka nia na kunuwia kwamba ni magoli mangapi ambayo una yahitaji, kufunga kwa siku hiyo. Endapo una pata nafasi funga kama leo ulivyo funga magoli nane sawa”
 
“Sawa baba”
“Nakuambia mambo haya, sikuwahi kumuambia mchezaji wangu yoyote hata pale nilipo kuwa kocha. Fanyia kazi haya maneno yangu, utaona jinsi dunia itakavyo kuheshimu sawa”
“Sawa baba”
Mzee Klopp akaendelea kunitembeza katika maeneo tofauti tofauti ya uwanja huu mkubwa wa mpira. Baada ya kumaliza matembezi haya, akanipeleka kwenye mabafu nikaoga na kuvaa nguo zangu. Safari ya kurudi nyumbani ikaanza taratibu.
“Baba nina weza kukuuliza sawali?”
“Ndio unaweza kuwa huru”
“Hivi ni club gani ambayo kwa mtazamo wako unaweza ona nitafanikiwa kufikisha kiwango hicho cha magoli hapa duniani?”
Mzee Klopp akaka kimya kidogo huku akionekana kulifikiria swali nililo muuliza.
 
“Club kubwa?”
“Ndio baba”
“Kusema ukweli, ukicheza nje ya hapa Ujerumani, hilo linawezekana kwa maana ligi ya huku, moja ni ngumu sana, pili ina wendawazimu wengi sana ambao, wao hawato ona huruma kukuvunja wewe miguu na wao wakapewa kadi nyekundu zitakazo waweka nje ya uwanja kwa baadhi ya mechi tu kisha wao wakarudi, ila wewe utaendelea kuuguza majeraha”
Mzee Klopp alizungumza kwa upole sana na umakini wa hali ya juu.
“Ligi ya Uhispania, kule kwa sasa kuna wafalme wawili tu wanao onekana kuliko wachezaji wengine. Wao ni Ronaldo na Messi. Hadi ukiwa mkubwa wewe hawa watu watakuwa wamesha stafu kucheza, ila kwa ligi ya Hispani siipendi sana japo ina pesa nyingi”
 
“Je ligi ya Uingereza?”
“Uingereza ligi yake haieleweki, haina mbabe, timu inaweza kupanda daraja na ikachukua ubingwa. Niligi yenye ushindani mkubwa sana naamini kwa wewe itakufaa kama kweli utakuwa unaipenda sana ligi hiyo”
“Ninaweza kukuomba kitu?”
“Ndio niombe mwanangu”
“Unaonaje ukanipeleka Uingereza nikafanya mazoezi japo kwenye timu moja wapo kubwa ili uangalie wapi wataweka kiasi kikubwa waninunue?”
 
“Hilo ni wazo moja zuri sana. Hakika wewe una akili sana, sikukaa na kulifikiria hilo, moyo wangu na mapenzi yangu niliyaelekezea Dotmund. Ila kutokana kwa sasa mpira ni biashara na fursa ya kutengeneza historia yako binafsi nitakupelekea jijini Liverpool ukajiunge na majogoo hao wa London kwa kufana mazoezi, ukipita hakuna shaka kwa maana utakuwa upo katika timu salama”
“Sawa baba”
Tukafika nyumbani na kumkuta Merry na mama wakiwa na furaha sana ambayo kwa haraka haraka wanaonekana kuna jambo wameliona.
“Yaani Ethan kwenda tu huko leo, ona ulivyo zagaa kwenye mitando ya kijamii, tazama jinsi wachezaji wakubwa walivyo weka picha zako Instergram”
 
Mery alizungumza huku akionionyesha picha hizo kwenye simu yake.
“Tena honey kuna habari nyingine nzuri sana”
Bibi Jane Klopp alizungumza.
“Kuna simu mbili moja imetoka nchini Hispania, raisi wa Real Madrid anahitaji kuzungumza na wewe na simu nyingine imetoka Uingereza, tajiri wa Chelsea Roman Abramovich wote wanahitaji kuzungumza juu ya Ethan”
Mzee Klopp akanitazama huku akiwa ametabasamu kwa furaha sana.
“Tena wamesema ikiwezekana wakutumie hata private jet uende na Ethan katika hizo timu”
 
Nikamuona mzee Klopp akiwa kama amewehuka kwa furaha, mara azunguke huku mara achukue simu ya hapa sebleni mara airudishe.
“Wametumia simu ile ya nyumbani”
“Niletee”
Bibi Jane Klopp akaanza kutembea kuelekea ndani huku akiwa katika mwendo wa haraka haraka. Kusema kweli furaha imenijaa sana moyoni mwangu. Bibi Klopp alirudi hapa sebleni haraka haraka huku simu hiyo ikiwa inaita.
“Ni namba kutoka Uingereza”
“Uingereza?”
“Ndio mume wangu?”
Mzee Klopp akaichukua simu hiyo, akaipokea na kuiweka sikioni mwake.
“Ndio”
“Sawa”
“Tutakuja”
“Basi nitawapa maelezo yapi ya kufwata”
“Sawa sawa”
“Haya”
 
Mzee Klopp akakata simu na kuanza kushangilia seble nzima hadi sote tukaanza kumcheka.
“Ethan ndoto yako imekuwa kweli”
Mzee Klopp alizungumza huku akininyanyua na kunikumbatia.
“Unakwenda Liverpool”
“Kweli baba”
“Niamini, acha kwanza tukazungumze na timu ya Liverpool”
Mzee Klopp aliendela kuzungumza huku akiwa amenibeba.
“Muweka mwenzako chini usije ukamuangusha”
“Siwezi kumuangusha kabisa, sasa inabidi muanze kumuandalia nguo, leo nina panga utaratibu wa ndege yao wanayo ituma kisha kesho tunaanza safari kuelekea Uingereza sawa”
“Sawa baba”
Niliitikia nikiwa na furaha sana. Mery akaniita na kuninong’oneza.
“Usiondoke pasipo kumuambia chochote Camila”
“Ninaweza kuwasiliana naye kupitia simu yako?”
“Ndio”
 
Mery akanipatia simu yake na nikakimbilia chumbani kwangu. Nikampigia Camila kupitia simu ya mama yake, akapokea, nikamsalimia mama yake na kwa bahati nzuri hakuwa mbali na Camila.
“Ethan mbona leo una furaha sana?”
“Nimeitwa katika kikosi cha watoto cha timu ya Liverpool jijini London”
“Ethan acha utani?”
“Haki ya Mungu vile baba ametoka kupigiwa simu sasa hivi”
Camila hakunijibu kitu chochote zaidi ya kukaa kimya.
“Halooo”
“Ethan?”
 
“Ndio mpenzi wangu”
“Huto niacha kweli ukienda huko?”
Camila alizungumza kwa unyonge sana hadi furaha yangu ikaanza kunipotea.
“Mpenzi wangu, siwezi kufanya chochote kibaya juu ya penzi letu”
“Ethan najua ni jinsi gani ninavyo kupenda, ukienda huko ni lazima wahitaji ubaki huko huko, na mimi sitaki mpenzi wangu iwe hivyo”
“Nakuapia Camila kwa jina la Mungu, siwezi kukusaliti. Najua unapenda kuniona ninafanikisha ndoto zangu, nakuomba unipe nafasi yenye baraka niweze kufanikisha ndoto zangu mpenzi wangu sawa”
“Sawa Ethan, ukienda kesho munarudi lini?”
“Sijajua kwa maana ninakwenda kufanyiwa majaribio ya kwanza, nikiwanikiwa basi tutajua ni lini nitatakiwa kurudi tena Uingereza”
 
“Ila Ethan kuwa makini, sasa hivi utanipoteza kabisa duniani kwa maana nina kupenda sana”
“Siwezi kukupoteza wewe ni wangu tu”
“Kweli?”
“Ndio mpenzi wangu”
“Sawa tutazungumza usiku sasa hivi tunajiandaa na mama tunataka kwenda mjini kwenye maduka”
“Poa nina kupenda Camila”
“Ninakupenda Ethana wangu mwaaaa”
“Asante mpenzi wangu”
Camila akaka simu na kunifanya nijawe na furaha sana moyoni mwangu, ndoto za kuwa mchezaji mkubwa duniana zinaanza kutimia taratibu.
‘Ethan”
 
Niliisikia sauti ya Ethan mwenzangu, ikiniita nyuma yangu ambaye uhalisia wake ni jini.
“Shitii umenistua sana”
‘Nisikilize sina muda mwingi sana. Kesho usiende hiyo safari kwa maana mukifika nchini Uingereza mmoja wenu kati ya baba yako au wewe atapigwa risasi na kufa hivyo musiendeee”
Maneno ya Ethan yakanistua sana moyo wangu, hakuhitaji hata nimuulize swali, akapotea mbele ya upeo wa macho yangu na kunifanya niwe katika wakati mgumu sana ulio iyeyusha furaya yangu mithili ya barafu katika jua kali.

==>>ITAENDELEA KESHO


from MPEKUZI

Comments