Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 09

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588 
ILIPOISHIA   

“Tunaweza kurudisha?”
Niliwahimiza wachazaji wezangu huku nikipotea kitambaa cha kuongoza timu kutoka kwa golikipa. Mpira ukaanza kwa kasi ya ajabu huku wachezaji wezangu wakijitahidi kwa hali mali kuhakikisha kwamba tunakomboa hili goli moja lililo sali, nikafanikiwa kupata mpira huku mbele yangu kukiwa kumebakia mabeki wawili, mmoja ndio yule ambaye kocha aliniambia niwe naye makini. Mabeki hawa wawili wakanifwata kwa kasi sana, nikiwa katika harakati za kuwapita, kutokana na uwefu wa vimo vyao, nikahisi kisi kitu kizito kikinipiga kichwani mwangu na mzima mzima nikaanguka chini na giza nene taratibu likaanza kupoteza nuru ninayo iona kwenye mboni za macho yangu na baada ya sekunde kadhaa nikapoteza kumbukumbu.

ENDELEA
Vilio vya sauti ya Camila, vikaanza kuchukua nafasi kwenye ufahamu wangu wa akili, nikajaribu kuyafumbua macho yangu, ila sikuweza kuwaona watu vizuri, ila niliweza kumuona Camila pamoja na watu walio valia makoti meupe.
“Inabidi usubirie hapa, sisi tunaingia ndani”
Niliisikia sauti ya kiume, kisha nikaona muelekeo wa kitanda nilicho lalia ukibadilika, nikawaona madaktri wakisaidia kuniwe juu ya kitanda kingine, taa kubwa zilizo washwa, zikazidi kuyafanya macho yangu kushindwa kabisa kuweza kuona na kungundua ni kitu gani ambacho kinaendelea. Hali ya kusikia sauti za watu nayo ikaanza kupungua na mwishowe sikuweza kusikia kitu cha aina yoyote.
                                                                                                                 ***
    Nikafumbua macho yangu na kumuona Ethan rafiki yangu akiwa amesimama pembeni ya kitanda nilicho kilalia.
“Karibu tena duniani”
“Mbona upo hapa?”
Nilizungumza huku nikiandelea kutazama mazingira ya eneo hili.
“Nimekuja kukujulia hali kwani ni vibaya?”
“Hapaana, sasa hivi ni saa ngapi?”
“Saa nane usiku”
“Duu”
Nilizungumza huku nikihisi maumivu makali sana ya kichwa changu, nikajishika na kujikuta kichwa kikiwa kimezungushiwa bandeji kubwa.
“Kwa nini hukunisaidia, nilipo kuwa nina pata hii ajali?”
“Nilikuwa mbali”
 
Mlango ukafunguliwa na akaingia nesi mmoja, akanisogelea hapa kitandani pasipo kumuona Ethan.
“Unajisikiaje Ethan?”
“Kidogo nafuu japo kichwa kina nigonga sana”
“Pole sana mtoto mzuri utapona sawa”
“Sawa”
“Ugua pole na asubuhi daktari atakuja kukuona”
“Sawa nesi”
Nesi huyu akatoka na kuniacha na Ethan.
“Siku nyingine unatakiwa kuwa makini sana kwenye mpira”
“Ila uliniambia umenipa nguvi, la sijaona matumizi yake?”
“Kwa sasa nimekuambia kwamba muda wake bado. Ukifika wewe mwenyewe utaweza kuona ni kiasi gani cha nguvu na mamlaka ambayo unayo ila kwa sasa usiwe na haraka”
“Sawa”
 
Tukazungumza mambo mengi sana na Ethan, hadi majira ya asubuhi, akaondoka na kuniahidi kwamba atarudi mchana. Madaktari wakaingia ndani humu na kunijulia hali, wakanichoma sindano ya kupunguza maumivu na kunipatia vidonge. Nikawajaribu kuwadadisi ili niweze kutambu ni tatizo gani ambalo linanisumbua, ila hapakuwa na hata mmoja aliye weza kuniweka wazi na wakaniomba niweze kumsubiria wazazi wangu. 
Ilipo timu saa moja kamili bibi Jane Klopp na mume wake mzee Klopp wakafika hospigtalini hapa.
“Unaendeleaje?”
Mzee Klopp aliniuliza huku akionekana kuwa na wasiwasi nami.
 
“Naendelea vizuri tu baba”
“Pole sana mwanangu”
“Asante baba”
“Madaktari wamekuambia kwamba una sumbuliwa na nini?”
Bi Jane Klopp aliniuliza kwa sauti ya upole na iliyo jaa masikitiko.
“Hawajanieleza, jana niligongana na mchezaji mwenzangu na nikapoteza fahamu”
“Pole sana”
Daktari akaingia na akamuomba mzee waweze kwenda kuzungumza ofisini na hapa chumbani nikabaki na bibi Jane Klopp.
“Ethan kuna tetesi nimezisikia ila nahitaji kuzi dhibitisha kwako”
 
“Tetesi zipi?”
“Nilisikia kwamba jana mjukuu wa raisi alitaka kujiua na wewe ukamuokoa na yote ni kutokana ana kupenda?”
Nikastuka hadi bibi Jane Klopp akalitambua hilo.
“Sizungumzi hivyo kwa ajili ya kukuhukumu, hapana jambo la upendo ni la kila mmoja, si mkubwa na wala si mtoto. Wewe kupendwa si jambo baya”
“Ni kweli mama Camila alini……”
Kabla ya kuzungumza tukashuhudia mlango ukifunguliwa, akaingia mama Camila pamoja na mume wake. Bibi Jane Klopp akanyanyuka kitandanina kuwapokea kwa heshima sana, nikawasalimia wazazi wa Camila huku mama Camila akinikabidhi uwa zuri kubwa.
 
“Unaendeleaje?”
“Ninaendelea kidogo nafuu”
“Pole sana, jana kwa kweli tulipata mstuko mkubwa sana baada ya kuona ajali ile uwanjani”
“Naendelea vizuri”
“Jane huyu ni kijana wako?”
“Ndio nikijana wangu”
“Nina furaha sana kusika hivyo kwa kweli. Mzee Klopp akaingia ndani humu huku akiwa ameongozana na daktari. Wakasalimiana na wazazi wa Camila, daktari akanieleza kwamba nimepata ruhusa ya kuelekea nyumbani na atakuwa akija nyumbani kunitembelea.
 
“Kwa hiyo sinto rudi shule?”
“Hapana, inabidi upate muda mzuri wa kupumzika”
“Ila dokta hali yake si inaendelea vizuri”
“Yaa itakuwa vizuri maelekezo yote nimempatia mzee hapa”
“Sawa”
Taratibu za kutoka hapa hospitalini zikamalizika, tukaagana na wazazi wa Camila huku wakiniahidi kwamba jioni ya leo mtoto wao atakuja nyumbani kwetu kuniona. Tukaingia kwenye gari na safari ya kuelekea nyumbani ikaanza.
“Ethan kupata ajali kama hizi kwenye mpira ni jambo la kawaida sana, isije ikatoke ukachukia mpira”
Mzee Klopp alizungmza huku akinitazama usoni mwangu.
“Siwezi baba”
“Hivi unajua mzee wako naye zamani alikuwa ni mchezaji mzuri”
“Wee”
“Yaa alikuwa anachezea Dotmund”
“Tukifika nyumbani nitakuonyesha picha zangu kipindi nilipo kuwa mchezaji”
“Sawa”
 
Tukafika nyumbani, nikamkuta dada Mery sebleni, akanipokea kwa furaha tofauti na siku zote. Tukapata chakula cha mchana huku dada Mery akiniomba msamaha kwa yale yote ambayo yaliweza kutokea kwa siku za hapo nyuma.  Furaha na amani ikarudi katikati yetu. Mzee Klopp akaanza kunitembeza kwenye chumba chake ambacho kina picha na vifaa vyake vya zamani akiwa mchezaji toka alipo kuwa mtoto hadi umri ambao alimua kustafu mpira.
“Unataka kuniambia huyu alikuwa ni wewe?”
Nilizungumza huku nikiwa nimeshika picha moja, ikimuonyesha mzee Klopp akiwa kijana mdogo sana.
 
“Yaa ni mimi, nilikuwa ninacheza namba kama unayo cheza wewe, ila kabla ya hapo nilikuwa nacheza kama beki, ila nilipo jigundua kwamba nina uwezo wa kufunga, kupiga chenga na kumiliki mpira kwa muda mrefu basi niliweza kujibadilisha mfumo wangu wa uchezaji na kuwa mfungaji, hadi nina stafu ndani ya kablu ya Dodtmud nimefunga magoli mia tatu na tano na historia yangu haijavunjwa na mtu wa aina yoyote hadi sasa hivi”
“Duuu, ina maana huku hama timu?”
“Yaa nilianza kwenye timu hiyo nikiwa mtoto na hadi nikastafu. Nikawa kocha wa timu hiyo kwa miaka saba baada ya hapo niliamua kustafu na kuendelea na mambo yangu ya biashara”
 
“Safi sana baba”
Mzee Klopp akanikabidhi tisheti yake moja”
“Hii tisheti itunze ukikua utaivaa. Hakikisha kwamba jina la baba yako huliangushi chini”
“Nakuahidi nitacheza mpira kwa jihudi zangu zote”
“Nafurahi kusika hivyo”
Tukaendelea kutembea maeneo mbali ya jumba hili, hadi jioni, tukarudi nyumbani na tukamkuta Camila akiwa na mama yake pamoja na bibi Jane Klopp. Camila alipo niona hakujali kuna watu wazima, alicho kifanya ni kunikimbilia na kunikumbatia kwa nguvu. Mzee Klopp akanikonyeza kisha akaondoka.
 
“Unaendeleaje mpenzi wangu?”
“Kidogo ninajisikia nafuu”
“Vipi madaktari wamesema kwamba umeumia sana?”
“Hapana, nahisi ni mtikisiko tu”
“Kichwa hakiumi?”
“Hakiumi nilikunywa dawa asubuhi”
“Pole mwanya, yaani leo siku nzima nimeshindwa kusoma. Nilipoteza furaha kabisa mpenzi wangu”
Camila alizungumza huku tukielekea kwenye moja ya bustan yenye majani mazuri.
“Usijali vipi timu yetu ilifanikiwa kusonga mbele?”
Camila akatingisha kichwa kwa masikitiko akimaanisha kwamba timu yetu iliweza kufungwa na kutolewa kwenye mashindano. Habari hii kusema kweli ikanisononesha moyo wangu.
 
“Tulifungwa goli ngapi?”
“Tano mbili”
“Mmmmm”
“Yaani baada ya kuanguka wewe, timu nzima nasikia ilichanganyikiwa, wachezaji wakapoteana uwanjani, yaani nasikia kipindi cha pili kilikuwa kibaya sana kwetu”
“Duu”
“Yaani inaonyesha dhairi wewe ndio roho ya timu”
“Mungu akijalia mwakani tutaendelea”
“Ucheze vizuri ili usije ukapata ajali kama hii”
“Usijali mpenzi wangu”
Tukaa chini pembezoni mwa bwawa lililopo katikati ya bustani hii, taratibu Camila akanilalia begani mwangu na akaanza kuimba nyimbo moja nzuri ambayo kusema kweli ikaniburudisha moyoni mwangu.
                                                                                                                          ***
    Kadri siku zilivyo zidi kusonga mbele ndivyo jinsi penzi langu mimi na Camila lilizidi kupamba moto, si shule tu, hata mitaani penzi letu ziliweza kuzungumziwa na watu wengi. Wapo baadhi waliponda mahusiano yetu wakidai sisi bado ni watoto wadogo sana na wapo ambao waliweza kutupongeza na kutuombea mema kwenye mahusiano yetu. Muhula wa mwisho, Camila akashika nafasi ya kwanza darasani huku mimi nikishika nafasi ya kumi jambo ambalo kidogo liliniuma. Sikusita kumpongeza mpenzi wangu kwa juhudi alizo ifanya.
“Tukiingia darasa la pili hakikisha kwamba unashindana nami kwenye masomo sawa”
 
“Sawa mpenzi wangu”
“Nataka siku na wewe ushike nafasi ya kwanza ili watu waweze kujua kwamba hata nyinyi watu weusi munaweza kuwazidi wazungu akili na kinato tutofautisha hapa ni rangi za miili yetu tu”
Maneno ya Camila kusema kweli yakanihimiza sana na kunipa moyo na hamasa ya kupania nikirudi mwakani ni lazima nishindana naye kwenye masomo yetu.
“Nashukuru mpenzi wangu kusikia hivyo”
“Sawa kesho nitakuja kwenu tushinde siku nzima”
“Sawa”
 
Camila akaingia kwenye gari lililo kuja kumchukua, kisha na mimi nikaingia kwenye gari latu na safari ya kurudi nyumbani ikaanza. Katika kipindi chote cha likizo mzee Klopp alinifundisha mbinu nyingi sana katika upande wa uchezaji wa mpira.
“Kesho tutaelekea kwenye kituo cha timu ya Dotmud kwa ajiki ya kuanza mazoezi na watoto wezako. Ukifanya vizuri utasajiliwa haraka sana, nina imani hoto niangusha”
“Siwezi kukuangusha baba”
 
Nilizungumza huku nikiwa nimejawa na furaha sana moyoni mwangu kwa maana hii ni habari nzuri kwangu na kipaji changu kwa ujumla.Kama alivyo niahidi mzee Klopp siku iliyo fwata alfajiri na mapema tukaingia kwenye gari na kuelekea kwenye makao makuu ya timu hiyo. Wachezaji wakubwa na makocha wote wakaonekana kumpa heshima kubwa sana.
“Ethan”
“Ndio baba”
“Ukijitahidi kwenye maisha yako, hii ndio heshima ambayo utaipata, hapa uwanjani nimeacha heshima yangu na kuna sanamu lililo chongeshwa na kufanana na mimi, lipo nje ya uwanja pale, nitakuonyesha tukitoka”
 
“Lina maanisha nini hilo sanamu?”
“Ni heshima, hakikisha kwamba una vunja rekodi yangu na una endeleza uhodari wa jina langu”
“Sawa baba”
Tukaingia kwenye moja ya ofisi, na kuwakuta wazee wawili ambao wote wakamsalimia mzee Klopp kwa heshima, nikawasalimia wazee hawa kwa heshima.
“Nimeleta mkombozi mpya wa timu, sasa jukumu liwe kwenu sasa kumuendeleza”
“Anaweza kweli?”
“Mimi sio muongeaji sana, si vijana wapo uwanjani, twendeni tukamjaribu”
 
Tukaondoka ofisi humu na kuelekea kwenye viwanja vya mazoezi, nikakuta timu ya watu wakubwa wakicheza katika kiwanja chao, huku timu ya vijana wenye umri wa kati wakicheza kwenye uwanja wao huku kiwanja cha tatu wakicheza wachezaji wenye umri kama wangu wa miaka saba hivi. Nikawatazama watoto hao, nikaona wanacheza kawaida.
“Baba ninaweza kujiunga na vijana hao wakubwa wakubwa?”
Kauli yangu ikawafanya wazee hawa kunitazama kwa mshangao.
 
“Kijana ana omba fursa nawasikiliza nyinyi”
“Twende tukakuombee kwa kocha wa vijana”
Tukafika kwa kocha wa vijana, kocha alipo elezwa kwamba nina hitaji kucheza kwenye timu yake, naye akaonekana kushangaa kidogo.
“Ila anapaswa akaanze kule chini”
“Nina omba nikishindwa basi nina toka nitaenda kucheza kule chini”
 
Nilizungumza kwa kujiamini. Kocha kanitazmaa kwa mshangao, kisha kwa ishara akaniomba nivue suruali yangu ili niweze kupewa jezi ya mazoezi. Kutokana nilisha jiandaa kwenye swala la viatu, sikuwa na haja ya kuvua viatu. Nikavaa bukta inayo nitosha, pamoja na tisheti. Mwalimu akagawa vikosi viwili huku wezangu ambao nimechaguliwa nao kwenye kikosi ninacho chezea, walianza kulalamika kwamba mimi ni mdogo sana na wengine wakaenda mbali sana na kudai kwamba ninatakiwa kujiunga na watoto wezangu. 

Kocha msaidizi, akaanzisha mechi hii. Wachezaji wezangu wakawa wazito sana katika kunipatia mipira huku wengi wao wakionekana kuto kuni amini. Ikanilazimu nicheze kwa kujitegemea, nikaanza kukaba, nikafanikiwa kupata mpira, kasi na nguvu alizo barikiwa zikaniwezesha kuweza kuwapiga chenga wachezaji wa kiosic ha pili, na nilipo fika karibu na goli, nikapiga shuti moja zito, kwa bahati mbaya likagonga mwamba hadi mwamba ukatingishika na kumfanya kipa kunikodolea macho. Wachezaji wote wakabaki wakishangaa kwa uwezo wangu nilio uonyesha, nikamtazama mzee Klopp nikamuona akiniyooshea dole gumba. 
 
Tukaendelea kucheza mpira, wachezaji wa kikosi changu wakaanza kuniamini, na kunipatia pasi, katika mashuti sita niliyo piga golini, manne nikafunga na mawili yakagonga mwamba. Wachezaji wa timu kubwa, nikaanza kuwaona mmoja baada ya mwengine akijongea kwenye kiwanja chetu kutazama uwezo wangu.
Kitu kingine nilicho barikiwa, ninaweza kupiga chenga kiasi kwamba wachezaji wengine wanaogopa kunikabili kwani ninaweza kuwadhalilisha chenga zangu. Hadi mapumziko, nimefunga goli tano.
 
“Ethan”
Mzee Klopp aliniita, nikatoka uwanjani na kusimama mbele yao.
“Inatosha mwanangu, sasa wazee munaweza kuzungumza biashara hapa hapa, nimewaletea Klopp Jr ambaye atarudisha heshima ya timu na vikombe sasa vitaanza kurudi kwenye club yetu siku si nyingi. Wazee hawa wakabaki midomo wazi huku kila mmoja akiwa hana usemi.
“Huyu kijana ni nani?”
Kocha wa timu kubwa aliuliza huku akinitazama.
“Ninaitwa Ethan Klopp”
“Klopp ni mwanao?”
“Ndio”
“Nimeona kitu kikubwa ndani yake, kitu ambacho kusema kweli sinto hitaji kukipoteza”
“Bora na wewe umeona, wezako hapa wana shangaa. Sasa tuzungumzeni biashara, munamsajili au niondoke na kijana wangu akawe zao la timu nyingine”
“Weee tukikataa nahisi tutakuwa wendawazimu, mtu unaona kwamba tumeletewa Mess alafu tumkatae. Klopp mimi nipo tayari mkusajili”
 
“Kiwango cha chini ni paund milioni kumi kama munapesa tuingie mezani, ila kama hamuna kesho nina panda naye ndege ninaelekea naye Hispani na huko munafahamu kuna mapapa wakubwa R. Madrid na Bacelona”
“Klopp kumbuka wewe hapa una heshima, usitufanyie hivyo bwana?”
“Nina heshima, ila huku anakwenda kuvunja rekodi na heshima yangu, siwezi kumuachia bure kwa maana ni zao langu hili na si lenu”
Mzee Klopp aliendelea kushikilia msimamo wake wa kuhitaji kuniuza katika timu hii jambo ambalo ni jema sana kwenye maisha yangu ya mpira nikiwa bado ni kijana mdogo wa miaka saba.

==>>ITAENDELEA KESHO


from MPEKUZI

Comments