Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 08

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA  

“Angalia mlangoni”
Nikatazama mlangoni, sikuona kitu chochote, nikageuka kumtazama katika sehemu ambayo alikuwa amekaa, ila sikumuona, nikastukia mlango ukifunguliwa, akaingia mzee mmoja aliye valia suti nzuri huku akiwa ameongozana na walinzi huku mkono wake wa kulia akiwa ameshika Camila ambaye usoni mwake ana mwagikwa na machozi. Nikanyanyuka kwa haraka kitandani na nikamsalimia mzee huyu kwa heshima sana, ila sura yake ikaonyesha kukasirika sana, na kwa haraka nikaweza kumtambua kwamba huyu ndio raisi wa hapa Ujerumani kwa maana picha yake ipo katika ofisi ya mkuu wa shule na waalimu wengine.

ENDELEA
“Wewe ndio kijana unaye itatiza akili ya mjukuu wangu?”
Mzee huyu alizungumza kwa ukali sana hadi mimi mwenyewe nikaanza kutetemeka huku machozi yakianza kunilenge lenga.
“Ninakuonya mtoto, kaa mbali na mjukuu wangu la sivyo hii nchi utaiona mbaya, na wewe umekuja shule kusoma na si kuingia ingia kwenye mabweni ya wanaume umenielewa?”
Camila akatingisha kichwa huku akiendelea kumwagikwa na machozi usoni mwake. Mzee huyu akanitazama kwa muda kidogo kisha wakatoka ndani humu na walinzi wake. Mwalimu wangu wa darasa akaingia huku akiwa amejawa na sura ya huzuni. 
 
“Ethan”
“Naam”
Niliitikia kwa sauti ya unyonge sana huku nikimtazama mwalimu wangu huyu ambaye ana nipenda kutokana na kipaji changu cha mpira uwanjani.
“Una mahusiano na huyu binti?”
Mwalimu aliniuliza kwa sauti ya upole sana huku akiwa amekaa kitandani, kwa uoga nilio nao nikajikuta nikishindwa hata kuzungumza zaidi ya kuanza kulia. Taratibu mwalimu akanivuta jaribu yangu na kunikumbatia na kuanza kunibembelea kwani habari hii ikifika kwa bibi Jane Klopp na mume wake sijui watanichukuliaje.
“Usiwe karibu na yule binti sawa”
“Sawa mwalimu, ila ni rafiki yangu tu wa kawaida?”
“Ndio nina litambua kwa umri wako huwezi kuwa na mahusiano ila muheshimiwa alikuhisi tu vibaya, ila nakuomba usipende kuwa naye karibu sihitaji kukupoteza kwenye darasa langu”
 
“Sawa mwalimu”
Mwalimu akaniachia huku akinitazama usoni mwangu. Akaniomba niweze kujipumzisha na nisitoke ndani humu hadi kesho. Mwalimu alipo ondoka rafiki zangu wakingia ndani ya chumba hichi huku nao wakiwa wanahitaji kufahamu ni kitu gani ambacho kimetokea hadi raisi kunifwata humu bwenini. Kwa mtazamo wa haraka haraka wengi wao wanahisi kwamba raisi amekuja kunipongeza kwa kufanya vizuri kwenye mechi yangu ya kwanza tu.
“Ethan unazidi kuwa maarufu”
Wezangu walizidi kunipongeza huku wakiwa wamejawa na fur asana, ila laiti kama wangefahamu kwamba nimetoka kufokewa tena na mkuu wa nchi yao wala wasinge zungumza lolote juu yangu.
                                                                                                                      ***
    Umaarufu wangu katika shule hii ukazidi kupanda siku hadi siku. Michuano ya mpira madarasa ya shule hii ya msingi yakazidi ninifanya nizidi kuwa kipenzi cha wanafunzi na waalimu wengi. Kwani nikiwa kama kapten wa timu yangu, ya darasa la kwanza, niliweza kuingoza timu yangu katika kila ushindi tulio upata katika mechi za madarasa tulizo kutano nayo. Katika safu ya ufungaji, niliongoza kwa magoli ishirini na sita huku anaye nifwatia akiwa na magoli kumi. Katika kipindi chote sikuhitaji kukaa karibu na Camila na kila nilipo muona ana kuja nilipo kwa ajili yangu, nilifanya kila ina ya mbinu kuhakisha kwamba nina mkwepa.
“Ethan”
Niliitwa na msichana mmoja tukiwa uwanjani tunajiandaa na mechi ya kucheza na darasa la sita.
 
“Ndio”
“Kuna ujumbe wako hapa”
“Kutoka kwa nani?”
“Wewe chukua”
Msichana huyu alinipa ujumbe huu, nikataka kuusoma ila mchezaji mwenzangu aka nizuia kwa maana tumebakisha dakika chache sana kabla ya kuingia uwanjani. Ujumbe huu nikauingiza kwenye soksi zangu za mpira kisha nikaingia uwanjani. Mwalimu akaniita kwa ajili ya kunipa maelekezo yake kama kocha.
“Una muona yule mwenye macho ya blue kiasi?”
Mwalimu alizungumza huku akinionyesha mchezaji wa darasa la sita.
“Ndio”
“Yule ni beki wao, na anacheza rafu anaweza hata kukuvunja. Hakikisha kwamba unakuwa makini naye sawa”
“Sawa mwalimu”
 
“Ushindi ni muhimu, kumbuka tuna mechi moja mbeleni, tukishinda hii ya robo fainal, najua tutakao kutana nao nusu nilazima tutawafunga na tutaingia fainali”
“Sawa kocha”
Nilizungumza huku nikiangaza angaza macho yangu katika kumuangalia ni wapi alipo Camila, ila nikashindwa kabisa kumuona jambo lililo nipa wasiwasi mwingi sana, japo ninamkwepa ila moyo wangu una niuma sana. Nikamuona mlinzi mmoja wa Camila akifika katika eneo hili kwa kasi sana, akamnong’oneza mwalimu jambo amalo hata mwalimu mwenyewe akaonekana kustuka kidogo. Mwalimu akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha aka ninong’oneza.
“Nakuomba uongozane na huyu mlinzi kuna jambo la muhimu sana limetokea, ila hakikisha kwamba unatumia kila mbinu unalitatua na unarudi hapa kiwanjani sawa”
“Sawa”
 
Nikavua kitambaa cha muongozaji wa timu(capten) na nikanza kukimbia na mlinzi huyu, jambo ambalo kidogo likawastua mashabiki walio weza kuliona tukio hilo. Tukakimbilia hadi kwenye mabweni ya wasichana na nikawakuta baadhi ya waalimu na wazazi wa Camila wakiwa chini ya gorofa hili huku juu kabisa akiwepo Camila mwenyewe akihiyaji kujirusha kutoka gorofani hapo ili afe. Hapa ndipo nikawazia juu ya ujumbe ambao nilipatiwa na sikuusoma.
“Wewe ndio Ethan?”
Mama Camila aliniuliza huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Ndio ni mimi”
“Ninakuomba umsaidie mwanangu, nakuomba mwanangu ana kuhitaji wewe tafadhali nakuomba sana kijana”
Nikasimama katika sehemua mbayo Camila ambayo anaweza kuniona, nikamtazama.
“Camila……Camil”
 
Niliita kwa sauti ya kuu na Camila akanitazama.
“Panda juu ukazungumze naye tafadhali”
Baba Camila alizungumza huku naye akionyesha dhairi kwamba ana wasiwasi mkubwa sana. Nikaanza kupandisha ngazi za gorofa hili huku nikikimbia, nikafika gorofa ya nane na nikapanda juu kabisa alipo Camila, nikamakuta akiwa amesimama kwenye ukingo wa gorofa hili na endapo atafanya mchezo kidogo basi anaanguka chini na kufa.
“Camila, kwa nini unataka kufanya hivyo mpenzi wangu”
“Ethan kaa mbali na mimi, hunipendi”
Camila alizungumza kwa ukali sana.
“Ninakupenda Camila, nina kuhitaji mpenzi wangu”
“Kwa nini ushindwa kupigania penzi letu. Ninakufwata ila unanikimbia kimbia, ni maisha gani ambayo unanifanyia lakini eheee?”
 
Camilia alizungumza huku akilia sana, kwa umri ambao tunao hakika haistahili kwa sisi kuwa na mapenzi ya namna hii, kusema kweli Camila ana nipenda hadi anaamua kutaka kujiua kwa ajili yangu.
“Hapana Camila, nina ogopa. Baba yako anaweza kunidhuru, je unataka nife ehee?”
“Acha nife mimi kama unaogopa kufa”
“Hapana Camila, sihitaji ufe. Nina kuapia kwa mwenyezi Mungu kuanzia leo wewe ni wangu, hakuna ambaye atatutenganisha, nife mimi au ufe wewe, ila wewe ni wangu Camila”
Nilizungumza huku machozi yakinimwagika usoni mwangu, nikaanza kutembea taratibu huku nikimfwata Camila alipo simama.
“Camila na kuomba usifanye hivyo mpenzi wangu, nakuomba sana.”
 
“Ethan wewe hunipendi una nidanganya”
“Nakuapia haki ya Mungu nipo tayari kwa lolote, nina kupenda sana Camila wangu”
Niliendelea kuzungumza huku nikipiga hatua za taratibu hadi nikafanikiwa kufika sehemu alipo simama Camila, taratibu nikampatua mkono wangu wa kulia huku nikiendelea kumtazama usoni mwake.
“Camila, nipo tayari tukue pamoja, tuje kuishi pamoja na kuzaa watoto pamoja. Nitakuepeleka kwetu Tanzania, ukaona mazingira mazuri ya nchi yetu nakuomba sana Camila wangu tafadhali.
Camila akanitazama kwa macho yake mazuri, akashusha pumzi taratibu.
“Una niahidi nini?”
“Tayari nimesha kuahidi mengi mpenzi wangu”
“Nataka kusikia upya”
“Nakuahidi kuwa na wewe, nakuahidi kuishi nawe, nakuahidi kukupeleka kwetu Tanzania, nakuahidi kupigania penzi letu, nina kupenda sana mpenzi wangu”
“Upo tayari kusimama mbele ya babu yangu na kumuambia kwamba una nipenda?”
“Ndio nipo tayari”
 
Nilijibu ili maradi kumridhisha, ila kusema kweli sina ujarisi wa kusimama mbele ya mzee huyu mkali sana, na nimuambie kwamba nina mpenda mjukuu wake. Camila akanivuta mkono wangu na kuanza kushuka kwenye ukingo huu wa gorofa. Tukakumbatiana kwa nguvu, Camila akaanza kunibusu mdomoni mwangu bila ya kujali kwamba tupo katika eneo la shule.
“Nisikilieze mpenzi wangu, uwanjani mechi imesha anza, ninakuomba twende ukanishangilie mume wako”
“Kweli mpenzi wangu?”
“Ndio”
“Na leo nataka ufunge magoli matano mpenzi wangu”
“Sawa, kwa ajili yako nitafunga”
“Nakupenda sana Ethan”
“Nakupenda pia Camila wangu”
Mlango wa eneo la huku juu ukafunguliwa, akaingia baba mama Camila kisha akafwatia mke wake pamoja na walinzi wao. Wote wakashangaa ni ushawishi gani ambao nimeufanya kwa binti yao hadi kugairi kujiua.
 
Camila akaniachiana kukumbatiana na wazazi wake.
“Tunashukuru sana kijana”
Alizungumza baba Camila huku akinitazama usoni mwake.
“Sawa sawa mzee”
“Wazazi wangu, naomba mumuambie babu, nina mpenda Ethan, ninataka awe ndio mwanaume wa maisha yangu, sijali ni muafrika au ni mweusi na wala sijali utoto wetu, ila ninampenda, naomba musikilize hisia zangu wanazai wangu”
Camila alizungumza huku machozi yakiendelea kumwagika. Walimu nao wakafika katika eneo.
“Tutamueleza na sisi ndio wazazi wako, sisi ndio wenye maamuzi juu yako na si baabu yako. Tupo tayari uwe na huyo kijana kwa maana hatujaona ubaya wowote kwake kwanza ni handsome boy”
Mama Camila alizungumza huku akinikonyeza. Nikatabasamu huku nami nikiwa nimejawa na furaha.
“Kweli mama?”
 
“Asilimia mia moja”
“Asante mama na baba nina wapenda sana”
“Tuahidi hauto fanya hili jambo tena?”
Baba Camila alizungumza huku akimtazama mwanaye usoni
“Sinto lifanya nina waahidi wazazi wangu ila mukinitenganisha na Ethan kwa namna yoyote basi nitajiua”
Camila alizungumza kwa msisitozo na wazazi wake wakaka kimya.
“Mpenzi wangu ni mchezaji mpira, na timu yake ipo uwanjani, twendeni tukamshangilie”
“Sawa twendeni”
Tukaondoka juu ya gorofa hili na kuelekea uwanjani. Tukiwa karibu ya uwanjani tukasikia shangwe kubwa ambazo zikanifanya nikimbilie uwanjani. Nikatazama ubao wa magoli, nikaona timu yangu ikiwa imefungwa goli mbili bila na goli hili la pili ndio limetoka kuingia muda si mchache. Mwalimu alipo niona akatanasamu sana kwani timu inacheza kwa kuto kujiamini na nina amini kwamba wachezaji wezangu watakuwa wakijiuliza ni wapi nilipo elekea na ni kitu gani ambacho kilinipata hadi nikaondoka kabla ya mechi kuanza.
“Umefanikiwa?”
 
“Ndio mwalimu yule pale na wazazi wake”
Nilizungumza huku nikimuonyesha alipo Camila na wazazi wake.
“Sawa anza kupasha”
Nikaanza kukimbia kimbia pembezoni mwa uwanja na kuwafanya mashabiki wa darasa langu kuanza kushangilia, wachezaji wezangu walipo ndani ya uwanja walipo niona nao wakaanza kupata hamasa ya kucheza kwa juhudi. Nikawatazama wakwe zangu, nao nikawaona wakiwa wamkini sana wakifwatilia mpira huu huku wakiwa wamekaa kwenye jukwaa maalumu la wageni rasmi, kocha akaniita.
“Kiungo kimepwaya, na hata ngome yao ni ngumu sana kuipita yule beki niliye kuonyesha ana cheza namba tano, hakikisha kwamba unakuwa naye makini”
“Sawa mwalimu, zimebaki dakika ngapi kabla ya kipindi cha kwanza kuisha?”
“Dakika kumi”
“Sawa”
 
Yakafanyika mabadiliko, akatoka mshambuliaji mmoja kisha nikaingizwa mimi. Uwanja mzima ukarindima kwa shangwe, kila mtu akafurahi uwepo wangu uwanjani. Hofu ikaanza kuwapata wachezaji wa darasa la sita, mimi na rafiki yangu Rafael ambaye huwa tunaendana sana kwenye swala la uchezaji na ushambuliaji, tukaanza kupeleka mashambulizi ya kasi sana kwa darasa la sita. Ndani ya dakika nne, Rafael akafanikiwa kufunga goli la kwanza huku pasi ya goli hilo ikitokea kwangu. Nikamuona jinsi Camila anavyo shangili huku akinipungia mkono.
“Tunaweza kurudisha?”
 
Niliwahimiza wachazaji wezangu huku nikipotea kitambaa cha kuongoza timu kutoka kwa golikipa. Mpira ukaanza kwa kasi ya ajabu huku wachezaji wezangu wakijitahidi kwa hali mali kuhakikisha kwamba tunakomboa hili goli moja lililo sali, nikafanikiwa kupata mpira huku mbele yangu kukiwa kumebakia mabeki wawili, mmoja ndio yule ambaye kocha aliniambia niwe naye makini. Mabeki hawa wawili wakanifwata kwa kasi sana, nikiwa katika harakati za kuwapita, kutokana na uwefu wa vimo vyao, nikahisi kisi kitu kizito kikinipiga kichwani mwangu na mzima mzima nikaanguka chini na giza nene taratibu likaanza kupoteza nuru ninayo iona kwenye mboni za macho yangu na baada ya sekunde kadhaa nikapoteza kumbukumbu.

==>>ITAENDELEA KESHO


from MPEKUZI

Comments